Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hii picha ya Mkhtaryan Leo mchana alipokuwa anaondoka kwenye viwanja vya mazoezi "Carrington" imeniumiza moyo sana. Ukimuangalia kwa makini jamaa machozi yanamlenga na inawezekana alilia kabisa. Hata mazoezi hakufanya nahisi kwa sababu kocha ashamtoa jamaa kwenye mipango yake. Na inasemekana jamaa anaumia sana kitendo cha Man U kum push aondoke ili aje mchezaji mwingine kiasi kwamba kumuona yeye ni nuksi Wa ucheleweshaji wa ujio Wa Alexis. Maisha yana changamoto asee!
 

Attachments

  • 330919.jpg
    13.3 KB · Views: 39
Dah hata mie imeniumaaa inabidi aende tu Kambi popote iwe mvua iwe jua maisha lazima yaende
 
Paul Pogba ana mchezo wenye ubunifu zaidi ya kiungo wa kati wa Manchester City Kevin De Bruyne, kulingana na takwimu.
Mchezaji huyo wa Manchester City amekuwa akionyesha mchezo mzuri katika kikosi cha Pep Guardiola msimu huu.
Lakini ni kiungo wa kati wa Manchester United aliyevunja rekodi ya usajili ambaye amefaa zaidi uwanjani.
Pogba ametoa pasi tisa za magoli katika mechi 13 za Man United.

De Bruyne amefanikiwa kutoa pasi kama hizo lakini katika mechi 23.
Usaidizi wa pasi zinazotolewa na Pogba ili kupata magoli ni mzuri zaidi ya mchezaji yeyote yule katika ligi tano za bara Ulaya msimu huu.
Paul Pogba (Man Utd) - Pasi 9 katika mechi 13
Neymar (PSG) - Pasi 9 katika mechi 14
Philipp Max (Augsburg) - Pasi 9 katika mechi 18
Pione Sisto (Celta Vigo) - Pasi 9 katika mechi 19
Leroy Sane (Man City) - Pasi 9 katika mechi 21
Kevin De Bruyne (Man City) - Pasi 9 katika mechi 23

Kevin De Bryune ametoa usaidizi kama huo wa Pogba lakini katika mechi 10 zaidi.
Neymar anamfuata Drogba katika jedwali la kutoa pasi zilizozaa magoli.
Hatahivyo, licha ya Pogba kuwasaidia wachezaji wenzake , ni safu ya mashambulizi ya Manchester United ambayo imekifanya kikosi cha Jose Mourinho kuwa nyuma ya Manchester City kwa pointi 12.

Antonio Valencia, Anthony Martial na Romelu Lukaku wote walifunga wakati United ilipoicharaza stoke City mabao 3-0.
Pogba alihusika katika kutoa pasi ya bao lililofungwa na Valencia kunako dakika ya tisa na bao la Martial dakika ya 29 baadaye.
Kwa jumla msimu huu City imefunga mabao 67 huku majirani zao wakifunga magoli 48.
 
Mshambuliaji wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan, 28, yuko huru kuhama kwenda London kujiunga na Arsenal. (Mirror)

Kiungo wa kati raia wa Armenia, Henrikh Mkhitaryan, 28, anasema anataka nyongeza ya mshahara kuweza kuhama Manchester United kwenda Arsenal. (Mirror)
 
Acha niisave hii picha ipo siku nitaishusha hapa akianza vitu vyake popote atakapoenda. Picha inaumiza sana hii
 
Mchanganyiko mzuri wa lukaku na yule beki wenu lindorf acha mahaba mkuu stock city ana squad kubwa kuliko man
 
Kabla nilikuwa sijakuelewa lakini now nimekuelewa kwa lugha uliyotumia, ni sahihi now Lingard anafanya vizuri mno, magoli 10 katika msimu mmoja ni kitu kizuri lakini ni mapema mno kumtumia yeye kama mfano wa kukuza vipaji kwa Mou, tujiulize Ni sahihi kwa Kipaji na Kiwango cha Martial na Performance yake uwanjani kwa msimu? Rejea msimu uliopita? Naamini akipewa nafasi zaidi na akiwa huru uwanjani anaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya haya tunayoyaona sasa, Kwa kipaji na Kiwango cha Martial ni kizazi cha Mbappe kama sio Neymar!! Ila naamini mfumo, falsafa na Itikadi za Mou zinarudisha nyuma Kiwango chake, Ye mwenyewe ameripotiwa mara nyingi akilalamika kuhusu nafasi na majukumu anayopewa uwanjani na hata kiwango chake sio Consistence ni kinapanda na kushuka tofauti na makinda wenzake.

Tunaona consistence ya kiwango cha De Bruyne wa Man City kikikuwa match to match.

Tumeona Floppy ya Mikh,

Simuoni Mourihno kama mlezi mzuri wa wachezaji wenye vipaji hasa makinda, jaribu kulifatilia hili.

