Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Upenzi Kama Huu Wa Unstable-Fanboys Ndiyo Unaonifanya Kuna Baadhi ya Washabiki Nikawa Siwaquote...

Yaani Kuna Madogo Hapa Timu Yao inapkmuwa Katika Wakati Mgumu Huwa Huwaoni Wanatoweka...

Lakini ikishinda tu! Hao wanamiminika Na Kuwa Wasemaji na Watoa Pongezi Wakubwa Hapa...

Huo Sio Ushabiki!! Kumbukeni Kina Canavaro na Kina Zambrota Waliikimbia Juve! Lakini Trezaguet alishuka nayo Daraja na Akapanda Nayo Daraja...

Kwahiyo Hata Kwenye Wakati Mgumu Support Timu Yako...

Man City Kanipiga 5 na wala Sikuzikimbia Nyuzi...

BTW: Leo 4G naona mumeirudisha.. Namshauri Lukaku asali sana amuombee Pogba Asiumie..
 
Word,huu uzi wiki hii utakimbiza sana sababu ya ushindi wengi hawana uvumilivu timu ikifungwa au kutoka sare.
 
huLALI
 

Mkuu ulichoongea ni kweli kabisa, na mimi ni mmoja wao, timu ikifungwa hunioni humu, ila sio humu tu yaani jamiiforum nzima siingii hata wiki kwa jinsi navyokuwa nafeel. Mimi kwangu timu ikifungwa maumivu yake sio. So fans tunatofautiana, kuna wale wenye mioyo migumu wanaoweza kuvumilia aina yoyote ya matokeo, ila sie wengine timu ikifungwa hata hamu ya chakula inapotea itakuwa kuingia humu jukwaani wakati ukijua utakutana na kejeli za kina King Ngwaba Ollachuga Oc na wengineo???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…