Manchester United (Red Devils) | Special Thread

★Is dis how agreement ends??? Mbona tunataka kulazimisha kama tunachukua Mwali wakuoa


@manutd
 
Darmian,

Ubingwa kumpa Liverpool bado mapema sana, japo ndio timu pekee katika kubwa walio serious zaidi. Mechi mbili zijazo kwa Liverpool zinaweza kuwapandisha morali au kuwashusha. Mechi ijayo wataenda Villa Park kucheza na Aston Villa hawa ni sawa na farasi mweusi asiye angaliwa na wengi kwa hiyo hawachezi kwa presha ila kiukweli wapo moto sana, wamecheza mechi nne msimu huu wameshinda zote ya mwisho walimfunga Wolves kwake 3 bila.

Baada ya Aston Villa wataenda mji wa Walton pale pale Liverpool kucheza na Everton, kwa form ya sasa ya Everton wakishinda pale Goodison Park basi Liverpool confidence yao inaweza kuwa juu mno ktk mbio za ubingwa ila wakianza kwa kufungwa inaweza kubadili hali yao ya kujiamini pia.

Pia umezungumzia kuhusu sajili zao, Liverpool ya sasa ina watu wa mipango na mikakati huwa wanajirekebisha kila wanapoona panahitaji kufanyiwa ukarabati wakiingia sokoni ujue ni very strategic move na sio kutuliza fujo za mashabiki wapo kimkakati zaidi.

Bodi yao ina akina Kenny Daglish anajua nini maana ya kumpa mwalimu nyenzo zake kwa wakati, yeye mwenyewe pia ni mwalimu wa mpira. Halafu changanya na Michael Edwards huyu ndiye master mind wa sajili nyingi sana za kimkakati ni director of football ila career yake kafanya sana kama perfomance analyst hata kipindi wanamsajili Mo Salah watu wengi waliaamini atashindwa kama awali alipokuwa na Chelsea.

Kwa kifupi, Liverpool ya sasa inaendeshwa na watu ambao career zao ni za mambo ya mpira sana. Hawafanyi sajili za kuuza jezi ila wanafanya sajili za kuleta mabadiliko zaidi uwanjani.
 
Mkuu kwa uongozi wa sasa wa Man utd usije ukawaonea huruma kabosa kwenye usajili wa gharama,mara 100 tunune sababu wakina glazer wanazila tu izo hela,wale jamaa hawapo kwa ajili yetu kabisa
 
Mkuu kwa uongozi wa sasa wa Man utd usije ukawaonea huruma kabosa kwenye usajili wa gharama,mara 100 tunune sababu wakina glazer wanazila tu izo hela,wale jamaa hawapo kwa ajili yetu kabisa
Hoja yangu ni kwamba, kwa hiyo hela, tunaweza sajili wachezaji wa kuziba nafasi zote muhimu tunazotaka kuziziba msimu huu.

LB, RW, Striker, RB, CD wote unawapata kwa hiyo hela. Na timu ikaziba mapengo yote.
 
Mourihno huwa ananichekesha sana..Jana wakati anahojiwa baada ya mechi ya chelsea alisema"On sunday we have a big work against super team(Man United) which is favourite to win the premier league"
 
Mourihno huwa ananichekesha sana..Jana wakati anahojiwa baada ya mechi ya chelsea alisema"On sunday we have a big work against super team(Man United) which is favourite to win the premier league"
Tutamtandika hataamini.
Toka nimeanza kuangalia ligi Tottenham ni easy prey wa United hivyo sitarajii challenge yoyote kwa Tottenham.

Wakijitahidi sana watatoa draw short of that tutawafunga tu tena kwa urahisi tu.
 
Unaona sasa?

Bissaka si amekuja juzi tu? Leo tunasajili mbadala kisa ameshindwa kufit eneo hilo. Bruno nae akiwa flop? Tutamsajili mbadala? Pogba je?

Hapo kosa la nani mchezaji kuja akiwa mzuri na kuflop baada ya msimu mmoja?
Mkuu ww huwa unalalamika mnoo cjajua ni kwanini kiongozi, wote tunalalamika ila kwa kiasi mkuu.
 
CAVAN,
Age 34yrs.
Injury prone
Big wages.
Nani kamwambiya ni majeruhi?cavani amepata changamoto kwenye first eleven baada ya ujio wa Icard na Neymar..
Hivi unakumbuka ibrahimovic aliponunuliwa man u alikuwa na umri gani?Kama sio 33?
Je hukuiona shughuli yake?
Cavani ni good finisher mkuu..
Ni mtu hatari sana....
He is not only an attacker but a goals scorer..
Man u lazima inunuwe striker,,, utaona shughuli ..
 
Hoja yangu ni kwamba, kwa hiyo hela, tunaweza sajili wachezaji wa kuziba nafasi zote muhimu tunazotaka kuziziba msimu huu.

LB, RW, Striker, RB, CD wote unawapata kwa hiyo hela. Na timu ikaziba mapengo yote.
Kweli kabisa mkuu
 
Correction kwa Aston Villa hapo wamecheza game mbili tu dhidi ya Sheffield na Fulham na kushinda zote sio game nne
 
Game ya man na Brighton ni kama game ya jana ya Tot na chelsea. Muamua matokeo ni Brighton. Kama atanunia kule kubebwa akapanga regular starters wa kila siku man atakua na wakati mgumu kusecure ushindi.
 
Nilisema hana thamani hiyo nikaambiwa nitulie maswala ya ukoo hayanihusu. Naona mwanaukoo mwenzao umegutuka kua kuna transfers zinafanywa halafu ni za viazi.

Kwa maoni yako. Ni kweli alaumiwe Lindelof au Maguire ni mzigo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…