- mourinho: baadhi ya wachezaji wa sevilla wana uwezo wa kuichezea manchester united.
- mourinho : tunahitaji viungo wawili msimu ujao
- mourinho: guardiola licha ya kurithi kikosi bora lakini bado amefanya matumizi makubwa sana kwa dhumuni la kujenga timu yake.
- mourinho : tunahitaji kutumia pesa kama manchester city ndipo tutaweza kushinda ubingwa.
- mourinho: nataka nitakapoondoka ndani ya klabu hii mrithi wangu akute wachezaji bora.
- ed woodward (CEO) : Manchester united ni brand kubwa sana duniani na tuna uwezo wa kumsajili mchezaji yeyote anayehitajika na benchi la ufundi.
nimejaribu kuunganisha hizi nukuu zilizowahi kuzungumzwa na watu muhimu kwenye klabu pendwa ya manchester united.
msimu uliopita tuliona mapungufu mengi sana kwenye timu yetu na mpaka muda huu ambao dirisha la usajili nchini uingereza limebakisha siku takribani 20 sijaona dalili ya klabu yetu kutatua matatizo yalioonekanwa kwenye msimu uliopita.msimu uliopita tuliona udhaifu kwenye eneo la mlinzi wa kushoto na mpaka leo klabu haijafanya maamuzi ya kusajili mlinzi bora wa kushoto.
- mlinzi wa kulia pia tuna udhaifu mkubwa sana lakini usajili tulioufanya ni wa kinda anayeitwa diogo dalot mchezaji ambaye haonyeshi dalili ya kumpa ushindani antonio valencia kwa msimu huu labda tusubiri msimu unaofuata. kama klabu ilikuwa imedhamiria kutatua changamoto ya upande wa kulia ilipaswa isajili mlinzi anayekaribiana na viwango vya trippier, pavard na sidibe. kama kweli united ni brand kubwa kwenye dili za usajili kwa nini tunashindwa kutumia pesa kwa ajili ya kutafuta mlinzi mwenye kiwango kikubwa kama walivyofanya man city kwa kyle walker?
- ameondoka michael carrick na nafasi yake amesajiliwa fred, tunategemea kuwa ni usajili bora kwa msimu huu mpaka sasa kwenye timu yetu. cha kushangaza klabu imemuongezea mkataba marouanne fellaini wa kuendelea kubaki manchester united, ina maana kwa dalili zinavyoonyesha hatutasajili tena kiungo mwenye ubora na back up yetu ataendelea kuwa fellaini.kwa akili ya kawaida kumbe kama michael carrick angeliendelea kuwa mchezaji wa timu yetu tusingefanya usajili wa kiungo. Pia kupewa mkataba kwa fellaini kwa mtazamo wangu hakuleti tafsiri nzuri kwa vijana kama perreira na mc tominay hivyo basi ina maana jose mourinho alikuwa anatudanganya pale aliposema anahitaji kusajili viungo wawili?
- sitaki kulizungumzia eneo la ulinzi wa kati ambalo nalo ni shidaa kiupande wetu
- sitaki kulizungumzia eneo la kiungo wa kulia ambalo nalo ni shida kiupande wetu
- pia sitaki kulizungumzia eneo la namba 10 mwenye ubora ambalo ndani ya timu yetu hatuna.
hivi ule ubabe wa mourinho kwenye soko la usajili aliokuwa nao chelsea umeishia wapi?
hainiingii akilini walinzi wetu wa kikosi cha kwanza ni
jones na
smalling ambao wanawekwa nje na
john stones halafu bado mourinho haonyeshi dalili ya kutafuta mlinzi mwenye roho ngumu kama
diego godin.
hainiingii akilini ninapoona winga wetu ni
mata na
lingard na wakati huo huo barcelona ambayo ina dembele na messi upande wa kulia wanapeleka offer ya tatu kwa
willian halafu sisi tupo kimya kama maji ya mtungini.
nadhani kati ya mourinho na ed woodward mmoja kati ya wawili hao anatudanganya.
nawakumbusha mashabiki na wapenzi wenzangu wa manchester united ya kwamba wale vilaza ambao msimu huu wanatimiza mwaka wa 26 bila ya ubingwa wa ligi kuu ya uingereza tayari wameshatatua matatizo yao makubwa yaliokuwa yakiwakabili.
allisson
fabinho
nabil keita
shaqiri
na bado hawajatosheka na huku upande wa pili kwa majirani waliotupita kwa points 18 msimu uliopita wamemuongeza
ryad mahrez kwenye kikosi chao na bado wanaendelea kutafuta mbadala wa
yaya toure.
ngoja tuendelee kuwa wavumilivu kama tunavyozivumilia millioni 50 za kila kijiji.