Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Auba namuacha yeye na Digea na hafungi.
Jamaa alitaka aongezewe mtonyo tu awaonyeshe rangi yake asili.
Hahahaha saiv ana uhakika hata akivunjiwa mkataba ana mtonyo wake wa uwakika.😂😂😂
Auba kama Willian tu
 
Wakuu uyu bruno fenandez toka chadema washindwe simwelewi, Hatuwezi mchukua robert snodgrass west ham January? au Dany drinkwater?
 
Wale jamaa wa China wanaweza wakawapa presha kama wanayoipata arsenal kwa ozil
 
Kwani adhabu ni mechi 3 vile?
Nilidhani mbili, nikajua jamaa kesha maliza.
Kuna aina 2 za foul mkuu kuna tactical foul ambayo mchezaji anacheza madhambi kumzuia adui asiende kufunga pili kuna misconduct foul....utovu wa nidham wowote kama kupigana,kutukana refa, fujo nyingine nknk so martial anadondokea hapo chini ndio maana anaserve 3 games ban, ila tactical foul nadhani ni game 1 tu
 
Wazo zuri mkuu ila kauli za Ozil dhidi ya Waislam wa China zilifanya China kuitishia arsenal kuwa mechi yoyote ya arsenal atakayocheza Ozil basi haitaoneshwa china.....

na sio kwamba arteta hataki kumtumia Ozil nooo, shida ni masuala ya kibiashara, kwani China ni moja ya nchi zinazoilipa vizuri FA na klabu katika matangazo ya soka na vilabu katika issue nzima ya mauzo ya jezi......

Kwahiyo united sidhani kama watafanya hii gamble kwani wanafanyaga hadi tour China, it means tour za klabu kuingia china zitakuwa banned kabisa ama kuwekewa vizingiti vya kibiashara

Ozil killed his own talent and football journey kwa kauli ndogo tu....ila mbinguni amejiwekea swawabu kubwa kwa kusimamia ukweli......
 
Ahsante kwa kunitoa tongo tongo.
 
United itakubali kuingia msala na China
 
Sikujua hili kwamba lilifikia hatua hii.

Kwahiyo Ozil hata kukanyaga China haiwezekani tena katika maisha yake ?.

Anyway ngoja tuwaachie wenyewe tu kwa sababu kama ni hivyo United hawawezi kufanya hiyo gambling.

But angeleta impact kubwa sana kwa timu yetu hasa upande wa kulia na asingehitaji kukimbia eneo kubwa sana uwanjani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…