Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Siku Hanibal Mejbir atakapopewa first debut hata Bruno tutamsahau.
kwa kuliangalia kundi la vijana liliopo pale klabuni kwa sasa unaweza kujijengea imani na matumaini ya kwamba yajayo yatakuwa na neema, hata hii sheria mpya iliotokanwa na vugu vugu la Brexit haitotuathiri sana kwenye eneo la uwekezaji wa soka la vijana hii ni kwa sababu tayari tunao vijana wa kutosha kutoka nchi zilizo nje ya Uingereza tuliowasajili siku za karibuni.

kutokana na mabadiliko hayo ya kuzuia usajili wa wachezaji waliochini ya miaka 18 kutoka mataifa yasiokuwa ya Uingereza ndio maana si ajabu klabu imeamua kuelekeza nguvu zake kwenye kutafuta vipaji na kuongeza scouting kupitia maeneo tofauti ya Uingereza hususani kusini mwa london eneo ambalo limezalisha vijana takribani 200 ndani ya miaka 10.


tusisahau kuwa na kundi kubwa la vijana wenye vipaji lakini wakakoseshwa mlezi bora kwa makusudi na wakakoseshwa huduma bora za uwanjani (dakika za kucheza) tutakuwa tunaendeleza mzunguko ule ule unaofanywa na timu nyenginezo zisizotoa nafasi ya kutosha kwa vijana waliokulia ndani ya klabu husika.
 
Kuna kipindi Arsene Wenger alikuwa anapata matokeo huku beki wa kati akiwa Johan Djallouh
alikuwa anapata matokeo yasiokuwa yakuendelea(consistency), matokeo hayo yalichangizwa zaidi na ukosefu wa wachezaji wengi wenye ubora ndani ya kikosi chake.

licha ya kwamba arsenal ya wenger walikuwa wana form isiotabirika kwa misimu kadhaa haifichi ukweli wa kwamba arsenal hii ya sasa imezidi kuwa na kundi la wachezaji walioshuka viwango zaidi ya Arsenal ile ya kina djorou, sylvestre, clichy, sagna, koscielny, song, diaby, frimpong, chamakh, RVP, nasri etc
 
Man United ya leo inakikosi kikubwa ila bado haijachanganywa vizuri kama United ingekuwa chini ya Arsene Wenger huenda asingesajili mchezaji yoyote dirisha hili maana watu wakuwatumia anavyotaka wapo.
tukiachana na ishu ya chemistry bado tuna matatizo ya mchezaji mmoja mmoja
hii safu yetu ya ushambuliaji inanipa ukakasi wa kuwa na matumaini ya kwamba msimu ujao tunaweza kugombania makombe ya ligi tofauti, hii ni kwa sababu tuna kundi kubwa la wachezaji ambao wanafanya makosa mengi ya kiuchezaji mara kwa mara pale mbele.

ukiwaangalia wachezaji wengineo si kwamba hawafanyi makosa pindi wanapocheza bali makosa yao mara nyingi huwa ni machache yanayoweza kufichika kwa mazuri wanayoyafanya. Kwa mfano hao jamii ya haaland, salah na mbappe si kwamba hawakosei kwa kila maamuzi wanayoyafanya ila kama wangelikuwa na makosa mengi kama ya rashford, greenwood na martial wasingelikuwa na jeuri ya kufunga magoli 34 kwenye mechi 37.

lakini ukija kwetu sisi mfano ni mara ngapi unashuhudia marcus rashford anakimbia na mpira au kufanya uamuzi wa kupiga mpira eneo husika bila ya kuruhusu mawasiliano kati ya mguu wake na ubongo wake?
hapo sijamtolea mfano greenwood, martial na yule mwanariadha daniel james na cha kusikitisha tukio hilo atalirejea tena mara kwa mara mpaka unafikia hatua unajiuliza hivi hawa wachezaji wetu wanafanya mazoezi kweli huku wakiongozwa na mwalimu.

kama utaamua kuwahukumu wachezaji wetu (james, martial, rashford, greenwood) kwa kuangalia benefactions zao eneo la (assist na goals) bila ya shaka utaondoka na kauli moja tu ya "wachezaji wetu ni sehemu ya kundi la wachezaji wanaofanya vizuri sana duniani"

kama utaziangalia factors nyenginezo bila ya shaka utaondoka na kauli hii "ni bora tuanze upya kiuwekezaji eneo la safu ya ushambuliaji na hawa waliopo wawe backup".

kwa kuwa Ole ameonekana kushindwa kuwapika na kuwakaripia hao vijana na kuwa na makali kama haya tunayoyashuhudia kwa wachezaji wengine mfano sterling au forden, mimi napendekeza tuanze upya kiuwekezaji kwenye safu ya ushambuliaji kwa sababu hawa waliopo hawanipi matumaini ya kuwa siku moja watakuwa na viwango visivyobadilika

