Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mzee baba kumbe upo?..tupo fainali ya Europa bana..
Nilikutana na changamoto za Dunia, lakini namshukuru mungu nimezishinda.
Mjengoni nimerudi jana, nashukuru kuwakuta wana chama wenzangu muko fresh.

Kuhusu Europe, tunachukua bila pressure, japo tunasuasua lakini naimani mpira wa Europe umehamia England, hispain mpira umesha hama.
 
Umerudi mkuu mana watu walikuwa na wasi wasi huenda machimbo yamezingua, eti yamekula kichwa
anyway ur welcome again.
Ha ha ha ha ha ha, mkuu kufa kulala kaburi tuta, hulijui hilo?

Mwa huu mwezi wa tatu tumepoteza waponcha wengi (kumi na sita kwa kukisia) mabox matatu yali katika na kusababisha mahafa hayo, namshukuru mungu niko mzima.

Walinikamata tu maporini (poli ni la mzungu) na kunihukumu miezi sita lakini namshukuru mungu kuna jamaa yangu wa kisukuma kapiga pessa kaja kunilipia, ila nimekunywa uji mwezi mmoja na siku kumi na nane.

Pessa tamu ila tusio na elimu tunazitafuta kwa mbinde, we acha tu, mungu mwenyewe anaona.
 
Dah pole sana mkuu.
 
Daah! Pole sana mwamba. Niliona kimya sana ata kwenye namba yako nilikuwa sikupati kabisa. Karibu sana, ila Chelsea wako fainali ya UEFA.
 
Daah! Pole sana mwamba. Niliona kimya sana ata kwenye namba yako nilikuwa sikupati kabisa. Karibu sana, ila Chelsea wako fainali ya UEFA.

Wanagawa makombe tu furaha yao kuingia final
 
Picha ya kwanza juu goli la Fulham Scot alikuwa ameshatoka kaingia Rashford ndiyo maana hapo Pogba anaonekana kwenye box

Ila bado panatakiwa mtu makini sana eneo hilo wanapoteza sana mipira
 
Kuna tofauti kwa wa nne. Anaanzia chini kidogo. Mechi 2 zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…