Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ama kweli binadamu ni wepesi kusahau....aisee umesahau hawa ndo waliwapa kiminyo mwanzo mwanzoni mwa ligi goli 2-1
 
Bayern Munich wanapenda sifa sana, huyu Serge Gnabry alikuwa fala fala pale West Bromwich kipindi cha Tony Pullis ila sasa hivi moto wake ni wa kuotea mbali. Naamini hata Marcus na Anthony wanaweza ku-transform kuwa more lethal kama huyu jamaa.
 
Ama kweli binadamu ni wepesi kusahau....aisee umesahau hawa ndo waliwapa kiminyo mwanzo mwanzoni mwa ligi goli 2-1
Na umeona mi nimeongea kwa kuangalia past? New Castle aliifunga Man U moja bila walivyorudiana uliona nini kimetokea?

Mimi nimeangalia usajili wa Man U, Everton na Crystal Palace kisha nikaangalia games za Everton na Crystal palace. Ugumu wa game na idadi ya magoli.

Wewe unaleta stori za hapo zamani za kale
 
Haaaahaaaa We unavyosema "palace ni ileile inayopokea bakora kila siku" unafikiri tumeelewaje unamaanisha nn...kwamba kila mkikutana nao ni kama shamba LA bibi mnajichotea points 3 sio....
 
Bayern Munich wanapenda sifa sana, huyu Serge Gnabry alikuwa fala fala pale West Bromwich kipindi cha Tony Pullis ila sasa hivi moto wake ni wa kuotea mbali. Naamini hata Marcus na Anthony wanaweza ku-transform kuwa more lethal kama huyu jamaa.
Bayern inaonekana sio tu klabu bora ila ni shule bora ya soka..wanaongozwa na watu wa mpira tu...tofaut na utd
 
The Day We Were All Waiting Is Here..

GGMU

Kitu kama hiki itakuwa sio mbaya IMO

De Gea
AWB Bailly Maguire Shaw
Matic Pogba
VDB Fernandes Rashford
Martial

Greenwood ningemueka benchi for this one
 
★Teden Mengi has officially been promoted to the senior #mufc squad.★

#GGMU


manutd | View attachment 1573819
Nilitamani sana huyu dogo aje aharakishe safari ya Axel Tuanzebe.

Sijawahi kuona kitu special kwa Tuanzebe zaidi ya kuwa na sifa za Phil Jones kwenye kitanda cha wagonjwa.

Nataraji kuona makubwa kutoka kwake msimu huu ni beki mzuri sana mwenye kila sifa za kuitwa central defender.
 
Huyu dogo siyo mtanzania kweli ?
Cc tumelala sn angelikuwa ana asili ya Nigeria or Ghana et al., lazima ungesikia lkn huyo mchaga huyo.
Amekanusha Mwenyewe kuwa Ana roots za Nigeria, maana wale jamaa walishachukua Credit.

Jina lake la Kati ni Mambuene, hivyo anaweza kuwa na Asili ya Congo pia.
 
Haaaahaaaa We unavyosema "palace ni ileile inayopokea bakora kila siku" unafikiri tumeelewaje unamaanisha nn...kwamba kila mkikutana nao ni kama shamba LA bibi mnajichotea points 3 sio....
Pia mimi nashabikia Arsenal...
 
Kama kawaida leo mapema sana ntasogea karibu na TV kuona nini United watafanya.

Kwa misimu mingi mechi za ufunguzi huwa tunaanza vizuri sana haijalishi opponent tunayeanza naye.

Tukiamuaga ni mwendo wa 4 kwa kila anayekatiza mbele yetu, kuna msimu tulifungua msimu na Swansea akala 4 aliyefuata naye akala 4 na aliyefuata 4 hadi wakatuita wazee wa 4G. Msimu uliopita nao The Blauz wakachukua 4 zao safi na sajili zetu zote zikawa na mwanzo mzuri, Maguire & AWB walipata clean sheet na The Flash bwana Daniel James akamgaragaza Kepa Arizabalaga. 😂

Leo naiona United ikipata ushindi kuanzia goli 3 ikiwezekana tunapiga 4 palepale 'Theatre of Dreams' ama 'Stretford End' au 'Sir. Matt Busby Way' wenyewe wanapaita OLD TRAFFORD.

Tunaenda kuanza msimu tukiwa na nyota wetu muhimu kama Pogba, Fernandes. Nilishukuru sana Pogba ku-recover mapema maambukizi ya virusi vya Corona.

Mpaka sasa naamini Pogba ashajua mustakabali wake kisoka upo Manchester United naamini hii itampa morali kupambana zaidi uwanjani. Martial amekuwa na positive attitude sana tokea Bruno amekuja, naona kabisa msimu huu aki-shine zaidi.

Huu msimu iwe isiwe tutafanya vizuri sana tuna timu nzuri kupambana EPL tuna kiungo bora kabisa EPL.

Yote kwa yote hatutakiwi kuishia hapa tu, United wafanye tu maamuzi wamlete Sancho na Telles. Telles atatusaidia sana upande wa kushoto kupandisha mashambulizi hata ukabaji, jamaa physically yupo vizuri na ana shooting power kubwa; wenyewe wanasema msimu uliopita ligi ya Ureno yeye ni mmoja wa wachezaji bora pamoja na Bruno na jamaa ana fighting spirit ya kutosha ukimuunganisha na Bruno ni bonge la timu unajenga. Sancho kila mtu anajua uwezo wake akishika upande wa kulia itakuwa ni vilio kwa wapinzani kila wiki.

#GGMU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…