Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kwa Man Utd wenzangu hivi mnajua kuwa kwenye PL Paul Pogba akicheza hatufungwi? Sasa hivi PP hajafungwa mechi 35! Tulizofungwa na Chelsea, Huddersfiel na Man City zote hakucheza.
Pia kwa wale haters wa Pogba wa kutoka vitimu vingine mjue Paul Pogba is invincible.

Paul Pogba was brilliant in Manchester United's 3-0 win over Stoke at Old Trafford. Find out why the Frenchman is the Premier League's invincible...

Paul Pogba could be forgiven for wondering what the fuss is all about with Manchester City. While Pep Guardiola's leaders lost their own unbeaten record this season, the Manchester United midfielder's run goes on. The 3-0 victory over Stoke on Monday Night Football made it nine wins and four draws for Pogba this season. It is a sequence that dates back to 2016.

Pogba is unbeaten in his last 35 Premier League matches, far more than any other player in the competition. Gabriel Jesus is the next man on the list with 28 games unbeaten. David Silva has gone 25 without losing. Pogba missed the home defeat to Manchester City and the losses at Huddersfield and Chelsea. But much more significantly, United missed him.

Paul Pogba starred against Stoke and is now unbeaten in 35 games

paul-pogba-manchester-united-premier-league-graphic_4206666.jpg

😀 😀 😀 😀 Spurs nuksi kweli!! Kwa makusudi bila ya Kulazimishwa au Kushawishiwa na Mtu Kaamua Kukivunja Kirekodi Uchwara... 😀 😀 😀
 
Pogba na mbinu mbovu za Mourinho zilivyoisadia Spurs

Manchester United wana tatizo juu ya Paul Pogba. Ni mchezaji muhimu ambaye bila uwepo wake ni shida, lakini pia anayefanya maisha kuwa magumu kwa kwa kikosi cha Jose Mourinho pindi anapopewa majukumu ambayo hana uwezo nayo.

img_3433.jpg

Na kuthibitisha hilo katika mchezo dhidi ya Tottenham Hotspur katika dimba la Wembley juzi Jumatano, Pogba alionyesha kiwango kidhaifu zaidi tangu ajiunge na United, na baada ya dakika 62 alitolewa nje na kocha wake Jose Mourinho. Timu yake ikiwa nyuma kwa magoli 2-0 na bado wakiwa wanapigiwa mpira mwingi na Spurs, ambao wachezaji wake 11 walikuwa na majukumu ambayo waliyamudu kulingana na uwezo wao, jambo lilopelekea kucheza vizuri zaidi ya wapinzani wao.
img_3431.jpg

Turudi kwa Pogba, kiungo mwenye thamani ya £89m anayeifanya United icheze vyema sana …. anapopangwa mahala ambapo kunaendana na uwezo wa kipaji chake. Pale Wembley, alikuwa akicheza kwenye safu ya viungo wawili – akicheza pembeni ya Nemanja Matic – lakini, akiwa na miaka 24 hivi sasa, Pogba bado hajawiva kwenye kuwa na nidhamu kwenye ulinzi ili kuweza kucheza kwenye nafasi hiyo vizuri. Hivyo pindi anapochezeshwa kwenye mfumo wa viungo wawili anakuwa tatizo hasa pindi timu yake inapocheza dhidi ya timu bora.

Matamanio yake ya kwenda kucheza mbele zaidi hayaepukiki na mara zote amekuwa akipanda mbele na kumuacha Matic pekee yake na walinzi wakiwa hawana ulinzi wa kutosha, na hili lilionekana dhidi ya safu kali ya ushambuliaji ya Spurs, ambao waliishinda mechi ndani ya nusu saa tu ya mchezo.

