Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Fellaini anapaswa kuwa definition ya uvumilivu na upambanaji. Ni ngumu kuamini ni msimu uliopita tu alikuwa anazomewa Old Trafford na mashabiki walitamani hata asiwe benchi. Leo hii tunalalama ameumia na hatumkumbuki Ander Herrera ambaye yuko available na ni mchezaji bora wa club wa msimu uliopita.

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
nawaomba radhi mashabiki wenzangu wa manchester united na nipo tayari kupokea adhabu yoyote kwa kosa langu nililolifanya kwa kuweka video isiyohusiana na thread hii.
  1. kwenye mechi saba za mwanzo tumeshinda mechi sita lakini bado tunaambiwa hatujacheza na timu kubwa lakini ukiwauliza ni timu kubwa gani hatujacheza nayo watakujibu Arsenal timu ambayo leo hii fundi denis bergkamp aamue kurudi tena uwanjani na umri wake wa miaka 48 bado kwenye kikosi cha kwanza atacheza.
  2. nilikuwa sijapata muda wa kuangalia mechi yoyote ya manchester city lakini nilibahatika kuangalia mechi yao dhidi ya chelsea na kiukweli walicheza mpira wa kiwango cha juu sana, ila nilichokigundua ni kwamba mchezaji mwenye kiwango cha Kelvin De Bruyne ndiye pekee tunayemkosa kwenye timu yetu, tunakosa kiungo wa juu mwenye maamuzi ya haraka kama de bruyne na ningependa japo baadhi ya mechi mourinho amjaribu juan mata kama namba 10 na awape nafasi antony martial na rashford waanze kwa pamoja.
  3. ni habari mbaya sana kuumia kwa fellaini wakati ambao yupo kwenye kiwango cha juu ila kwangu mimi pia ni habari nzuri kwa sababu nitapata kuona combination ya viungo wawili (matic + herrera) wenye uwezo wa kutembea na mpira uwanjani na kufika eneo la adui mara kwa mara, uwepo wa fellaini ni faida kubwa sana kwa timu linapokuja suala la kulinda lakini mechi zote tatu alizoanza tulizidiwa sana (rejea mechi ya crystal palace jinsi cabaye alivyotuvuruga, everton, southampton).ukijaribu kuwaangalia liverpool utagundua ya kwamba wana watu takribani wanne wenye uwezo wa kumiliki mpira hivyo basi naamini kama ataanza herrera itakuwa ni jambo zuri sana.
  4. niwakumbushe tu wapinzani wetu wanaosema hatujacheza na timu kubwa ya kwamba liverpool msimu uliopita takribani mechi zote kubwa alishinda lakini alishika nafasi ya 4, kuifunga chelsea, arsenal halafu ukafungwa au kutoa suluhu na west bromwich ni uwendawazimu, uwendawazimu ambao anafanya liverpool tu duniani tokea msimu 2008/2009.
  5. nimalize kwa kumtakia heri ya kuzaliwa mfalme zlatan ibrahimovic aliyetimiza miaka 36 siku tano zilizopita,kwa mujibu wa taarifa nilizo copy na kupaste ni kwamba zlatan ibrahimovic
  • ndiye mwanadamu pekee ambaye kama atatembelea nyumbani kwako basi wewe ndio utakuwa mgeni
  • ndiye mwanadamu pekee ambaye alimsaidia nurser wakati anazaliwa
  • zlatan ndiye mwanadamu pekee aliyezaliwa akiwa ni mzee lakini atakufa akiwa ni kijana
  • siku moja zlatan alichelewa kwenda shule lakini cha kushangaza mwalim aliwaadhibu wanafunzi wengine kwa sababu waliwahi mapema kuliko zlatan
  • pia kuna wakati alishindwa kuhudhuria skuli siku mbili mfululizo matokeo yake siku hizo zikaitwa jumamosi na jumapili
  • wakati graham bell anatengeneza simu mtu wa kwanza kumpigia simu alikuwa ni zlatan
  • kabla rais wa sweden hajafanya maamuzi yoyote lazima apate ushauri kutoka kwa ibracadabra
 
Martinez kocha wa ajabu sana. Belgium imeshafuzu WC anawachezesha watu kama Fellaini wa nini? Utafikiri hajawahi kuwa EPL club manager!
Pumbuvu sana huyo jamaaa, sasa jmosi no pogba no fella.......
Mkuu bonny zile stat zake zitaharibiwaa
 
Mshenzi sana huyo roberto, amemcheza fella ubeligiji bila sababu ya msingi.....
Nadhani waje waweki sheria za clubs kuwa zinatoa ushauri juu ya waajiriwa wao wakiitwa timu za taifa....
kukosekana mkuu fella kutatukost sana jmos pale anifield....
 
