Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kabisa hawa jamaa tunawaonea tu yani.
 
Mimi mwenyewe jana nimelisema hili..tunacheza sana nyuma,backpass tu muda wote..hakuna kiungo wa kutengeneza nafasi za kuonekana,tunategemea counter tu kwa timu zinazojisahau

Tutengeneze kwanza kiungo chetu
 
Mimi mwenyewe jana nimelisema hili..tunacheza sana nyuma,backpass tu muda wote..hakuna kiungo wa kutengeneza nafasi za kuonekana,tunategemea counter tu kwa timu zinazojisahau

Tutengeneze kwanza kiungo chetu
Ni aibu timu yetu haina mchezaji mwenye ujasiri wa kumpiga chenga mpinzani na kutoa assist. Hata kutembea tu na mpira ni kazi kwa kiungo chetu.
 
Timi inazidi kufa hii, Huyo ozil hastahili kuchezea team ya United.. United hii inahitaji agressive players wa kufia uwanjani na sio huyo "Mpemba" Ozil... Mtu lonyolonyo Kama Ozil hatufai
 
Vipi DRINKING WATER jamaa anapiga kazi sio mchezo alichukua epl with Leicester city.
Mkuu narudia Tena , Manchester United haina tatizo la wachezaji ila tuna tatizo la Timu.. Unaweza kuwa na wachezaji wazuri ila ukakosa kocha wa kuunda timu .. Leicester City ilichukua EPL sio kwa kuwa na wachezaji Bora kuzidi Man City au Chelsea Bali timu ilikuwa Bora zaidi ya mchezaji mmoja mmoja ... Na hapo ndipo United tunapozidi kukosea kila siku kuwa matatizo yetu yatamalizwa na Mchezaji flani. Si kweli na haitakuja kutokea .. Tatizo la United litamalizwa kwa timu kuundwa kitimu baaaasi. Kama Ni suala la mchezaji mmoja mmoja United imesajiri wachezaji wengi Bora na waliishia kuwa flop (Lukaku, Depay , Micktaryan na Dimaria N.K.. Ndio maana leo tunamuona Pogba , au Rashford hawafai .. Bado tupo kwenye circle ile ile ya kuona timu yetu itasonga kwa juhudi za mchezaji mmoja badala ya timu nzima ...



Chelsea ambayo imeondokewa na Mchezaji tegemeo (Hazard na Beki David Luis ) huku ikiwa ina adhabu ya kusajiri tunaona inavyosukwa kitimu na sio "kimchezaji "mmoja...






Huyo Drinkwater Sion Kama Ni Bora Kama alivyokuwa Herera ambae alitemwa ..Au Ni Bora kuzidi Fred.. Au Ni Bora kuzidi Nemanja Matic ... Akija United atakumbwa na wanachokumbana nacho wakina Matic (Flop
 
Umecheza Misimu minne katika umri wa 21 wakati wenzako unakuta wanaanza kupata namba baada ya kuhitimu anapata namba kwa kusuasua umri 22 huko
 
Salah nilivyosoma historia yake hajapitia academy

Mane ndio ameishi maisha ya kubangaiza sana katika umri huu wa Rashford wa miaka 21 , Mane Na Salah wamestruggle sana mara sijui kufanyiwa majaribio ndio wakati dogo Rashford amekulia kwenye youth system Ya Club tajiri duniani tokea ana miaka nane huko
 
Tufanye Rashid katua pale Etihad ..paap ata fanya vitu anavyofanya Samatta kwa sasa? Tuseme tu ukweli kama Rashid angekuwa bora kama unavyosema basi angeweza kuamua matokeo kwenye game zenu mnazocheza ...Ku flop kwa hao ulowataja hakubadilishi chochote mkuu. Uko walipotoka walikuwa vizuri sana ..sasa Rashid kacheza timu gani said ya Man u? Atoke aende timu nyingine ili tuone uwezo wake ..tujue shida ni timu au ni yeye mwenyewe... Rashid ni overrated player mkuu ..timu ikiwa vizuri ndo tunaona anatakata ..kwanin ikiyumba hamna kitu anafanya...