Kama kiungo wa kati wa hadhi ya Pogba – anatakiwa kuwa na uwezo wa kuwa na umakini mkubwa ili kuweza kucheza kwa jukumu la kuzuia endapo atatakiwa kufanya hivyo kutokana na mazingira. Lakini hawezi kufanya hivyo, hilo limeshaonekana na sasa ni wazi ni ubishi wa Mourinho kubadili mbinu na sio kumtuma mchezaji wake staa kufanya kazi ya kuzuia mashambulizi dhidi ya wachezaji aina ya akina Dele Alli na Christian Eriksen.

Baada ya kuona Pogba akishindwa kutimiza maagizo aliyompa pamoja na kujaribu mara kadhaa kwa zaidi ya saa 1 ya mchezo – Mourinho aliamua kumtoa Pogba na kumuingiza Fellaini.

Chini ya Mourinho, baadhi ya wachezaji wamekuwa wakipewa ulinzi kuliko wengine – mmoja wao ni Pogba, lakini jana hali ilikuwa tofauti. .

copypasteimage-16.jpg

Kutolewa katika mchezo dhidi ya Spurs baada ya kucheza kwa dakika 60, muda mfupi baada ya kuonekana akisemeshana kwa nguvu na Mourinho katika kipindi cha kwanza – kwa Pogba hili jambo zuri. Tangu aliporejea United akitokea Juventus, jana ilikuwa mara yake ya 4 kushindwa kumaliza mechi ya Premier League ambayo alianza.

Mchezo wa kwanza ulikuwa dhidi ya Crystal Palace mwezi May 2017, hapa Mourinho alimtoa kwa ajili ya kumuandaa na mchezo wa fainali ya Europa League vs Ajax, pia mnamo November 2017, akiwa ametoka kwenye majeruhi Pogba alicheza kwa dakika 70 tu, pia mchezo mwingine ambao hakumaliza ni ule aliopewa kadi nyekundu vs Arsenal.

Lakini safari hii vs Spurs, Pogba alitolewa kwenye mchezo kwasababu za kiufundi kama Mourinho alivyoeleza – kwamba alimuondoa kwa kuwa hakuwa anacheza vizuri. Hata hivyo Mourinho pia hawezi kuepuka lawama.
img_3432.jpg

Kama Mourinho angempanga Ander Herrera pembeni ya Matic na kumtumia Pogba kucheza mbele yao, kama ilivyokuwa katika mchezo vs Everton mwezi uliopita wakati Pogba alipocheza kwa kiwango cha juu na kufanikiwa kuwa Man Of The Match – basi kiungo huyo mfaransa asingechexa vibaya vs Spurs kwa sababu angecheza eneo analolimudu zaidi kwa ufanisi mkubwa.

Lakini usajili wa Alexis Sanchez, ambaye ameiongezea makali safu ya ushambuliaji ya United, lakini pia ameleta mkanganyiko wa mbinu na majaribio ya kulitatua tatizo hilo lilifeli vibaya vs Spurs.

Wakati Pogba akicheza chini, Mourinho alimtumia Sanchez, Martial na Jesse Lingard nyuma ya mshambuliaji wa kati.

img_3424.jpg

Martial na Lingard wameonyesha kwanini wanastahili nafasi katika kikosi cha kwanza hasa katika mechi za hivi karibuni, wakati Sanchez ilikuwa lazima aanze lakini watatu hao hawawezi kucheza nyuma ya mshambuliaji.

Kwanza kwasababu inamuondoa Pogba katika kucheza kwenye nafasi anayoimudu zaidi – nafasi ambayo anakuwa hatari zaidi kwa timu pinzani lakini pia inapelekea Mourinho kumpa majukumu mengine ambayo hayaendani na uwezo wake. Pogba sio mzuri kwenye kufanya ‘tackling’, sio mzuri kwenye kuzuia mipira ya juu na pia hana uwezo mkubwa wa kugundua hatari mapema kama ilivyo kwa viungo wa ulinzi. Pia anakosa nidhamu ya kubaki nyuma.

