Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Najua we are comfortable now, na kitendo cha Haaland kusajiliwa Dortmund hakiwaumi watu wengi sababu ma strikers wetu wote kwa sasa wapo fiti na wapo form, sidhani kama watu wangekuwa na mtazamo huo huo mwezi septemba, Oktoba na Novemba mwaka huu unaokwisha

Unasema tungesajili senior striker ili awafundishe, nimewahi kuuliza huko nyuma, senior striker unayewaongelea ambao wapo sokoni ni akina nani, sikupata majibu. Utanishangaza ukinitajia Mandzukic, Falcao, Ibrahimovic wakati tumemuacha Lukaku ambaye angeweza kufanya hiyo kazi ya "kuwafundisha madogo" kama unavyoshauri

Kwa sasa hivi kikosi chetu kina pure striker wawili, Martial na Greenwood ambaye bado hajacheza senior football kiasi cha kwamba akaaminiwa na kupewa majukumu ya timu, Rashy sio striker (sio namba 9), DJ sio namba 9.

Haaland sio senior (kwa idadi ya miaka aliyonayo), lakini ni senior kwa uzoefu wa kucheza senior football. Pamoja na kumbeza kwamba ametokea ligi laini, lakini kote huko amekuwa outstanding. Ligi ya mabingwa Ulaya ameng'ara, je na hayo ni mashindano nyoronyoro? Wachezaji wakubwa wote Ulaya tunawapitisha kuwa ni bora au wabovu kwa namna watakaocheza ligi ya mabingwa Ulaya.

Haaland ana magoli 8, ni wa pili nyuma ya Lewandowski mwenye magoli 10, na wanaomfuata wana goli 6, kwenye chati ya wafungaji wa UCL 2019/2020. Kuliweka suala hili ili lieleweke vizuri, Haaland kiufungaji yupo juu ya mchezaji anayetajwa kuja kuwa Ballon'dour winner siku zijazo, Mbape ambaye ana goli 5 kwenye UCL. Kwahiyo hapa tusikaririshane uongo kwamba dogo anafunga magoli ligi nyepesi nyepesi tu, huyu dogo ametoboa safu za ulinzi chini ya Koullibaly na VVD, kwa taarifa yako.

Nakukumbusha pia RB Salzburg, timu unayodai inacheza ligi nyepesi ndio imewaleta kwenye ulimwengu wa soka, akina Mane, Naby Keita, Minamino (Liverpool) Upemecano (RB Leipzig) n.k. Kwanini Haaland asiwe bora kisa tu ametokea ligi ya Austria.

OGS akiwa mchezaji alitokea Norway, Nesterloy alitokea Uholanzi, Delle Ali ametokea MK Dons timu ya ligi daraja la 3, Ibrahimovic alitokea Malmo ya Sweden, orodha ni ndefu sana.

Pia nikukumbushe, kuwa scouts wapo kwa ajili ya hiyo kazi, ya kutafuta diamonds kwenye mashimo na si kwenda kununua almasi kwenye masoko yaliyopo mjini

Mwisho nikwambie, kusajili siku zote huwa kuna asilimia flani ya gambling, kuna wakati unaweza ukasajili mchezaji na akacheza kwa kiwango ambacho haukukitazamia au akang'ara, kwa United kufanya gambling ya £20million tu kwa Haaland isinge disturb pochi nene ya Glazers.

Kitu pekee kilichonifurahisha kwa huyu dogo kwenda Dortmund na sio kuja United, ni kutoongeza wigo wa kufanya biashara na tapeli Mino Raiola

Huyu dogo ameshakwenda, tuangalie mambo mengine
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila mkuu usisahau tupo majeruhi moja tu tuwe timu isiofunga. Bila martial timu yetu ni ovyo kabisa katika ufungaji. Tunahitaji backup ama patner wa Martial.

1. Ole anamjua Haaland hivyo angekuja isingekuwa ngumu kwake kumtumia.
2. Euro milioni 20 ni pesa ndogo sana kwa Man U hasa Era hii ambayo kila mchezaji mzuri ni 50m kupanda.
3. Kuna mifumo ole anatumia inawezekana wote Martial, Rash, Haaland na James kuanza, na hata mmoja akianzia benchi ni kawaida watapokezana.

Timu zote za Man U ambazo zilikuwa zikitesa zilikuwa na Depth kubwa sana. Mfano Man U ya 1999 ina Cole, yorke, sherigham, na Solskjaer wote ni striker hao, ukija ya 2008 una Ronaldo, Rooney, Tevez, saha, welbeck etc

Ili tuwe na depth nzuri tunatakiwa striker, midfield/winga ya kulia inayojua kufunga na no 10 ama playmaker/kiungo mshambuliaji.

Ila yote hayo Nakubaliana na Ed/ole kwa kumtolea nje Raiola na Baba wa Mchezaji, Fergie pia aliwahi kufanya hivi kwa Tevez, mchezaji hatakiwi kumilikiwa na mtu.
 
Umeandika habari ndeeeeefu ...aaagh straika gani ya man u iko fom ..Rashid?? Mashow???

Acha utani bana...

#CFC


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani unamaanisha mchezaji haitakiwi kumilikiwa na wakala
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwenye ligi alizocheza huyo dogo sidhani kama upo sahihi ktk kufanya huyo dogo asiwe na sababu ya kusajiliwa na Man U. Ole mwenyewe alipatikana kutoka wapi, pogba alipatikana wapi? Labda kwa Hoja ya kwamba tuna vijana wengi Wa umri Wa haaland wenye uwezo Mkubwa tunaopaswa kuundeleza
 
Jamaa umeeleza vema sana
 
Namchukia sana mino raiola
 
Arsenal bana sikutegemea watazingua kiasi kile First half Chelsea ilikuwa ovyo no shot hata moja yet michezaji ya Arsenal imerelax mfano lacazette alipasiwa vizuri anazingua ovyo tu.


Jumatano mkianza na soka la Chelsea tegemea kipigo! Maana mtakuwa manataka kushambulia ovyo ovyo mkijisahau kuwa wakata mnashambulia.mkikosea pasi ikatua kwa fred fred huyo anampa David James mbio mbio mbio mbio!


Ole wako Rashford utuzingulie chance.
 
Hahahah umenichekesha, eti wakikosea akaidaka Fred shida itaanzia hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…