Juzi baada ya kuifunga Burnley (BURNLEY) Sista mmoja akatuma screenshot akazungushia na kaduara kumaanisha wana mechi mkononi na wakishinda mechi ijayo (Hii ya Wolves) anakua nyuma ya mshika namba 4 na akishinda ijayo anakua namba nne.
Sasa mimi nasema mwambieni SISI TULIO NAMBA NNE tumekubali kumpa points tatu za kiporo chake kisha alete screenshot ya msimamo tujue kama atakua kaifikia namba nne.
Next game ni dhidi ya Villa, mnaanza nao kwenye Carabao kisha ligi, mtatia aibu mkipotezwa kote kuwili.
Also clean sheet bado ni msamiati. Hawa ni wale walikua wakishangaa bei ya White wakawa wanasema Varane ameshinda makombe mengi yeye na Maguire watatengeneza ukuta umetulia.
Varane anapokea 340K back four ya Arsenal inapokea 310K lakini tunajua ni ukuta wa dunia ndiyo unasumbuka kupata clean sheet against Newcastle, Wolves, Burnley and the like