  • leo hii marcus rashford ana magoli 54 kwenye mechi 172 za ligi kuu ndani ya misimu takribani 6, kama utetezi wake ni kucheza pembeni basi hata mbappe na salah wanacheza pembeni na wana takwimu nzuri za magoli na assist zaidi ya marcus.
  • antony martial ana magoli 56 kwenye mechi 167 naye amecheza takribani misimu 6 ya ligi kuu
ina maana kwenye mechi takribani 330 washambuliaji wetu muhimu kwa pamoja wamefunga magoli 110,
 
Yupo bize na sajili dogo dogo kila mwaka
 
Yule mzee alikua na maajabu sana
 
Pale mbele kwa mtazamo wangu mimi tunahitaji striker kama Haaland,,na right winger kama Sancho..then ;

✓Rashford na Martial wapambanie left wing.

✓Greenwood awe backup ya right flank na pia striker.
 
Bado hajafukuzwa tu
 
Pale mbele kwa mtazamo wangu mimi tunahitaji striker kama Haaland,,na right winger kama Sancho..then ;
ni wazo zuri sana ila sidhani kama linaweza kutekelezeka ndani ya dirisha moja kubwa la usajili, hao wawili thamani yao inafikia paundi millioni 190.

kugombania namba kwa rashford na martial pia ni idea nzuri sana, changamoto kubwa itakayojitokeza ni kwa pande mbili hizo zikiongozwa na mawakala wao kutokuridhika na mfumo huo kwa sababu wote wameshajijengea imani ya kwamba wanastahili kuwepo kikosi cha kwanza pindi wanapokuwa wazima.
 
Rahim Sterling(26) carrier
Mp 285, G 95 A 50

Marcus Rashford(23) carrier
Mp 172, G 54 A 28



Ukiangalia hizo stats hao wawili utofauti wao ni ni mdogo.

Ila tusisahau
Mmoja amecheza kwenye timu ambayo ni mabigwa wa EPL msimu wa 2017/18 na 2018/19, na runner up wa msimu 2019/20.
Na mabingwa watarajiwa msimu 2020/21.

Huyo mwenzie amecheza timu ambayo nafasi ya juu waliyoikamata ni nafasi ya pili(2017/18).

Hoja yangu: kama Rashford haonyeshi kiwango cha kuwa 1st 11, basi Sterling si mfano mzuri kuutumia kwenye hoja yako( based on perfomance)

Hao wengine Mbape, Haland, na Sarah.
Uko sahihi.


Mwisho uniwie radhi kuchukua sehemu ndogo ya maandishi yako nakuikosoa.
Ukiona hivyo ujue sehemu kubwa uko sahihi(isipokuwa hapo kwa Rashford na makali ya Sterling)





Sent using Jamii Forums mobile app
 

===================
mkuu hapo juu sijaweka ulinganisho wowote wa kitakwimu kati ya rashford na raheem sterling, kuwatumia foden na sterling kama mfano lengo kuu ni kuonyesha jinsi gani kocha wao alivyosimama kidete kuhakikisha wachezaji hao wawili wanaonyesha kiwango bora na cha uhakika (consistency) cha uchezaji soka kwa kila msimu.

bila ya shaka Guardiola amechangia kwa kiwango kikubwa sana mabadiliko ya kiuchezaji ya raheem sterling ya kutoka kuwa mchezaji anayeamini zaidi mbio hadi kuwa mchezaji hatari anapokuwa ndani ya boksi la adui.

Tukija hapo kwenye takwimu ukiachana na msimu huu ambao mpaka sasa amefunga magoli 9 sterling amekuwa na rekodi ya kufunga magoli 20, 17 na 18 kwa hii misimu mitatu nyuma ya ligi kuu chini ya guardiola.

Na ukija kwa rashford licha ya kwamba wana ulingano fulani wa mechi za kucheza yeye amefunga magoli 10 msimu huu, magoli 17 msimu uliopita, magoli 10 msimu mwengineo na magoli 7 msimu mwengineo.

sterling na foden wapo kwenye mikono ya mwalimu sahihi ukilinganisha na rashford pamoja na mdogo wake greenwood
 
Marcus Rashford has been directly involved in more goals (31) in all competitions than:
🇫🇷 Karim Benzema (30)
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Jadon Sancho (26)
🇫🇷 Antoine Griezmann (25)
🇧🇪 Kevin De Bruyne (24)
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Raheem Sterling (22)
🇺🇾 Luis Suarez (21)
🇧🇷 Neymar (19)
🇸🇳 Sadio Mane (18).
=======================
 
Phil Jones has now missed more games through officially recorded injury than he has played games for Man United (Per TransferMarkt Stats)
  1. Number of Games played for Man United (including off the Bench apps): 224
  2. Number of games missed through recorded/noted/reported injury: 228
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…