Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Why ufanye double change ?
Yah kwakuwa aliyetoka alikuwa ni beki kwahiyo tunatoa kiungo mmoja tunaingiza beki, zen tunatoa kiungo mwengine ambaye hana kasi (vdb) tunaingiza Greenwood, lengo ni kuhakikisha tunatawala mpira cz njia nzuri ya kujilinda ni kumiliki mpira na sio kukaba.
 
Peleka cv ukachukue nafasi ya OLE SENDEKA
 
Nafikri hakukuwa na sababu kabisa ya kumtoa Sancho ndani.

Alitakiwa afanye Sub ya mtu mmoja kwenye midfield kwa sababu walikuwa wanne uwanjani na wote wanacheza role zinazofanana karibu wote.
Pogba, Bruno, VDB na Fred hapa ndiyo alitakiwa kufanya sub

Najua kwanini Ole hakufanya sub kwenye midfield mtu ambaye alikuwa option ya kwanza kutolewa ni Donny mwalimu hakufanya hivyo kuepuka kelele zinazopigwa nje kuwa hampi gametime Donny ila alitakiwa kutoka huyo tu then baada ya muda unaingiza Greenwood kulia.

Kosa la pili ilikuwa ni kuwatoa Bruno na Ronaldo at once kuwatoa hawa ilikuwa ni kuwapa advantage Youngboys yakutokuwa na threat yoyote golini kwao na yeye pia kujinyima magoli ya set pieces pamoja na counters.

Kibaya sana unafanya sub kuingiza Lingard na Martial over Bruno na Ronaldo.

Kifupi jana kocha kadhihirisha wazi kuwa yeye ni PE teacher
 
 
 
Msijari mtabeba kikombe cha uji
 
Hahahahah! Leo umemuita Ole PE teacher, humtetei tena?

Binafsi zile sub mimi naona alijikoroga mwenyewe ila pamoja na threat ya Ronaldo kule mbele bado Young Boys walitupigia mpira safi tu ni kwasababu yetu ya kukaa nyuma. Goli la kwanza ni uzembe wa timu nzima wakiongozwa na kocha wao kucheza kwa kujilinda, tukawapa nafasi ya wao kuvuka mstari bila wasiwasi kwasababu kule mbele alibaki mtu mmoja waliyemdhibiti na wale jamaa angebaki mule wangemuumiza walianza kumchezea hovyo hata akiwa hana mpira.

Ronaldo alitoka uwanjani Young Boys wamesawazisha, kama nilivyosema Ronaldo kubaki peke yake mbele ilikuwa siyo msaada watu walisham-mark. Ole alichofeli ni kucheza kwa kujilinda na kuwatoa wachezaji muhimu kuliwapa nguvu zaidi Young Boys kuzidi ku-press.

Yote kwa yote Young Boys wamempa Ole wake up call, inabidi akaze na awe na plan B za uhakika, Ole ni kama hakujiandaa kucheza na wachezaji pungufu. Sub ya Ronaldo na Bruno pia ilikuwa muhimu kwa mchezo wetu wa weekend, mimi naamini kufuzu ni suala la muda tu ila ligi ni muhimu kwasababu tuna-compete na the best for a long season while UCL at early stages msimu huu tupo group jepesi.
 
Atalanta na Villarreal ni group jepesi? Haupo serious mkuu. ..mwanzo lilionekana jepesi lakini saivi mjipange sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…