JAMANI, MMEMSIKIA IGHALO HUKO?
MMESIKIA huko? Straika, Odion Ighalo amesema yupo tayari kuipandisha Manchester United kwenye matawi ya juu zaidi baada ya kuongeza muda wake wa mkopo kwenye klabu hiyo kwa miezi sita zaidi.
Fowadi huyo Mnigeria ametua Old Trafford kwa mkopo akitokea Shanghai Shenhua, ambapo dili lake la awali la kuanzia Januari lilipaswa kumalizika Juni na sasa amesaini dili jipya litakalomfanya kubaki kwenye timu hiyo hadi Januari 2021.
Ighalo amefunga mabao manne katika mechi nane alizochezea Man United tangu alipojiunga mwanzoni mwa mwaka. Lakini, ilikuwa arudi zake China, wakati Ligi Kuu England ikitarajia kurejea baadaye mwenyewe huu na sasa atabaki kuwanyoosha.
Katika dili hilo jipya la meizi sita, Man United imekubali kulipa mkwanja wa Pauni 10 milioni. Na sasa, Ighalo anasema yupo tayari kumsaidia Ole Gunnar Solskjaer kukipandisha chati za juu kikosi hicho cha Old Trafford.
“Nimefurahi sana. Ni ndoto kwangu mimi kuwa hapa. Nipo fiti na acha mambo yaanze,” alisema Ighalo.
“Tangu siku ya kwanza niliyotua hapa, niliweka wazi kitu ambacho nataka kukifanya, hivyo nipo tayari kuendelea na kazi hiyo.
“Kama nilivyosema, tangu nilipokuwa kijana mdogo, nilikuwa naishabikia timu hiyo, hivyo kuja hapa kucheza ni ndoto kubwa iliyotimia. Sasa nimeongeza muda wa mkopo wangu, hivyo nimejitolea kwa kila kitu.
“Nataka kupiga kazi kwa nguvu zote na kufurahia mafanikio makubwa.”
mwanaspoti
Sent using
Jamii Forums mobile app