Ianni, Sarri na Mourinho, yameisha.!
Baada ya Ross Barkley kufunga goli la kusawazisha katika dikaka za majeruhi , kocha msaidizi wa Maurizio Sarri , Marco Ianni alitoka kwenye benchi lake na kwenda kushangalia mbele ya Jose Mourinho na kuibua tafrani katika eneo la ufundi.
" Sichukizwi na kitu chochote, kilichotokea na msaidizi wa Sarri , Sarri ndio alikuwa wa kwanza kuja kwangu na kuniambia kwamba atalifanyia kazi."
"Ianni ameshakuja kwangu na kuomba msamaha , nimemuambia sahau kuhusu hilo, hata mimi nilishafanya makosa mengi kwenye maisha yangu ya soka."