matumaini na mawazo ya mashabiki
ujio wa paul pogba ndani ya manchester united ulileta matumaini makubwa sana ya kwamba tumeanza rasmi process ya kujenga timu bora itakayoleta ushindani kwa muda mrefu barani ulaya, wengi wetu pia tulijawa na imani ya kushuhudia maingizo bora ya wachezaji wengine baada yake hii ni kwa sababu tuliamini hakuna mchezaji mwengine yeyote tutakayeshindwa kumsajili kwa sababu ya dau lake (tumeweza kwa paul, kwa nini tushindwe kwa raul). Si hivyo tu bali pia ujio wake ulituaminisha ya kwamba kupitia paul ndio utakuwa msingi wa manchester united kiuchezaji
matumaini ya paul na wakala wake
Mino anatwambia ndoto kubwa ya paul ni kushinda michuano ya ulaya, Ina maana kitendo cha mteja wake kurudi tena manchester bila ya shaka kulitokanwa zaidi na mikakati bora waliyoelezwa na upande wa manchester united nyakati hizo wanafanya mazungumzo ya kibiashara kati ya pande mbili hizo. Sitaki kuamini ya kwamba paul amerudi tena kwetu kwa sababu ya mshahara pekee huku akitupilia mbali ndoto yake tajwa hapo juu.
chimbuko la kusambaratika kwa mahusiano
Bila ya shaka imani ya watu wawili hao ilianza kufifia baada ya kushuhudia kusuasua kutekelezwa huo mkakati bora wa kiuwekezaji walioelezwa nyakati hizo na upande wa mancheter united. Naamini mkakati lengwa hapa ni suala la usajili wa wachezaji bora watakaoungana na pogba kwa dhumuni la kujenga timu bora pamoja na kuondoa wachezaji wenye viwango visivyoendana na hadhi ya manchester united (sitaki kuzungumzia mzunguko wa usajili wetu)
ukiongezea na matokeo mabovu ya timu (sometime paul hakuwa muhusika mkuu), kushushiwa shutuma paul na kocha mkuu kwa kushindwa kuonyesha kiwango bora (mgogoro wake na jose), kelele za mashabiki, wachambuzi na legends kulizidi kuchochea moto kwa upande wa paul kutamani kuondoka lakini klabu iliendelea kusimamia msimamo wa kutokuruhusu paul aondoke licha ya mwalimu naye kuonyesha nia ya kutamani kumuondoa paul, hatimaye tulishuhudia kuondoka kwa mwalimu na kubaki kwa paul
Pogba na ugonjwa wake binafsi
majeruhi ya mara kwa mara yanayomfanya atumie muda mwingi kitandani, mshahara mkubwa usioendana na anachotupa tokea asajiliwe, kukosa mchezo bora (consistency) jambo linalopelekea asiwe na nafasi ya uhakika na nafasi maalum ndani ya kikosi, ukiongezea na matatizo ya wakala wake ya ubwatukaji na uchonganishi yanazidi kuchochea hasira za wanafamilia ya manchester united wanaotamani kuuona mwisho wa paul akiwa na jezi nyekundu, si hivyo tu bali pia tabia za wakala wake zinaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa sana vilabu vyenginevyo kusita kufanya biashara naye kwa hofu ya muendelezo wa matendo yake
man utd na ugonjwa wake
hatuna mchezaji mwengine anayelingana na paul kiuwezo kwenye nafasi yake hivyo basi inakuwa ni vigumu kwa united kuwaridhisha mashabiki wanaotamani paul aondoke na kuleta mchezaji mwengine, bado tuna matatizo mengi ya kiufundi tunayopaswa kuyatatua kama vile eneo la ushambuliaji, kiungo wa chini mwenye uwezo wa kutimiza majukumu kwa ukamilifu (aliyebora zaidi ya scott na fred), winga wa pembeni, mlinzi wa kati, mlinzi wa kulia mbadala wa wan bissaka,
Maafikiano ya pande mbili ndio suluhisho
sidhani kama upande wa raiola bado atakuwa na jeuri yenye kuambatana na upofu wa kuamini ya kwamba bado ana nguvu ya kuzishawishi timu kubwa kumsajili mteja wake kwa dau litakalowekwa na upande wa manchester united bila ya kusahau maslahi binafsi ya kwake (pesa ya wakala) na ya mteja wake. Juve wapo hali mbaya kifedha na kiuchezaji, Paris wanaweza kuvutiwa naye ila ishu ni FPP na dau litakalowekwa na man utd, real madrid wameshampa kandarasi luka modrik kwa maana ya kwamba eneo la kiungo halitakuwa kipaombele chao (ukiongezea na kipigo cha corona ndio zaidi haitokuwa rahisi kwa hivyo vilabu kumtafuta edwoodward)
pia sidhani kama klabu itakuwa tayari kujiingiza katika msako mwengine wa kutafuta mchezaji atakayerithi nafasi ya paul baada ya kuondoka kwake, tumekuwa wazito sana kukamilisha usajili wa mchezaji hatimaye tunajikuta tunatumia wiki kadhaa kufanya negotiation na pande hasimu, kumuondoa paul na kuleta hapo tunazalisha process nyengine ndefu na ya gharama.
Naamini klabu itatumia njia ya mazungumzo na upande wa paul ili asaini kandarasi mpya yenye maboresho ya maslahi na si vyenginevyo, klabu haitokubali kuuziwa uhuni na raiola kwa kumuachia pogba aondoke bure kama wanavyofanyiwa AC milan kwa donnarumma.
" kwa sasa Pogba, raiola na manchester united ni wakorofi wanaohitajiana"
pumba za daemusin