Kwa lugha nyepesi:
Fantasy Premier League (FPL) ni mchezo rasmi unaokuwepo kila msimu ukiandaliwa na Premier League. Fantasy inakuwa ni kama virtual league ambayo mashabiki au hata wachezaji na makocha wanaweza kucheza.
Ipo hivi, FPL inakupa £100m unazotakiwa kuzitumia kutengeneza kikosi utakachokitumia katika msimu mzima wa PL.
Utanunua wachezaji kwa kuzingatia budget uliyonayo na thamani za wachezaji mbalimbali, mfano: thamani ya Ronaldo kwenye FPL ni £12.5m. Ukishatengeneza kikosi chako cha wachezaji 15 utakisajili kwa jina upendalo.
Sasa FPL huwa inatumia real time events kugawa points, kwa makipa hupata points kutokana na clean sheets wanazopata hivyo ukichagua kipa ni lazima awe na rekodi nzuri kiudakaji pia awe na defense nzuri na mpinzani anayekutana naye awe dhaifu katika eneo la ushambuliaji, vivyo hivyo kwa beki ila beki au kipa wakitoa assist au kufunga goli points zao ni nyingi kushinda kiungo au mshambuliaji.
Sheria zipo hivi, kila wiki ya mchezo (GW) utapewa free transfer 1 ya kuweza kuuza mchezaji uliyenaye na kununua mpya ila pia zipo chip kama Free hit na Wildcard zinazokuwezesha kufanya unlimited transfer ya kikosi chako ila tu Freehit hubadili kikosi kwa GW moja tu na kitarudi kile cha mwanzo.
Captain wako wa timu points zake zitazidishwa mara mbili ila pia kuna chip ya Triple Captain ukiitumia points zitazidishwa mara 3.
Wachezaji walioko bench points zao hazihesabiwi ila kuna chip ya Bench Boost ambayo ukiitumia points za bench zitahesabiwa.
Chip hutumika mara moja tu katika msimu isipokuwa Wildcard huwa mbili moja huanza kutumika GW2 baada ya msimu kuanza na nyingine hutolewa December katika mzunguko wa pili.
Mchezaji akikosa penati au akipata kadi ya njano/nyekundu katika mechi anakatwa points.
Kufanya mabadiliko ya wachezaji (sub) hufanyika kabla ya deadline katika GW, hivyo inapaswa kuzingatia deadline.
Huwezi kufanya sub baada ya deadline, kama mchezaji kwenye kikosi cha kwanza hatacheza hata dk 1 mwisho wa GW chaguo la kwanza sub litaingizwa automatic kuchukua nafasi ya ambaye hakucheza.
Zawadi kwa washindi zipo hivi:
Meneja wa mwezi
Mshindi wa kikombe cha ligi
Mshindi wa FPL
Mshindi wa FPL
Ni yule atakayejikusanyia points nyingi msimu mzima. Huwa anapewa siku 7 za kutembelea England na kukaa katika hotel ya nyota 5 huku akionyeshwa maeneo mbalimbali ya kitalii. Pamoja na zawadi kutoka kwa wadhamini wa ligi TAG ambao hutoa saa ya thamani.
Bila kusahau mshindi hupewa nafasi ya kutazama mechi mbili azitakazo katika msimu unaofuata akipewa VIP hospitality.
Mshindi wa mwezi
Ni yule anayeongoza kwa points katika mwezi husika, ana zawadi pia.
Mshindi wa ligi
Hii ni kama kombe la Carabao au FA zinachukuliwa timu zilizo nafasi za 4m+ kupanda juu na zinakuwa zinakutana H2H mpaka zitakazobaki mbili kucheza fainali huwa inaanza GW14 au GW18 kama sikosei.
Zipo Fantasy Football nyingi mfano ya UEFA Champions League ambayo bado haijaanza mpaka Jumanne wiki ijayo, zilizopita ni kama EURO2020, FIFA WC2018. Zipo pia za ligi kama Bundesliga na nyingine nyingi.
Pia zipo ligi ndani ya FPL ambazo huwa zina zawadi, mfano ligi ya Betway Tanzania, Shabiki OS kipindi kutoka EATV na nyingine nyingi.
Mimi huu ni msimu wa 3 nacheza, FPL ni nzuri sana kwa sisi mashabiki inakufanya ujue ligi nzima maana kuna muda inabidi ufatilie kujua wachezaji gani wakali uwanunue.
Ila tu huwa inakufanya uwaombee wachezaji pinzani ilimradi tu upate points, si unamuona Papaa Gx anavyotusema ila hapo alipo ana michezaji ya United aiombea kila wiki ifunge, sasa hivi anamtaka Ronaldo.
Mwaka 2018 mtanzania Yusuf Sheikh alileta ubingwa nyumbani baada ya Mo Salah kumpa nafasi ya kwanza kidunia pale alipom-triple captain.
Ni hayo tu zaidi pitia website ya Premier League > Fantasy utajua kila kitu kufusu FPL.