Angalizo:- ni shabiki wa damu wa Man United guys tuwe huru zaidi na tujenge hoja bila kudhihakiana, kutukanana na kuvunjiana heshima, naamini humu sote ni waungwana na mashabiki wa Damu wa Man United.
 
Kocha gani ambae anachukua makombe halafu kikosi chake sio cha gharama kubwa?
Nisaidie nadhani anamaanisha kuwa Mourihno ni aina ya Makocha wanaopenda kuwa na wachezaji waliotayari kwa mapambano, wachezaji waliokamilika au waliokuwa ili iwe rahisi ye kuwapa majukumu na sio hawa wanaokuwa/vijana/makinda
 
Sawa pamoja na kuwa ya hovyo lakini inawezekana hukuielewa post yangu vizuri, nimeiongelea game ya Liverpool vs Man City, nimeisifia Stike ya Liverpool kwenye game na Man City tu kama mfano au hadidu na rejea yangu.

Lakini siamini kama hawa wote uliowataja ni washinda ni au kipimo chetu kwa sasa.

Wapinzani wetu ni Man City katika EPL wametuzidi kila kitu, Point na hata Goal difference, ni kweli Strike yetu haijafunga magoli mengi kama ilivyo kwa City.

Lakini hata hao tuliowazidi ni kwa magoli machache, tofauti kati yetu na City ambapo kuna pengo kubwa, City ana uwiano mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa dhidi yetu.

Kwa kuingalia Man City basi bado kuna kazi kubwa ya Kufanya, City wana magoli Mengi ilihali sisi tuna magoli machache.

Simuongelei David Moyes mana hakuwa na sifa za kuifundisha Man Unite au kuwa mrithi wa Sir, na nilishangaa alivyopewa timu sikutegemea makubwa kutoka kwake, na pale ndio mwanzo wa kuharibika historia yetu.

Nakubaliana na wewe kuwa tunahitaji heshima na Makombe lakini hoja yangu ni kucheza soka la nguvu na la kushambulia zaidi kama ilivyokuwa Man United ya Sir Alex.

Fergurson hakuwa na timu ya kutisha lakini wachezaji walikuwa na njaa na kiu ya kutafuta ushindi muda wote walikuwa wanapambana.

Luis Van Gaal nadhani tuliwahi kumtimua Falsafa zake zilihitaji misimu zaidi ya minne kuleta matunda, alikuwa analeta aina mpya ya soka pale old T.
 
[/QUOTE]

Nashukuru kwa Homework@Chief Mkwawa, tuendelee kujenga hoja na kufahamishana.

Tunapokosea tuelekezane, ila tunaokosa pia tunaenda kuona mabadiliko kupata mafanikio makubwa zaidi ya haya, lazima turudi kwenye Ufalme wetu.
 
Ukikumbuka alikuwa Top classic player duniani hivi karibuni, aliamini furaha yake ingekamilika pale Old Trafford kwa kucheza kwa heshima na kwa muda mrefu, lakini ndio hivyo ameshushwa thamani kwa kubadilishwa na mchezaji, hapewi nafasi ya kuchagua timu, kuondoka kwa Heshima, ila Kwangu Mikh atabaki kuwa mmoja ya wachezaji wazuri mno tuliowahi kuwa nao lakini tulioshindwa kutumia uwezo wao.

Jamaa ni fundi haswa, tumtakie maisha mema na yenye mafanikio huko aendako.
 
Mchanganyiko mzuri wa lukaku na yule beki wenu lindorf acha mahaba mkuu stock city ana squad kubwa kuliko man
Aaaah aaaah aaaah Stock City wana Norma player while Man United tuna World Classic Player (Pogba), Top Players ( Matic,Valencia Lukaku, Martial, Herera) na Normal players wa kutosha.

Kuna tofuti kubwa sana kati ya Stock na Man Unite.

Welcome Alex Sanchez. No 7.
 
Duuuuh hii picha jamaa kama analia hivi. Utashangaaa mikosi ndy kwanza imeanza man utd tena upya. Kulazimishwa kuondoka 7bu ya mtu mwingn kuja ni kushushwa heshima. Mbn mi naona jamaa haja drop sana kivile ila muda zaid wa kucheza ungemtengeza upya!! Basi amuuze na lukaku ambaye ni mzito hadi kugeuka tu anachukua mwezi. Unaccepted to mikhi but pains to him na mimi. Sanchez anaeza asifanye lolote pale Man utd. Lets wait and see.
 
Tatizo LA Mou ni kuwanyima Uhuru wa chezaji uwanjani. Hilo ndo limefanya wafikie pabaya na Mkhtaryan. Na kuna kipindi hata Martial alishakata tamaa akaomba kwenda sevilla kwa mkopo. Kwa kifupi some times mou huwatumia wachezaji Fulani ktk nyakati Fulani si kwa matakwa ya moyo wake Bali ni kwa sababu hakuna namna. Na anapopata suluhisho,haijalishi huyo mchezaji yupo form au la anamuweka kando kupita kiasi. Rejea Herrera msimu ulopita mpaka tukasema itabidi awe captain.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…