Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kama tumezadiwa penalty nyingi maana yake strikers wetu wanaingia sana kwenye box hivyo ni threat kwa timu pinzani
 
Halafu wakuu muda mwingine tuongee kwa kuangalia "Numbers"..

Usijiropokee tu kuwa Washambuliaji wa Liverpool wanafunga kila siku tofauti na sisi wakati front three yetu imewazidi magoli this season..

Tu-base kwenye hoja zinazoweza kupewa backup na statistical data
 
Naondoa

1 Smalling
2 Phill jones
3 Rojo
4 Lingardinho
5 Perreira
6 Mata
7 Fred

Naleta

1 Regullon ile LB ya Madrid iliyoko sevila kwa mkopo
2 World-class CB Kama Upermecano
3 Alcantara
4 Sancho
5 Jiminez

Nawapa onyo

1 Rashford
2 Dan James

Ila tu kama ningekuwa Ole + Ed Woodward
 
Unaweza ukatupa mfano walau mmoja wa striker ambaye anafaa kuwa first choice pale united ?
Cavani.PSG..ana 33 ...tangu ujio wa icardi na neima amekuwa yupo benchi na anapatikana kwa free transfer,, ila ana sifa zote za striker,,na ana gerentii ya kufunga..na ana good experience..
Mousa dembele, Lyon..ana 23....amekuwa na msimu mzuri tangu atoke Celtic,,amefunga magoli 58 kwenye mechi za leage 1 ktk mechi 42 alizocheza..
Paul ,,volve ..huyu jamaa ana 29 nae atatusaidia sn ktk kufunga,,
Jovic ,,real Madrid..huyu Dogo ana 22 ,alikuwa franfruit ya German ,alicheka sana na nyavu mwaka Jana,,akanunuliwa real,,lakini hajang' aa sana,,ila yupo sokoni..
Kuna ile striker ya sevila,,jina limenitoka kidogo,,
Na ole ameshawaonya martial na rashford kwamba anatafuta striker wa kuchalenge nafasi zao..
Don't take their position for granted..
 
Mkuu Darmian uko sahihi sana kwenye ulinganifu wa magoli kati ya attack trio yetu na ya liverpool. Kitu cha kujiuliza ni kwamba kama magoli ndio hutoa points ambazo mwisho wa siku ndizo huamua bingwa wa ligi,kwanini magoli yetu mengi hayajatusaidia kunyakua ndoo msimu huu? Wakati mwingine uhalisia ni bora zaidi kuliko takwimu. Kuna kauli moja maarufu sana mzee wenger akiwa kwenye peak aliwahi kusema kuwa namnukuu "sitaki striker anayefunga goli tano kwenye mechi moja halafu anakaa mechi tano hajafunga. Nataka striker anayefunga goli moja kila mechi katika mechi tano mfululizo" mwisho wa nukuu. Maana yake ni kwamba washambuliaji wetu kuna baadhi ya mechi wanakosa mbinu za kupenya defense ya adui,ila siku wakifanikiwa hufunga magoli mengi. Nadhani hili liko wazi sana,mbinu za OGS zikigoma kufanya kazi hakuna mtu wa kuchukua maamuzi magumu timu ishinde. Ndio maana watu humu wanawataka awkina Cavan na uzbabu wao waje kwa scenarios kama hizi. Asante
 
Msimu Wa Epl toka January Aje Bruno



Timu yetu mwanzo wa Msimu ilikuwa inatembelea magongo, Martial majeruhi mbele, Matic na pogba kati majeruhi baadae akaumia Mc tominay, ilifika kipindi hadi perreira ndo awe midfield tulipoteana sana.

Ila toka Aje bruno, Matic na pogba kupona tumekuwa wazuri kushinda timu yoyote pale Epl.
 
Umeua mkuu,,umeeleweka vyema sana,,
Man u tunahangaika sn ktk kufunga,,baadhi ya mechi,,
Wakati liver wao lazima washinde japo goal moja,,,lakini ushindi ni muhimu..
 
Hivi mkuu striker anakosa goal 4 anafunga 1 utabeba kombe gani?
Striker anafunga Leo goal 2 anakaa mechi tatu anafunga tena,,
Utafananisha na wanaofunga goal 1 kila mechi?
Striker hatuna mkuu,,man u ina wingers ,,
Yule mtoto greenwood yule akiongeza juhudi kidogo atawafunika wote hao,,akina martial na rashford..
Na haturopoki mkuu ,,tunaongea kwa takwimu..
 
Kwa usajili wa Van De Beek, naona tutakuwa tumeokoa Euro MIL40 kwa ajili ya eti yule Muingereza Grealish aliyepewa thamani ya Euro mil 80.
Maana naona jirani wenzetu pale London wameshapigwa mjini kwa Chillwell 50MIL 😀 😀 .
Kama tulivyopigwa 80 ya Maguire.
 
Tunaanza kuongea lugha moja.

Moja kati vitu ninawachukia waingereza ni kujikuza kule wasipostahili.

Wanajiona wana viwango wakati ni wakawaida sana.

Muingereza pekee niliemkubali kizazi hiki ni Wayne Rooney labda kidogo umuweke David Beckham.

Ila wengine sioni uajabu wowote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…