Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Nimewahi kusema hapa kuwa ma natural strikers wengi (karibu wote), De Lima, Inzagi, Raul, Kane, Aguero, Vardy, Drogba n.k huwa hawana mbwembwe za dribbling

Messi, CR7, Neymar, Hazard hawajawahi kuwa ma natural strikers ...... Mainly they are creators turned strikers or sometime false strikers
 
Fist touch ipi hiyo? Angalia yeye na Rashford au yeye na Martial nani anaongoza kupoteza mipira
Mkuu nimekusoma, baada ya kukumbuka kuwa Lukaku ni mfungaji bora wa muda wa belgium.
 
Mkuu nimekusoma, baada ya kukumbuka kuwa Lukaku ni mfungaji bora wa muda wa belgium.
Ndio hivyo Mkuu, tunachohitaji pale sio kubadili sura ya striker

Tunahitaji kubadili quality, striker ambaye ni mzuri zaidi ya Lukaku

Imagine Lukaku is just 24 years old, na ana magoli zaidi 40 timu ya Taifa ya Ubelgiji .... Yaani kwa umri alionao tayari ameshakuwa all time top goalscorer

Kuna mambo mazuri amefanya katika ngazi ya club alizopitia, japo sio katika top level

Pia jamaa ni moja kati ya ma creators WA goal scoring opportunities, sidhani kwa sasa United kuna mpiga krosi mzuri kama yeye na Dalot
 

Mkuu Muondoshe De Lima hapo
 

Mkuu unamjua de lima vizuri, de lima alikuwa mbwembwe kwenye dribbling zake hatari sheikh!! Mtoe kabisa kwenyr hiyo list, sio hadgi yake hao.
 
Ile kazi ya Football Director inamuhitaji MTU mwenye mawazo kama haya. Jamaa wanamtaka Ferdinand, sijui ni kupeana vyeo pale OT au nini? Kwahali iliyopo ilistahili apatikane Football Director mzoefu kutoka timu kubwa moja wapo ya Ulaya.
 
Mbona EDwin Van Desar alipata hii kazi bila uzoefu wowote ?
Ulishawahi kumwona Van Der Sar kwenye TV analaumu makocha ??
Yeye ni mmoja ya sababu ya Ajax kurudi kwenye soka la Ulaya mwaka juzi walifungwa fainali ya Uropa na mwaka huu wako nusu fainali ya Champions league licha ya kutumia budget ndogo kwenye usajili wao
 
Kwa maana hiyo kuna watu wazuri pia hata kama hawana uzoefu kutoka vilabu vikubwa vya ulaya
 
Kuhusu Sporting Director

Muda wa majaribio umepita pale OT, tulipaswa kupata mtu ambaye ameshaifanya ile kazi kwa mafanikio

Tumeweka kocha ambaye bado hajawa proved kwenye highest level

Ghafla tunakuja kwa Sporting Director ambaye hajawahi kufanya hiyo kazi

Kama ni lazima kuajiri ma legend, ninaimani wapo wengi ambao angalau wamefanya kazi kama hizo mfano Van de Sar na wengine wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…