Mashabiki kuna wakati huwa tuna babaika sana
Kipindi Martial ameumia, tuliona kabisa kuwa ni bora Lukaku na Sanchez wangeachwa kikosini wangeweka ujazo kwenye squad yetu
Nakumbuka wakati huo, Greenwood alipata nafasi kadha wa kadha, lakini hakuonesha makeke kiviiile (mimi naendelea kuamini dogo ni bora kuliko Tony na Rashy kwenye ku score)
Kipindi hicho tulihitaji sana striker, tulipiga sana kelele kuhusu hitaji la striker na OGS alisema ni dhahiri kuwa nafasi inayopewa kipaumbele kuzibwa katika madirisha yajayo ni striker, na mashabiki wote tuliunga mkono wazo hilo
Ghafla Greenwood yupo form (kwa kufunga mfululizo), tunaona tena haina haja ya striker...... Hahahaha, mashabiki bhana, ndio maana bodi sometime huwa haisikilizi kelele zao.
Tumewahi kuwaza ikitokea Martial na Rashy wameumia kwa wakati mmoja hata kwa wiki 3 tu, nini kitatukuta? Tutamweka pale mbele Greenwood na Pereira, au na Lingard? Ikitokea katika mechi 5 mfululizo dogo hajafunga, si mashabiki tutamkataa? Je akiwa na mtu mwingine hatuoni kama itamsaidia kumpunguzia pressure?
Tunasema aletwe mtu mwenye experience, nani Mandzukich mwenye miaka 34? Falcao? Zlatan? Are we serious?
Utoto wa Haaland. Kiumri Haaland na Greenwood wanaweza kuwa sawa au wamezidiana kidogo, lakini tunapaswa kutofautisha kati ya age vs maturity, Haaland ameanza kucheza senior football mapema ukilinganisha na Greenwood, kwenye hoja hii hii, leo tukiambiwa Mbape aje United tutamkataa kwa sababu tutam discourage Greenwood au Rashy?
Je tumesahau hii ni Manchester United inayohitaji ushindani wa hali ya juu kwenye namba, je tumesahau hii ni United inayohitaji options mbalimbali kwenye kila namba uwanjani? Je tumesahau kuwa ushindani ndio utaongeza ufanisi kwa wachezaji wetu? Je tumesahau kwa wakati flani tulikuwa na Andre Cole, Dwight Yorke, OGS na Teddy Sherigham katika kikosi kimoja? Juzi juzi ndani ya kikosi kimoja alikuwepo Berbatov, Tevez, Rooney, CR7, je hatutaki kurudi kwenye zama hizo?
Hoja ya kutafuta striker mwenye experience ndio aje awasaidie madogo si hoja sahihi sana, labda sokoni angekuwepo, Harry Kane, Aguero na wachezaji wa kaliba hiyo tungeweza kuishabikia.
Nakubaliana kumchukua Haaland ni gamble, kwanza anatoka ligi ambazo (Norway, then Austria) sio strong kama premier lakini pia kwa umri wake anaweza akaharibikiwa asipoji handle vizuri baada ya kuanza kula £100,000+ kwa wiki.
Lakini it is the gamble worth taking, isitoshe wanasema hawezi vuka £60million, mchezaji mwenye goli 27 katika mechi 22 zikiwemo za UCL atatusaidia sana.
Nakumbuka Madrid Wali gamble kwa Jovetic (na mwaka jana wengi tulimtamani aje United) lakini mpaka sasa bado haja onesha makali. Icardi hali yake sijui ipoje huko alipo?
Kuna jambo hapa kuna baadhi ya watu wananifurahisha sana, Erlin Haaland wanini wakati tuna Mason Greenwood? Tena kwangu mimi naona Erling anacheza mahala ambapo hana pressure na kapewa muda zaidi kuliko Mason. Kwangu mm kama ananunuliwa mshambuliaji basi anapaswa awe mzoefu kuja kumpa uzoefu mtu kama Mason calibre ya Harry Kane na sio kinda mwenzie tena ambaye anamzidi uwezo. Kama kuna kitu kitanifanya nilidharau bench letu la ufundi ni kumnunua huyu Erling. It's a total joke! And It will be very disrespectful kwa Mason.
Sent using
Jamii Forums mobile app