“I feel weaker without Fellaini in my squad, doesn’t matter if it’s on the pitch or on the bench. If his conditions are improved, he will be selected, I need him,” Jose
 
Watuache na mpiga tofari wetu #TUMEMPENDA_WENYEWE.
 
Marcus Rashford produced a brilliant piece of skill vs Lithuania

Rashford.


With England having already booked their place at the Russia World Cup after their 1-0 victory over Slovenia on Thursday, their match against Lithuania was a dead-rubber.

The Manchester United wonderkid played the majority of the match of the right wing and completely embarrassed the Lithuania defenders.
 

Scholes on management
While Scholes doesn’t appear to be any closer to becoming a manager, he has previously admitted he wants to be 100% committed when he eventually does.

"When I go into management, I want to do so with 100 per cent commitment," he said.

"At the moment I have a lot of responsibilities and things going on in my life that I cannot simply drop immediately.

"Most importantly I have a young family who need their dad around, having been away a lot during my playing career.


"There was no way, for example, I would ever have tried to combine a coaching job with my work on television."
 
Big Fella ni pengo lakini linazibika, nadhani Matic ndo habari akiumia.
Niongelee kuhusu Majeruhi na match tulizonazo this October.

Kwa taarifa zilizosahihi na zilizothibitishwa na timu tutakosa huduma ya Fellain kwa muda wa wiki 2 na Siku kadhaaa kwa maana hiyo hatohusika kwa namna yeyote kwenye game yetu na Liverpool,ni Pengo nitaeleza kwa nini?

Pia ni kweli hatutokuwa na Pogba kwa muda wa miezi miwili na siku kadhaaa hivyo atakosa match zote kubwa za round ya kwanza msimu huu ni pigo hasa nitaeleza kwa nini?

Inaonekana kuwa Majeruhi yameanza kuiandama timu yetu tukiwa tayari tumecheza michezo zaidi ya 10,tukielekea kwenye Peak,kumbuka Ligi ina jumla ya michezo 38,timu ndio inapanda mlima, ndio mana Mou analalamikia haya mapumziko ya Match za kalenda ya Fifa.

Eneo la kiungo limeonekana kuathirika,wachezaji muhimu wawili wanakosekana,Kila mtu anajuwa umuhimu wa Pogba katika kiungo cha Juu na kila mtu anafahamu Super sub Fellain katika kubadilisha na kutuliza mchezo katika eneo la kiungo.

Fellain amemuaminisha kocha kuwa yeye ndio Plan B,binafsi sifurahishwi eneo la kiungo kuchezwa na Fellain na Matic,hamna Chemistry,timu haichezi mpira katika kiungo na mara nyingi huwa tunazidiwa licha ya kushinda,tumeona game za hivi Karibuni,Fellain huwa ni mzuri anapokuja kama sub mana huja kutekeleza kile Mwalimu anachokitaka.

Tunaenda kupambana na Liverpool iliyovizuri katika eneo la Kiungo,Wana wachezaji wazuri Katika eneo la Kati,binafsi humuogopa sana Coutihno,lakini Coutihno huyu sio yule wa msimu uliopita,hana Furaha tena pale Liverpool.

Nimejaribu kusoma soma kuhusu Mou kuelekea match yetu na Liverpool,ameonesha kutokuwa na wasiwasi licha ya kuwa na Majeruhi, anaimani na kikosi chake,anafahamu ana watu wa kazi,ndio mana hatakiwa kuwazungumzia akina Fellain na Pogba ama Caric,Ye anawazungumzia waliofit sasa kuelekea kwenye mapambano.

Matic anatuambia tusiwe na wasiwasi timu itashinda bila uwepo wa akina Pogba na Fellain.

