Manchester United (Red Devils) | Special Thread

anthony martial amekanusha taarifa zilizotolewa na ralf ya kwamba hataki kuitumikia. martial anasema amekuwa muaminifu kwa takriban miaka 7..... vita imeanza
Watoto wameshaanza kujipambanua
Bado Rashford naye atajitokeza
Ugonjwa wa Manure ndio huo Ole aliwabembeleza sana
MOU alipotaka kuwabana watoto walishinda akatimuliwa
Ole kaja mbembelezaji kaendana nao akashindwa
Huyu kocha anachotakiwa ni kuwauza au kuwaweka benchi mpaka akili zao zikomae
 
Zamani kidogo ilikuwa mtaa wa sita FC lakini hata hiyo siku hizi imekuwa shida kuipata.
alichokosea ralf ni kuendelea kumtegemea cavani kwa mechi ya jana, nafikiri diamond formation lilikuwa ndio suluhisho kwa dakika 20 za mwisho kama alivyofanya mechi ya juzi alipomuingiza donny. ralf anasema tatizo linalomuumiza zaidi ni kushindwa kumiliki mpira tunapokuwa kwenye transition, kiwango chetu cha kumiliki mpira hakiridhishi.
 
Martial ni mmoja wa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa hapo kwenu na hatuoni anachoifanyia timu, weka benchi hadi aondoke mwenyewe
Ndio ninachokisema, wamuuze tu hana tena morale ya kucheza na akili yake inawaza kusepa, hizi nyingine mboyoyo tu anajitetea, RR maybe kaangalia wachezaji wanaotaka kucheza, mtu kashaomba kuondoka bado upambane kumweka 1st 11 wa nini?

Fatilia situation ya Halland na Dortmund kama alivyoreport Fabrizio jana, Dortmund wanataka Halland adecided future yake sasa hivi ili waanze msako mapema wa replacement, Man U Martial kasema anataka changamoto mpya ila board ipo tu sidhani kama hata kuna mipango ya kuangalia eneo hilo, nilisikia wanataka kumtoa Amad kwa mkopo, Sancho mwenyewe unga unga mwana jana kajaribishwa Elanga ngoja tuone
 
Kuna ile footage ilisambaa ya mazoezini Pogba na Mourinho wanataka kupigana hiyo ndio tabia iliyopo huko, Mou alikaza na ndio maana alifanikiwa, hakucheka na players japo board ikamtimua baadae, taratibu watajitoa mmoja mmoja mapangoni, RR akaze hapo hapo, msimu tushaharibu huu, tukubali tu ila tuanze na matatizo mapema kama tunataka mabadiliko baadae au msimu ujao
 
lakini huyu ni kocha wa muda hivyo sidhani kama ana muda wa kufanya hayo yote kwa dirisha dogo. changamoto nyengine ni kuwa na wachezaji wenye mishahara mikubwa jambo linaloleta ugumu kuwauza wachezaji.
 
na ndio tuliowajaza. muda huu chini ya ole tungelikuwa tunamgombania trippier na declan rice. chini ya ralf tunamlenga tchouameni, neves na zakaria kwa dau lisilovuka paundi million 90 kama utawataka wote. kumbuka hiyo hela tulilipa kwa maguire pekee

Tulitakiwa tuibe management toka Bayern au Ajax tuje kujenga timu.

Huyu DoF na Fletcher ni empty heads.

Mishahara ilitakiwa ishuke kwa 50%. Increament ilitakiwa iwe by merit system.
 
lakini huyu ni kocha wa muda hivyo sidhani kama ana muda wa kufanya hayo yote kwa dirisha dogo. changamoto nyengine ni kuwa na wachezaji wenye mishahara mikubwa jambo linaloleta ugumu kuwauza wachezaji.
Bodi inataka kumtoa mkopo na timu itakayomchukua ilipe mshahara wote na gharama za mkopo. Hakuna timu itakayofanya hivyo, PSG?? ila imesheheni fowards wengi. In this planet, no other teams will accept Man U Loan conditions for Antony Martial
 
Namuona hata Jamie Callagher anavyochambua na kuguswa na matatizo yetu united kuliko legends wetu wengi,kuna wakati huwa naona kama rivalry yetu ni ya kimauzo zaidi kuliko uhalisia.
Sisi liverpool ni ndugu zetu zaidi kuliko man city.
 
Wachezaji wa United bado mentality zipo kama wapo chini ya Ole.

Hakuna kocha anaeweza badili attitude wachezaji aina hii.

Na hii imetokana na Man Utd kukosa proper structure ndani ya uwanja. Kila kocha anapokuja ni kama tunaanza upya.

Ilitakiwa itengenezwe falsafa ya timu then aajiriwe kocha based on already established system.

Ole ndo ameiharibu United. Laissez faire attitude imewafanya wachezaji wajione ndo mafaza. Wapewe mishahara mikubwa ila wacheze kwa kujisikia.
 
Tatizo unawaweka benchi almost wote mpaka unakosa kikosi.

Midfield ina shida kubwa sana. Utamuweka nani benchi na nani aanze?
 
Bodi ya Man Utd ndo mzizi mkuu kwenye matatizo tunayopitia.
 
Dirisha lijalo inatakiwa kuwaweka sokoni wachezaji kama 10 hivi.

Iwe fundisho kwa wengine wote mayai, kwamba usipo deliver unaoneshwa mlango wa kutokea.

Na mishahara ipigwe panga kwa nusu wakati wa kurenew mikataba, kama hutaki anza safari mapema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…