Kama au endapo Mourinho atafanya usajili wa kiungo mrithi wa Michael Carrick ambaye atacheza pamoja na Matic, Pogba atakuwa huru kucheza kwenye kiungo cha kushoto mbele – sehemu ambayo anaimudu vilivyo. Akileta madhara kwa timu pinzani na uwezo wake wa kuichezesha timu – akiwa kiunganishi cha nafasi ya ulinzi na ushambuliaji huku akitengeneza nafasi kwa washambuliaji.

Yote kwa yote, mchezo wa Spurs ulikuwa ukumbusho mwingine kwamba Pogba sio kiungo mkabaji na Mourinho alifanya makosa kumchezesha kwenye ulinzi vs Spurs.
Sahihi
 
Mkuu ujifunze mpira...Mpira ulipokuwa unaanzishwa wachezaji wa Totenham walikuwa wamezidi(wamevuka mstari wa katikati) ilitakiwa mpira urudiwe kuanzishwa lakini ikaacha watu wakaenda kufunga (search hiyo clip uingalie kabla hujakurupuka kurudi hapa kujibu) achilia mbali ile ya Sanchez kufyekwa miguu makusudi na Dele Ali na refa akaishia kwenye yellow pekee.

Miaka Yote Niliyofuatilia Soka Sikuwahi Kuwaona Washabiki Wa Man United Wakililia Matukio Uwanjani...

Najiridhisha Kuwa Wewe si Mshabiki Wa Man United, Bali Ni Mshabiki Wa [HASHTAG]#Kulialia[/HASHTAG] UnitedUnited.
 
Ukijaribu kuangalia kwa makini game ya Spurs Juzi, utagundua kwa haraka Sana wachezaji wa Utd hawakucheza to their fullest abilities either kwa kupenda au kutopenda na hakukua na ile fighting spirit kwa badge ya timu.

Spurs walikua wakipoteza Mpira wanakabia juu haraka na kwa ufanisi mkubwa, which in turn Utd wakawa wanashindwa ku plan for attacking game quickly. Hali ilikua tofauti na Utd wakipoteza Mpira, instead ya kukaba instantly huko huko juu wao walikua wanarudi nyuma na kuacha spaces kwa players wa Spurs ku plan their attacks very freely kwa sababu hakuna bugudha ya kukabwa na opponents wao.

Hiki kitu kiliigharimu time Sana, Sijui ndio tactic ya kocha ama Nini, ila kwa muono wangu unapocheza na timu inayo build up attacks very fast hutakiwi kuacha wawe free kama Utd ilivyo fanya Juzi.

Otherwise, Sanchez Is a bargain..

GGMU..
 
What a wonderful analysis
 
In front of Dele Alli and Eriksen Pogba is Vulnerable! 😀 😀 😀 😀
Mkuu acha chuki za kijinga...PP anaongelea rekodi ya mechi 35 bila kufungwa wewe unaongelea Dele na Ericsen ambao hawajafikisha rekodi ya kutofungwa mechi 4.!!!!
 
In fact You are the real invincible
 
Baadhi ya wachambuzi wana maoni kama haya, na Mimi huwa sipo nao mbali na ndio maana kuna ndugu yangu humu tuliwahi kusuguana sana juu ya maoni ya Paul Scholes alipoongea kwa uchungu sana kuhusu commitment ya Pogba kwa timu hasa ukizingatia Pogba ndio roho ya timu akizingua na timu kuna uwezekano Mkubwa Wa kuzingua. Mourinho badala ya kusimamia ukweli akaamua kuwalaghai watu kwamba Scholes anamuonea wivu Pogba kwa sababu ya hela zake anazopata. Na kwa bahati nzuri kwake akapata wafuasi katika hilo hata humu JF
 
Attachments

  • Screenshot_20180203-092316.png
    Screenshot_20180203-092316.png
    34.8 KB · Views: 43
Anaweka midfield matic, lingard na pogba wakati anajua kabisa lingard na pogba wanapenda kupanda juu kushambulia na kuacha gap kubwa hapa katikati kwa adui kupita kirahisi. Kule mbele tayari tuna visu vikali, ingetakiwa matic na herrera wakae katikati kuwapa support mabeki na pogba ndiye awe midfielder huru kupanda mbele kuwasaidia martial, lukaku na sanchez.
Sema mourinho sometimes simwelewagi mipango yake.
 
