Kabla ya kuelekea kwenye mapumziko Richarlison aligongesha mwamba baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliochongwa na Kiko Femina.
Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinatimia, United walikuwa mbele kwa magoli matatu kwa bila
Kipindi cha pili kilianza kwa Watford kufanya mabadiliko kwa kumuingiza mshambuliaji Troy Deeney ambaye alifanikiwa kufunga goli la kwanza la wenyeji kwa adhabu ya penati baada ya Marcos Rojo kumuangusha chini Roberto Pereyra kwenye eneo la hatari.
Dakika chache baada ya kupata goli la kwanza, Watford walipata tena goli la pili kupitia kwa Doucoure akimalizia mpira ambao ulishindwa kuokolewa vyema na walinzi wa United, wakati wenyeji hao wakiwa na matumaini ya kusawazisha, Lingard alizima ndoto yao kufuatia kufanya juhudi binafsi za kuwatoka walinzi wa Watford kisha kuweka mpira nyavunia.
Zlatan Ibrahimovic dakika za mwishoni kuchuka nafasi ya Lingard na kufanya kuwa mchezo wa 50 kwa Msedeni huyo ndani ya United.
Vikosi vilivyoanza Watford: Gomes (c); Mariappa, Prodl (Carrillo 58), Kabasele; Femenia, Cleverly, Doucoure, Hughes, Zeegelaar; Huges (Pereyra 58), Richarlison; Gray (Deeney 72). United: De Gea; Valencia (c), Lindelof, Smalling, Rojo, Young; Matic (Herrera 54), Pogba; Lingard (Ibrahimovic 88), Lukaku, Martial (Rashford 65).