Tuna Under Herera,ambaye watu wengi walikuwa wanajiuliza hatma yake pale united licha ya uwezo mkubwa aliouonyesha last season kupelekea kuwa mchezaji bora wa Club.

Herera anaenda kucheza kiungo cha juu akisaidiana na Mata,Matic akicheza kiungo cha Chini.

Matic na Herera ni watu wa kazi,na vema wanakuja kucheza pamoja kipindi hichi ambacho tunatakiwa kucheza na Liverpool,Totenham,Man City na Benifica.

Kuna mpira flan hivi wa kasi na nguvu eneo la kiungo tuliumiss kwa muda,ule wa kama ule wa Man City vs Chelsea au ule wa Man U vs Chelsea last season,basi game yetu na Liverpool jumamosi tutashuhudia aina hii Burudani,watu wa kazi watawajibika.

Sina hakika kama Mou ataanza na Darmian au Young aliyonekana kucheza vizuri kama beki 3.

Nasikitika huyu muhuni kutokupona haraka Marcus Rojo.

Kwanini Mou hana wasiwasi,siri ni moja tu,Liverpool hawapo vizuri katika match hizi za mwanzoni,hawana kipa, hawana beki nzuri kulinganisha na Man united lakini vile vile strike force yao sio ya kutisha na kulinganisha na Strike force ya Man United,Man City kidogo ndio wa kuwachunga na kuchanga vizuri karata zetu.

Mou anafahamu kwa Liverpool hii haiwezi kuwazuia akina Mikhtaryan,Martial,Rashford, Lingard na Lukaku kutokufunga magoli.

Mou hana wasiwasi na beki zake,wametimia na hamna Majeruhi kinachobaki ni Tactics tu za kocha,Na Mou ni mzuri zaidi ya kocha wa Liverpool.

Binafsi siioni Liverpool ikiizuia Man United kupata ushindi ingawa mpira unadunda na kuna bahati lakini this season Man United tumejiandaa tuna wachezaji wa wastani wenye kupambana.

Shughuli ingekuwa pevu kwa Liverpool kama hawa wanaume wawili Pogba na Fellain wangekuwepo uwanjani Siku hiyo,Mou atakosa Super sub kwenye eneo la kati.

Pengo la Pogba litazibwa vizuri na Herera akishirikiana na kati ya Mata au Mikh.

Kukosekana kwa Super sub kutamlazimu Mou kuanza na Lingard ili Martial atokee Banch as Super sub.

Wachezaji wawili kwa Man United wenye uwezo wa kubadilisha mchezo kwa sasa basi ni Fellain na Martial.

Ndio mana nimeagiza Supu nyingine ya ulimi hapa kwa Mangi niliposikia Aserne Wenger anamtaka Anthony Martial,nikishushia na Coca-Cola ya Baridi.

Nasubiri Match ya Man United vs Man City nitatoa Uchambuzi wangu hasa juu ya kiungo cha Man City.

Ila kwa Match yetu inayofata jumamosi basi mashabiki Wenzangu tuondoe shaka na tuvae jezi zetu,tuwahi kwenye tv zetu na kulipia ving'uzi vyetu,hutakiwi kukosa game yeyote ya Man United kama unataka furahi huu msimu,Mou hajawahi kuniangusha.

Man United 3 - Liverpool 1.
 
Kweli mkuu umenena...Mimi ni mmoja ya watu ambao nilikuwa namwona kama ni mchezaji ambaye hastaili kuwa pale united ila kwa kweli msimu huu katuprove wrong...

Hope atarejea soon
 
Anthony Martial on the other hand has only started one game this season in the Premier League under United gaffer Jose Mourinho.

He has lost his place in the France squad, but regular games in Wenger’s team will put him back in the frame for Didier Deschamps' team.

But the Gunners will have to meet Manchester United's asking price of £50 million for them to have the opportunity of luring the Frenchman to the Emirates when the January 2018 transfer window opens.

Spanish side Barcelona are also reportedly interested in the signing of Anthony Martial, and the Catalan giants are expected to submit a bid in January 2018.

Earlier, NAIJ.com had reported of what Manchester United boss Jose Mourinho told Anthony Martial to do for him to keep his place at Old Trafford.
 
Bei yake watajuta kuulizia huyo mchezaji! Wataambiwa 100£
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…