Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Duuh....na leo pia..!!! Bora hata ya De Gea
 
Burnley msimu uliopita hakuna tumu ya top 4 iliyochukua au iliyo mpiga nje ndani. Ngoja na huu msimu uishe tuje tuangalie record zao.

Mi hata sishangai ni mmepata kile mnachostahili.
 
Kujlinda kwetu khasa hii mipira iliyokufa bado inatupa taabu lukaku peke yake katoa assist 3 mbili tukafungwa na city moja ya Bournemouth walikosa. Jana lile goli akawa anautafuta ule mpira kama sindano vile nasisitiza ajikite zaidi mbinu za kujilinda anapokuwa karudi eneo hilo kwani ni sehemu ya majukumu yake. Watu mpaka wanaingiza imani kuwa Pogba akiwa nahodha basi majanga yanatutokea binafsi sidhani kama ni sahihi ni mchezo tu. Tunakosa sana magoli hilo lipo wazi kisha pana aina flan ya kunyimana pasi khasa Rashford ana ubinafsi na maamuzi ya kitoto pia.
 
Mm naona kama timu ina mgomo baridi kwa mbali.Watu hawataki Lukaku afunge wanamnyima pasi za kufunga.Sitashangaa kilichomtokea Mourinho Chelsea kikatokea Man U kama hatadhibiti wachezaji hawa
 
Kocha analipwa 388 ama kweli mtanyooka mwaka huu. Siku zote nawaombea njaa .
Jini linashikwa bila maombi tena kwenye himaya yake.
Timu ilishakufa long hiyo toeni mipira mjue ukweli muanze upya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…