Mimi Naamimi Kuna Jambo Haliposawa Kwa Mourinho! Ni kweli Hakosi la Kujibu ila Ni Vizuri aconcentrate kwenye Hoja zitokanazo na Maswali anayoulizwa. Kwakweli Majibu Ya Mourinho Kwenye Press Conference yamenifanya nizifuatilie Hizi Conferences zake.
Kinacho nishangaza Ni Kwanini Anapoulizwa Maswali Kuhusu Man United na Reporters Wa Man U yeye Katika Majibu Yake Hufanya Matatizo Ya Liverpool Kuwa Ndiyo Kigezo na hoja Yake Kubwa ya Utetezi??
Kwamfano alipoulizwa Mwenendo Wa Timu Yake alijibu "Watu Wananilaumu Mimi Niliyemaliza Nafasi ya Pili (Last Season) na Kumuona Bora Mtu (Klopp) ambaye Hajashinda Chochote".
Sasa Liverpool inahusu Nini Katika Press Zake Jamani? Mourinho huwa Hakosi Jibu Hata Kama lipo nje Ya Mada.
Na njia moja ya Kujitetea kwake Ni Kushambulia Bodi, Wachezaji na Makocha Wa Timu Nyengine.