Tukiiangalia Match ya Liverpool na Man City kuna vitu vingi vya kujifunza juu ya Match Ile iliyojaaa ufundi na msisimko wa aina yake.
Liverpool wametuonyesha udhaifu wa Man City, Man City hawana mabeki wazuri wala kipa, same as Liverpool lakini wana Striking force nzuri inayowafichia madhambi yao.
Tactically, zilikutana timu zenye Falsafa moja ya kushambulia muda wote wa Mpira, lakini Zenye madhaifu sawa upande wa Mabeki na Kipa.
Kushinda mchezo kulihitaji mbinu za Makocha binafsi, Kloop baada ya Match ametuambia alitumia mifumo zaidi ya Minne kuweza kupata ushindi Ule haikuwa kazi rahisi kuwasimamisha na kuwafunga City ya Pep Gurdiola.
Kosa kubwa alilofanya Klop ni kupunguza pressing force langoni mwa City kwa kuwatoa Salah na Mane' ili kulinda ushindi jambo lililoipa City nafasi ya kusawazisha magoli.
Ni makosa kujilinda mbele ya Viungo na Washambuliaji wa City, Gurdiola ni fundi katika Creativity eneo la 18 la timu pinzani, anawafanya akina De Bruyne, Sane na Silver kuwa ma ghost pale mbele, watakufunga ndani au nje ya 18 licha kuweka wachezaji zaidi ya Sita kuzuia.
Klop aligundua udhaifu wa City kuanzia safu ya Kiungo, ndio mana alitumia zaidi Mawinga/viungo wa pembeni wenye mbio.
Na goli la mapema la Chamberlain liliwashangaza City.
Tumemuona Gurdiola licha ya kutanguliwa goli zaidi ya tatu hakuwa na Pressure alibadilisha mchezo na kuifanya City kucheza mpira wake dakika 15- 20 za mwisho za mchezo na kufanikiwa kurudisha magoli mawili.
Strike force ya Liverpool haikuwa makini, wangeweza kushinda magoli zaidi ya Site kama wangekuwa na utulivu, Mane' hakuwa na bahati.
Pengo la Countihno lilionekana katika kiungo cha Liverpool na kazi kubwa ikahamia kwa Salah.
City nao kumkosa Silver kulifanya mfumo kutokuchezeka, wa pasi nyingi nyingi na fupi fupi kati ya Silver, De Bruyne na Sane hali iliyopelekea kutokuona makali ya Aguero.
Ukiangalia kikosi cha Liverpool, City na hata Chelsea hakuna timu yenye kikosi chenye mchanganyiko Mzuri kama Man Utd kwa sasa pale Old T.
Mourihno anatakiwa kubadilika na kuachana na mbinu zake kujilinda, anatakiwa kuifanya timu na wachezaji kuwa huru.
Man Utd ingekuwa chini ya Gurdiola tungekuwa tunaongea mengine muda huu.
Mfumo wa kujilinda na kukaba unafanya vipaji vingi kupotea au kufanya pale Old T.
Timu inakosa kasi na ari ya kushambulia, Mikhtaryan ndio huyo ameshapotea licha ya uwezo na kipaji alichonacho, A. Martial hayupo huru uwanjani na anabidi kutumia muda mwingi kulinda kuliko kushambulia.
Licha ya Shughuli ya Matic kuijua lakini hatuoni ile kasi yake uwanjani, Matic mwisho wake ni katikati katikati haruhusiwi kwenda kushambulia.
Wakati msimu uliopita ndio alikuwa moja ya Wachezaji waliokimbia Km nyingi, Mou anaua kipaji cha Any Hererra kwa kumtaka akabe kuliko kushambulia, Kabla Herera alikuwa kama Countihno wa sasa.
Kwa falsafa ya kukaba zaidi kunaifanya timu kukosa Ubunifu pale mbele, ni kweli tunashinda lakini katika mazingira magumu, hard football na sio Sexy football kama ya City au Barcelona.
Asili ya Man United ni kucheza soka la nguvu, kushambulia na la kasi kwa kutumia Mawinger zaidi.
Tete si za kusajiliwa Sanchez au Ozil nataka kujua Mourihno amekubali kubadilika, hawa akina Sanchez ni wachezaji wanaocheza soka wakiamini katika vipaji vyao na kasi ya timu.
Mourihno akibadilisha style na falsafa yake na kucheza soka la kushambulia na kasi muda wote, timu itafunga magoli mengi zaidi ya wanachokifanya City.
Timu ina upungufu wa Creative players kutokana na mfumo, kwa sasa ni Pogba tu, lakini kuna akina Mikh, Martial na Matta.
Asernal World Class Player alikuwa Sanchez na Ozil pekee timu ilikosa top players wengi.
Man United kuna mchanganyiko Mzuri.
Tusubiri Ujio wa Sanchez.