JESSE Lingard. Ndiyo, Jesse Lingard huyuhuyu unayemjua wewe. Ndiye, mchezaji ambaye yupo kwenye kiwango bora kabisa kuliko mastaa wote unaowafahamu wewe huko Ulaya.
Ni Lingard huyuhuyu ambaye mashabiki wa Manchester United hawamkubali sana. Lakini, ukitafuta ukweli na kama unapewa chaguo la kusajili mchezaji kwa sasa kwa kuzingatia ubora uliopo, ukiwekewa Lionel Messi na Lingard, hakuna atakayekushangaa ukimbeba Lingard. Hahahaha. Hii inahusu kiwango cha sasa cha mastaa hao wawili.
Kwenye mabao 14 ya mwisho yaliyofungwa na Manchester United, Lingard amehusika kwenye nusu ya mabao hayo, kiwango bora kabisa ambacho kinamfunika Messi hadi kuingia anga za mpinzani wake wa miaka yote kwenye soka, Cristiano Ronaldo.
Kwa kukusanya rekodi za mechi tisa zilizopita, Lingard amewaburuza mastaa wote wanaonekana kuwa bora huko Ulaya. Katika mechi hizo timu za mwisho, Lingard amefunga mabao saba na asisti mbili. Rekodi bora kabisa, ambayo hata Messi hazifikii, lakini zikimweka kwenye daraja moja na wakali kama Ronaldo, Neymar na mwenzake Kylian Mbappe. Cheki rekodi za mastaa wengine.
Jesse Lingard – mabao 7, asisti 2
Hii inaitwa usiyempenda kaja. Lingard si mchezaji anayeshabikiwa sana huko Man United, lakini ukweli utabaki palepale, ndiye mwokozi wa kikosi hicho cha Old Trafford kwa siku za karibuni. Lingard amekuwa kwenye kiwango bora kabisa, ambapo katika mechi tisa za mwisho alizocheza, amefunga mabao saba na kuasisti mengine mawili.