Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hao uliowataja utawalinganisha na Mata, Rojo, Baily, Jones, Young, Smalling, Matic, Lingard, Sanchez?

Nimemaanisha hao wachezaji 18 ambao wapo toka 2015 hawapati namba ya uhakika Everton au Wolves.

Jaribu kupata picha leo hii Madrid wana hawa wachezaji tulionao sasa. Am sure wangevunja mkataba na zaidi ya nusu ya kikosi. Management yao ipo very ruthless.

Angalia tu hata Bale anavyoambiwa asepe, akipatikana mkataba watamfurumusha hutaamini japo ana mkataba wa muda mrefu.
 
Mkuu nakuomba kwa heshima zote umuondoe mtumishi wa wa Bwana "Marcus Rojo " katika hiyo orodha ya wahuni wa Tandika ..



Utakuwa umenifanya kuwa na sikukuu tamu kama ukimuondoa huyo mtu kwenye hicho kichaka..
Msimu huu Rojo hajafikisha hata mechi 15.

Ameshakuwa spana mkononi.

Aende tu.
 

Huo unaoita Uvivu na Kitokukimbiza unaweza ukaja mkuta hata huyo James.

Pace na kukimbiza mipira inategemea na mfumo wa timu.

Kama kocha si muumini ya Pace na kukimbiza mipira mirefu basi huyo dogo atakuja kucheza kama Martial.
 
Huo unaoita Uvivu na Kitokukimbiza unaweza ukaja mkuta hata huyo James.

Pace na kukimbiza mipira inategemea na mfumo wa timu.

Kama kocha si muumini ya Pace na kukimbiza mipira mirefu basi huyo dogo atakuja kucheza kama Martial.
Si kweli nahitaji kuuona huo mfumo, mwishoni wa mwezi wa 11 ambapo mou alikuwa anakaribia kufukuzwa kila mechi wapinzani wetu walikimbia zaidi yetu.

Mechi ya kwanza kabisa ambayo Ole alifundisha na tukashinda 5 maelekezo aliyowapa wachezaji ni kuhakikisha Hakuna timu inayokimbia zaidi yao. Ushahidi huu hapa
https://www.goal.com/en-tza/news/so...rs-to-never-ever-be/ner00cvrxbg41r9ktpd6owhb4

Amgalia timu zote kubwa hata zile zinazopiga pasi kama Barca na Man city wakipoteza tu mpira wanakaba kama nyuki kwa pamoja.

Kwetu sisi kuna "mafaza" kina Martial, pogba, Rashford etc kama wamevaa viatu vya Big G vile.
 
nimepata homa ghafla muda huu nipo ICU lakini sijapoteza maarifa yangu wala nguvu, hizi tetesi zitamtoa mwanadamu mjinga uhai wake.
magazeti ya ureno yameandika maneno haya:
Bruno Fernandes muito perto do Tottenham
Miguel Pinho reuniu-se com dirigentes dos londrinos, que vão avançar com uma proposta


kwa msaada wa google translator.
Bruno Fernandes very close to Tottenham, Miguel Pinho met with leaders of the Londoners, who will come up with a proposal.

gazeti la manchester evening news wanadai ya kwamba bruno fernandez usajili wake utatangazwa rasmi klabuni manchester united baada ya kumalizika kwa michuano ya european nation siku ya jumapili.

niwe mkweli sijawahi kuiamini manchester united kwenye ishu ya usajili haijalishi tetesi za kumuhitaji ngassa.
unakumbuka dili la ronaldinho gaucho lilivyogeuka kituko
unakumbuka dili la lucas moura tulivyopinduliwa na waarabu
unakumbuka dili la luka modric
vipi kuhusu sneijder
 
Kwa kweli hata Mimi hizo tetesi zimenipa wakati mgumu sana
 
Wanatafuta sababu za kununua waingereza tu! Ndio utaona dakika za mwisho wanavutwa akina declan rice kwa dharura utadhani walikuwa wamefungiwa.
 
Leo asubuhi nimepishana na shabiki wa liver akaniambia we simama usalimiane na Bingwa dah roho ikaumia sana na hizi dharau.
Halafu timu mpaka sasa haieleweki na usajili sifuatilii nitaona mwishoni nani kaja inatosha.
 
Leo asubuhi nimepishana na shabiki wa liver akaniambia we simama usalimiane na Bingwa dah roho ikaumia sana na hizi dharau.
Halafu timu mpaka sasa haieleweki na usajili sifuatilii nitaona mwishoni nani kaja inatosha.
Huyo jamaa amekosea sana ingetakiwa akwambie piga magoti hapo hapo ulipo umsalimie Bingwa
 
HILI GENGE LINA HALI MBAYA SANA......Kwishnei.........Kwisha habari yenu
 
AC MILAN mpya ya Uingereza mnajisikiaje kuitwa hivi hahahahahahahahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…