Manchester United (Red Devils) | Special Thread


Nimeisoma hiyo meseji yako uliyasema haya tarehe moja December hii hii...wasipomfukuza Mourinho hata Europa league hawataiona next season.
 
Ajabu sana hii wakat van gaal alimtumia lingard kama 7
 
Mourihno sometimes naona kama ni mtu anayebahatisha tu..game plan zake recently ni za ovyo ovyo sana...Matic anaonekana kabisa miguu imekuwa mizito lakini bado kocha ana stick naye tu..

Anamtoa Dalot anamwingiza Fellaini..nje kuna Mata,Martial...Huu si upuuzi huu mkuu

Poor Mourihno..
 
tunakumbushana jamani leo ni jumatatu tulivu lakini huenda ikageuka na kuwa jumatatu yenye machungu.
  1. barcelona
  2. real madrid
  3. bayern munich
  4. man city
  5. dortmund
  6. fc porto
  7. psg
  8. juventus.
kama kuna mdau anayeamini porto na dortmund ni wepesi anahitajika kurudi nyuma na avute kumbukumbu mechi dhidi ya sevilla msimu uliopita.
hivi kuna timu isiyotaka kupangiwa na manchester hii yenye goal 0 kwenye mechi 17?
msimu uliopita tulishindwa kuimaliza game nyumbani kwetu na msimu huu tunatakiwa tukamalize gemu ugenini.
 
Binafsi nimekata tamaa kwa upangaji ule wa timu hadi wakina fabinho wanang'aa dhahiri hamna kocha hana mbinu kila mmoja tulipokuwa tukiangalia mpira alishangaa sana 4 playars wa maana wapo bench
 
Mpira unabadilika kila kukicha wahitaji viungo wengi kama pilau wenye kasi na maamuzi ya haraka watu wakubwa kama nyumba muda wao wa kucheza unazidi kupungua big fella mzito hana kasi sijui mwalimu alifikiria nini? unapofikiria mipira ya juu wenzio wanapita chini na kuua hiyo game plan yako. Tumestahili kufungwa na tunahitaji kubadilika sana
 
Ndo mana pep anafukuza vi academy hivi ukiviendekeza unavuna mabua kajitu hakawezi hata kutengeneza nafas wala ku drible kakifunga leo goli hadi mwakan mwez wa 3 kanapangwa kisa kanakimbiakimbia akimbie na jana


Rashford namuona kabisa kila mech anajaribu kuleta kitu tofaut ana drible anakimbia anatengeneza nafasi anaweza kumtoka bek haka hata kukakingia kifua rahisi lakin kale ka ku dab na kushek hovyo sana
 
Poleni jana mlipigwa na kitu kizito sana! Hope mnaendelea vizuri
 
 
Hahaha,kwetu wachezaji wanaoweza kukokota mpira hawana nafasi kabisa. Angalia Pereira, mata,Fred wote hao kwasababu sio wazuri kwenye mbinu za kocha za kukaba wanaonekana sio kitu.

Hii timu ukimleta mtu kama Pochettino tunabeba ubingwa asubuhi na mapema.

MUFC ina wachezaji wazuri ila mbinu za kocha ni za kizamani mno.

Tazama kulikuwa na haja gani ya kuanza na mabeki watano?katikati viungo wote hamna wa kutengeneza,Matic akizongwa tu anaachia mpira kama mgonjwa kazi yote inamuelemea Herrera.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…