Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mbona edwoord alisha resign long time mkuu? Hivi Fletcher unajua anafanya kazi gani pale man united kweli?
 
Diego Simion aachane na Atleti? Kuwa serios mkuu..
 
Nimeona sehemu kuwa baada ya kuachia nafasi ya CEO,bwana ED atateuliwa kuwa consultant wa klabu ingawa sijajua kwenye eneo gani. Hapa inaonekana mjinga atakuwa anaiongoza UNITED nyuma ya pazia bila kuguswa na mashabiki.
 
Hivi Poch anatofauti gani na Ole mkuu?
Poch kuanzia southampton hadi Tothenham alijenga vikosi vizuri sana na timu zake zilicheza mpira mzuri sana.....tofauti ya Ole na Poch ni kuwa mmoja alifikisha final timu akiwa hajasajili kwa misimu 2 (spurs vs liverpool)....

Pia Tot walikuwa wanacheza mpira mzuri sana chini ya Poch japo falsafa yake haipo clear yani haieleweki kama ni pasi au nini..
.....japo ni attacking football ila haipo well organized kiasi hicho.....

tofauti nyingine ya Ole na Poch ipo katika technical ability haswa tactic yani wanacheza sawa tu ila poch anapata kilichobora kwa wachezaji kuliko ole pia anajua kutumia wachezaji kulingana na ubora wao.....

siunakumbuka dele ali alipanda bei hadi paund mil 100 haha..

anaejua atatuelewesha zaidi.
 
Huyu Ralf amewahi kufundisha timu ipi zaidi ya kuwa DoF pale Red Bull Liepzig .?
RB Leipizig, Schalke, Hoffenheim, Hannover 96.

Nilimfahamu 2004 alipoichukua Schalke 04 kutoka kwa kocha niliyekuwa nampenda nikiwa mdogo Jupp Heynckes kwa ssb ya kazi yake Real Madrid. I was curious ni nani huyu anambadili Jupp pale Schalke kipindi hicho. Huu msimu Schalke wali-challege bundesliga walimaliza wa pili na walibeba kombe la ligi.
 
Mbona edwoord alisha resign long time mkuu?
Ed Woodward didn’t resign, he announced that he would be leaving his post at the end of this year. Kwa kifupi bado yupo ofisini. Anajiandaa kuchukua nafasi mpya kama mshauri mkuu wa timu.
Hivi Fletcher unajua anafanya kazi gani pale man united kweli?
Technical director.
 
Wenyewe wanasema ndiye alifanya mapinduzi ya mfumo was Gegenpressing na pia ndiye mentor wa hiki kizazi kipya cha makocha waliowahi kufundisha bundesliga kama vile Thomas Tuchel, Julian Nagelsmann, Ralph Hasenhuttl na Jurgen Klopp.

Simuoni kama ni mwanadamu atakayehimili na kuvumilia udhaifu wa bodi yetu yenye tatizo la kutake action kwa haraka pale panapohitajika kufanywa hivyo.

Huyu mzee atatusaidia sana maeneo yote mawili ambayo bado yanaendelea kufanya vibaya, eneo la kwanza ni la ndani ya uwanja kwa kuimplement structure inayoeleweka kiuchezaji bila ya kujali mchezaji gani yupo uwanjani, eneo la pili ni recruitment kwa kutafuta wachezaji sahihi na wenye uwezo kwa bei nafuu watakaoweza kuingia kwenye mfumo kwa haraka.

Kuna mifano tele ya wachezaji waliopitia kwenye mikono yake akiwa kama kocha na hata DOF ambao wanafanya vizuri mpaka muda huu kwenye mchezo we soka kama vile sadio mane, werner,keita, firmino n.k

Tujaalie umeshamkabidhi ajira ya muda mfupi mzee rangnick, baada ya kuondoka kwake unachukua hatua gani?

Unadhani bodi itakwenda kuwatafuta wanafunzi wake na kuwapa timu au itaendelea kucheza squid games ili mradi Siku ziende.

Kwa ufupi hii bodie yetu itaelewa somo la urithi wa structure ya kiuchezaji kutoka kwa mwalimu A to B.
 
Umemuelezea vizuri kweli Jombaa. Huyu jamaa inaonekana ni mtu mwenye mikakati na endapo ataichukua timu kipindi cha mpito ni rahisi sana yeye kuwa very instrumental ktk kutafuta kocha mpya kwa utulivu.

Baada ya hapo apewe nafasi ya mkurugenzi wa ufundi huyu jamaa John Murtough ni puppet tu wa mfumo uliopo ktk timu. Sijaona mahala popote pale ambapo yeye ama-recommend Ole kuondolewa.
 
  1. Wote wanaelekea kushindwa kuziongoza timu kubwa walizokabidhiwa(ole na poche)
  2. Mmoja amejijenga vizuri sana kupitia timu ndogo alizozifundisha ndio maana vilabu vikubwa vilimuona ni chaguo sahihi litakoloweza kuwaletea mafanikio bila ya kujali kiwango cha bajeti watakachompa kwa sababu huko nyuma alishaprove uwezo wake wa kufanya kazi kwenye mazingiraduni ukilinganishana yale ya timu kubwa zenye wage bill ghali, hapo namzungumzia Mauricio pochettino
  3. Mmoja alishindwa hata kujijenga kwenye timu ndogo aliopewa kwenye ligi iliojaa ushindani, nafikiri aliishusha daraja.
  4. Mmoja hategemei individual brilliance kwenye kuyasaka mafanikio ndio maana yupo hapo alipo, mwengine alibebwa na Bruno kwa kipindi kirefu ndio maana ni nadra kumweka nje anapoperform vibaya.
  5. mmoja hawezi kumanage kikosi chake kwa kuwafanya wachezaji wote ni sawa, kwa mfano wiki iliopita baada ya maechi ya Atalanta unaambiwa rashford hakufanya mazoezi kwa sababu ya injury lakini Siku ya jumamosi alikuwepo uwanjani vile vile rejea mfano wa maguire, Donny, Bailly, lingard, telles.
  6. Tactics nitahitaji uwanja mpana wa kuandika na kwa kipindi hiki haiwezekani,sijazoea kuandika kwa kutumia simu
  7. Mmoja hata kama atafukuzwa kazi leo ana uhakika wa kurudi tens kibaruani Ila Huyu mwengine ndio utakuwa mwisho was career yake kwa vilabu bora pale ulaya.
  8. Pochettino haiwezi Manchester united
Nimeona niongezee hayo
 
  1. Pochettino haiwezi Manchester united
Kama ambavyo mimi huwa simuelewi Poch kwenye suala la mbinu na team management ndio maana naona ni mara 10 kumchukua Rodgers kuliko yeye. Msimu wake wa mwisho pale Spurs,timu ilikuwa inaelemewa kwa kila kitu lakini jamaa hata hastuki,ni heri ya Ole huwa anachungulia ka screen kake upande wa kushoto kutafuta maneno ya kutudanganya kwenye mahojiano.

Kumleta Poch United ni sawa na kujihakikishia miaka 3 mingine ya kusubiri treni bandari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…