Pogba na mbinu mbovu za Mourinho zilivyoisadia Spurs

Manchester United wana tatizo juu ya Paul Pogba. Ni mchezaji muhimu ambaye bila uwepo wake ni shida, lakini pia anayefanya maisha kuwa magumu kwa kwa kikosi cha Jose Mourinho pindi anapopewa majukumu ambayo hana uwezo nayo.

img_3433.jpg

Na kuthibitisha hilo katika mchezo dhidi ya Tottenham Hotspur katika dimba la Wembley juzi Jumatano, Pogba alionyesha kiwango kidhaifu zaidi tangu ajiunge na United, na baada ya dakika 62 alitolewa nje na kocha wake Jose Mourinho. Timu yake ikiwa nyuma kwa magoli 2-0 na bado wakiwa wanapigiwa mpira mwingi na Spurs, ambao wachezaji wake 11 walikuwa na majukumu ambayo waliyamudu kulingana na uwezo wao, jambo lilopelekea kucheza vizuri zaidi ya wapinzani wao.
img_3431.jpg

Turudi kwa Pogba, kiungo mwenye thamani ya £89m anayeifanya United icheze vyema sana …. anapopangwa mahala ambapo kunaendana na uwezo wa kipaji chake. Pale Wembley, alikuwa akicheza kwenye safu ya viungo wawili – akicheza pembeni ya Nemanja Matic – lakini, akiwa na miaka 24 hivi sasa, Pogba bado hajawiva kwenye kuwa na nidhamu kwenye ulinzi ili kuweza kucheza kwenye nafasi hiyo vizuri. Hivyo pindi anapochezeshwa kwenye mfumo wa viungo wawili anakuwa tatizo hasa pindi timu yake inapocheza dhidi ya timu bora.

Matamanio yake ya kwenda kucheza mbele zaidi hayaepukiki na mara zote amekuwa akipanda mbele na kumuacha Matic pekee yake na walinzi wakiwa hawana ulinzi wa kutosha, na hili lilionekana dhidi ya safu kali ya ushambuliaji ya Spurs, ambao waliishinda mechi ndani ya nusu saa tu ya mchezo.

Kama kiungo wa kati wa hadhi ya Pogba – anatakiwa kuwa na uwezo wa kuwa na umakini mkubwa ili kuweza kucheza kwa jukumu la kuzuia endapo atatakiwa kufanya hivyo kutokana na mazingira. Lakini hawezi kufanya hivyo, hilo limeshaonekana na sasa ni wazi ni ubishi wa Mourinho kubadili mbinu na sio kumtuma mchezaji wake staa kufanya kazi ya kuzuia mashambulizi dhidi ya wachezaji aina ya akina Dele Alli na Christian Eriksen.

Baada ya kuona Pogba akishindwa kutimiza maagizo aliyompa pamoja na kujaribu mara kadhaa kwa zaidi ya saa 1 ya mchezo – Mourinho aliamua kumtoa Pogba na kumuingiza Fellaini.

Chini ya Mourinho, baadhi ya wachezaji wamekuwa wakipewa ulinzi kuliko wengine – mmoja wao ni Pogba, lakini jana hali ilikuwa tofauti. .

copypasteimage-16.jpg

Kutolewa katika mchezo dhidi ya Spurs baada ya kucheza kwa dakika 60, muda mfupi baada ya kuonekana akisemeshana kwa nguvu na Mourinho katika kipindi cha kwanza – kwa Pogba hili jambo zuri. Tangu aliporejea United akitokea Juventus, jana ilikuwa mara yake ya 4 kushindwa kumaliza mechi ya Premier League ambayo alianza.

