Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Aisee umemjibu kisomi na kiufundi kabisa huyo mshamba
 
Labda tunamtafsiri vibaya Bruno.

Inawezekana kutokushangilia kwake alifanya hivyo kuonyesha sadness kwamba manager aliyemleta pale amekua sacked.

Ukweli anaujua yeye. Tusi judge
Tatizo tuna judge sana wachezaji kwa kuwaangalia, muda mwingine tunauchukulia mpira kama tunacheza play station au PES vile, wachezaji nao ni binadamu wanapitia mengi na wana hisia pia, mchezaji unaeza kuta hata mama yake anaumwa anaona sio issue kushangilia sisi tukajudge anataka kuhama
 
Kuna kitu nimekiona kuhusiana na kikosi chetu.
Wenda Carrick anayajua matatizo ya beki zetu za kati ndio maana kaamua kuja na viungo wengi wa kabaji ili kuwalinda akina Bailey.

Nilianza kulaumu kikosi, lakini ghafra nimebadili msimamo, kikosi kiko poa kuliko tunavyo dhani.
 
Sasa hivi bado hamjamuelewa vizuri carrick

Subiri dakika za 70 mkianza kutuma matusi humu, ndio mtakua mmemuelewa
 
Kujifariji
 
Kwa upangaji wa kikosi kwa mechi ya leo,ninaona kabisa Carrick anaudhubutu wa kujaribu mbinu na wachezaji kulingana na adui anayemkabili kuliko Ole. Kwa hili nampongeza bila kujali matokeo yatakuaje hapo baadae.
Au kuna mkono wa Don Rangnick?
Na mm nmehisi hvyo, Rangnick anahusika, nahisi ndio formula tutakayoitumia hii. Alafu naona kabisa Carrick ataendelea kuwa kocha msaidizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…