Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Unachoongea ni sahihi lkn hii haifuti ukweli kwamba tm kocha, tunaona barca juzi tu hapa walikuwa wanacheza hovyo kuja kocha mpya mwenye mbinu kuzd aliyepita tm imebadilika kabisa, tunayaona hata kwa Everton, Leeds, Bayern, City n.k, hicho unachoongea ww ni sawa lkn czani km it holds any water when it comes to bad results to man utd cz tm km man u huwez kuniambia staffs wote ni wabovu weeee!! unatumia vigezo gani mkuu, man kubwa sana man ni zaidi ya hicho unachokisema ww mkuu yn unataka kutuaminisha kuwa wachezaji wote waliosajiliwa pale ni wabovu? Co kweli kabisa.

Kuhusu tm kubadilisha badilisha makocha co shida Liverpool kabadili makocha wngp mpk kumpata klopp? Pale utd kaondoka mtu mzito sana ilikuwa ni lazima tuyumbe hata angekuja nani ila ipo siku tutapata kocha anayeendana na fortune ya tm cz kocha wkt mwngne ni bahati na tm pia.
 
Asubuhi tujitahidi kuamka mapema sana tuchanje kuni za kupikia wali ili marehemu asione tumemletea zarau kwa mara ya pili
 
Wakati lampard anasajili sim card, na sasa zinaanza kumletea faida.! Ole Sendeka alikuwa anaandika maneno kwenye kanga ili amchambe FL
 
Huu ugonjwa uliua watu wengi sana,. Nngeshangaa kuona mgonjwa wetu mpendwa angebaki salama
 
The best 007,

Hujiulizi ni kwa nini chini ya Ed ndani ya miaka 7 tu, tumekuwa na makocha 5? Ni kweli Ole ni kocha mbovu lakini nani amemuaajiri kocha mbovu? Nimesema hapo juu ukifanya observation ndogo tu, Manchester United tumekuwa na football executives wanne tu ndani ya miaka 28 iliyopita toka Premier League ibadilike na sisi ndio tuliofanya vizuri ktk mfumo mpya tumebeba mara 13. Lakini ktk hao football executives wanne kuanzia Martin Edwards (1980-1997), Peter Kenyon (1997-2003), na David Gill (2003-2013) hawa wote wamefanya kazi na kocha mmoja tu kipindi chote hicho na kila mmoja amebeba EPL zaidi ya mbili. Kwa nini Ed Woodward amefanya kazi na makocha 5 na hajashinda kombe la EPL ndani ya zaidi ya miaka 7? Kama factor ya kuwa na timu bora ni pesa basi Ed ndiye aliyepaswa kuwa na timu bora zaidi chini yake maana hata ukifanya inflation adjustment yeye ndiye aliyetumia pesa kuliko chief executives wote waliomtangulia.

Bado tu unaamini tatizo la Manchester United ni kocha? Are serious bro? Okay, tufanye kweli tatizo letu ni kocha. Je ni nani anayewaajiri hawa makocha wabovu? Kumbuka wachezaji ni end products ya talents baada ya ku-assemble best talents from coaching staffs to recruitment teams na mwenye jukumu la kufanya hili ni football executive. Hata aje malaika kuwa kocha wa timu ukiwa na football executive mwenye uwezo mdogo ni sawa na kuigeuza Tanzania iwe sawa na Marekani kiuchumi.
 
The best 007,

Nimeona pia umefanya comparison na timu zingine si kila timu tatizo lake ni management zingine ni technical (coaching area) zaidi mfano mzuri hao hao Everton ila wote uliowataja hapo bado wapo ktk hatua za awali huwezi pata picha halisi kwa sasa mf. Barcelona wajumbe sita wa bodi akiwemo na makamu mwenyekiti walijiuzulu mwaka huu pia director of football (Eric Abidal) alifutwa kazi ndio wakaanza upya kusuka uongozi wa juu mpaka kocha.

Kwa upande Manchester City, the brain behind them ni Ferran Soriano huyu ndiye mastermind nyuma ya ile Barcelona ya 2003 - 2008 alikuwa ndiye mtendaji mkuu na makamu wa rais kipindi hicho. Chini ya Ferran Soriano baada ya yeye kuajiriwa as football executive ameshinda mataji ya EPL matatu toka mwaka 2012 mpaka sasa.

Kwa Bayern hapa the brains behind them ni Karl-Heinz Rummenigge na Franz Anton Beckenbauer na hawa shughuli zao sio za kitoto wapo hapo toka miaka ya 90. Kwa Liverpool mwaka 2017 waliajiri chief executive mpya anaitwa Peter Moore huyu chini ya kipindi chake Liverpool wamebeba EPL, UEFA na Fifa Club World Cup ndani ya miaka mitatu tu na sasa hivi amemaliza muda wake mwaka huu mwezi wa nane.

Ubora wa timu ya soka coaches ni kipisi cha mwisho kabisa ila watu wanaofanya kazi zaidi ni nyuma ya macho ya watu wengi yaani football executives hawa ndio wenye majukumu ya kuunganisha hizo talents japokuwa sisi tunawaona wanaokuwa uwanjani zaidi na tunawapa sana wao credits ila the brains behind ndio kila kitu. Ukiajiri makocha wabovu na wao watasajili wachezaji wabovu, ukiajiri wasaka vipaji wabovu watasaka vipajia vibovu na ukiwa na negotiators wabovu kila mchezaji sokoni utamkosa na hata ukimpata utapigwa bei. Football executive ni kila kitu ktk timu. Liverpool (Peter Moore, 2017- Aug, 2020) na Machester city (2012 - mpaka sasa) mafanikio yao yamekuja baada ya kuajiri watu wapya hizi nafasi.

Kitu ninacho jaribu kukisema hapa kuna tofauti kubwa sana kati ya mpishi wa chakula (kocha) na mtu nyuma ya hicho chakula mpaka kipikwe jikoni (Chief executive).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…