Mchezo wa kwanza ulikuwa dhidi ya Crystal Palace mwezi May 2017, hapa Mourinho alimtoa kwa ajili ya kumuandaa na mchezo wa fainali ya Europa League vs Ajax, pia mnamo November 2017, akiwa ametoka kwenye majeruhi Pogba alicheza kwa dakika 70 tu, pia mchezo mwingine ambao hakumaliza ni ule aliopewa kadi nyekundu vs Arsenal.

Lakini safari hii vs Spurs, Pogba alitolewa kwenye mchezo kwasababu za kiufundi kama Mourinho alivyoeleza – kwamba alimuondoa kwa kuwa hakuwa anacheza vizuri. Hata hivyo Mourinho pia hawezi kuepuka lawama.
img_3432.jpg

Kama Mourinho angempanga Ander Herrera pembeni ya Matic na kumtumia Pogba kucheza mbele yao, kama ilivyokuwa katika mchezo vs Everton mwezi uliopita wakati Pogba alipocheza kwa kiwango cha juu na kufanikiwa kuwa Man Of The Match – basi kiungo huyo mfaransa asingechexa vibaya vs Spurs kwa sababu angecheza eneo analolimudu zaidi kwa ufanisi mkubwa.

Lakini usajili wa Alexis Sanchez, ambaye ameiongezea makali safu ya ushambuliaji ya United, lakini pia ameleta mkanganyiko wa mbinu na majaribio ya kulitatua tatizo hilo lilifeli vibaya vs Spurs.

Wakati Pogba akicheza chini, Mourinho alimtumia Sanchez, Martial na Jesse Lingard nyuma ya mshambuliaji wa kati.

img_3424.jpg

Martial na Lingard wameonyesha kwanini wanastahili nafasi katika kikosi cha kwanza hasa katika mechi za hivi karibuni, wakati Sanchez ilikuwa lazima aanze lakini watatu hao hawawezi kucheza nyuma ya mshambuliaji.

Kwanza kwasababu inamuondoa Pogba katika kucheza kwenye nafasi anayoimudu zaidi – nafasi ambayo anakuwa hatari zaidi kwa timu pinzani lakini pia inapelekea Mourinho kumpa majukumu mengine ambayo hayaendani na uwezo wake. Pogba sio mzuri kwenye kufanya ‘tackling’, sio mzuri kwenye kuzuia mipira ya juu na pia hana uwezo mkubwa wa kugundua hatari mapema kama ilivyo kwa viungo wa ulinzi. Pia anakosa nidhamu ya kubaki nyuma.

Kama au endapo Mourinho atafanya usajili wa kiungo mrithi wa Michael Carrick ambaye atacheza pamoja na Matic, Pogba atakuwa huru kucheza kwenye kiungo cha kushoto mbele – sehemu ambayo anaimudu vilivyo. Akileta madhara kwa timu pinzani na uwezo wake wa kuichezesha timu – akiwa kiunganishi cha nafasi ya ulinzi na ushambuliaji huku akitengeneza nafasi kwa washambuliaji.

Yote kwa yote, mchezo wa Spurs ulikuwa ukumbusho mwingine kwamba Pogba sio kiungo mkabaji na Mourinho alifanya makosa kumchezesha kwenye ulinzi vs Spurs.

Nategemea mechi ya leo Herrera atanza na Matic, Pogba akicheza 10.
 
View attachment 688865
Mourinho hakupaswa kumuacha Eric dier alitakiwa kumsajili huyu kipindi wanataka paund 48 kiungo cha ukabaji na kuwalinda mabeki anavitendea haki sana pogba na matic wangekuwa huru sana.

Namkubali sana huyu jamaa.
Matic angekuwaje huru sasa mkuu? Dier na Matic wote wanacheza position moja, wangekuwepo wote timu moja labda mmoja akae bench. Role yao wote wawili ni kama ilivyo kwa kante, fernandinho, casemiro
 
Back
Top Bottom