Na ndo maana nikasema Samatta ana uwezo mkubwa wa kukipiga apo OT na kuleta matokeo mazuri kuliko uyo Rashid...

Kila la kheri Chelsea
 
Unaposema Rashford huwa Yuko vizuri timu ikiwa vizuri , Ni mwaka gani hii timu imekuwa vizuri !!! Nachojua Mimi tangu kuondoka kwa sir Alex furguson "Babu" timu haijawahi kuwa kwenye ubora wake ndio maana makocha wote baada ya furguson walifukuzwa na huyu tulie nae atafukuzwa kabla ya December ...



Nimekupa orodha ya wachezaji ambao walikuwa Bora zaidi ya Rashford ila baada ya kuja United wakaflop na baada ya kuondoka huko walipo wanauwasha Moto ( DEPAY, DI MARIA, DALEY BLIND, LUKAKU, MICK, Sanchez) ... SAsa Kama hawa wameweza kufanya vizuri huko walipo baada ya kuondoka United kwanini Rashford asiweze kufanya vizuri baada ya kuondoka United!!!??.... Usinifanye nikudharau "Kukuona Mbugila" kwa kuwa na tabia za "Double Standard"




Mbona wewe ulimuuza Mo Salah na ulimuona hafai na ukamuuza De Bruyne ambao wote tunajua wanachofanya. Walishindwa kutusua wakiwa Chelsea ila kwasasa mmoja ana Kikombe Cha UEFA ...



AMINI NAKWAMBIA ASILIMIA 98% YA WACHEZAJI WA UNITED WAKIENDA TIMU ZINGINE MADHUBUTI LAZIMA WAFANYE VIZURI KWASABABU NILIZOAINISHA HAPO JUU..


Kama unabisha hiki nisemacho ngoja nikuache.
 
Kwanza Nani kakwambia ukipitia Academy ndio unakuwa Bora !!... Na Nani kakwambia usipopitia academy huwi Bora ...


Sasa Kama hoja yako ni ubora wa mchezaji sio lazima kupitia Academy mbona huwazungumzii Christiano Ronaldo na Lionel Messi ambao wamepitia Academy na uwezo wao kisoka "Kusakata Ngozi" hakuna mchezaji yoyote wa uswahilini ameweza/ameweza na hakuna atakaekuja kuufikia katika kusakakata kandanda.....



Hivyo basi nikuombe upime uwezo wa hawa wachezaji wa wanayofanya uwanjani na sio mambo ya academy.
 
Sure
 
Academy hazina maana? Hivi mfano somo la Physics kukawa kuna wanafunzi wawili mmoja kafundishwa na mwingine hajaingia darasani nani unadhani anatakiwa kufaulu?
 
Vipi kuhusu future....???? Mwisho wa msimu, 2 to 5 years to come?

Kwamba mchezaji wa United aitamani Leicester au Cristal Palace kisa kwa sasa wanafanya vizuri

Akina Kante, Drinkwater waliacha timu yao ikiwa bingwa mtetezi, wakaenda Chelsea
Vipi kuhusu fedha??
 
Academy hazina maana? Hivi mfano somo la Physics kukawa kuna wanafunzi wawili mmoja kafundishwa na mwingine hajaingia darasani nani unadhani anatakiwa kufaulu?
Naomba uniquote ni wapi nimesema academy hazina maana.. Na ukiweza kuniquote kuwa nimesema academy hazina maana nitaandika ombi maalumu kwa Bwana Maxence Mello aniondoe humu Jamii Forum.


Nakuomba uache kunilisha maneno. Naona unajibu usivhokielewa.



Kuwa na wikendi Njema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…