Ongera Man u mwendo wa dozii....
Kidogo tu kilichoonekana...
...... Walichokikosa Everton ni Romero Lukaku wao tu kumalizia kazi nzuri ya kikundi cha viungo( Davies, Sirgudson, Gana na Shneiderlin). Bado Wayne Rooney mchezo huu ulimhitaji kucheza kama second streker zaidi kutokana na aina yake ya uchezaji.
Baada ya ule mguu wa Valencia kwenda moja kwa moja ndani ya nyavu za Jordan Pickford. Na kabla ya Everton kuutawala mchezo eneo la kiungo katika mchezo huu. Romero Lukaku alishindwa kuweka mipira miwili ya wazi kwenye nyavu za Jordan Pickford. Pamoja na ubora wa Lukaku kwa hivi sasa lakini bado anatatizo la kuzitumia vizuri nafasi zote zinazopatikana, na katika mchezo huu nafasi mbili za wazi akibaki yeye na kipa alishindwa kuzitumia.
Kipindi cha kwanza mchezo ulikuwa chini ya ulinzi wa Manchester United, Nemanja Matic na Marouane Fellaini waliwafanya viungo wa Everton kukubali kuwa wageni pale OT. Maumbile ya viungo hawa wawili wa Manchester united yalifanikiwa kuwatisha viungo wa Everton na kumfanya Rooney kushuka chini na kuongeza nguvu katika eneo la kiungo.
Baada ya kuanza kwa kipindi cha pili hapo ndipo Ilikuja Everton mpya tofauti na ile ya first half. Half time team talk iliwasaidia sana vijana wa Ronald Koeman.... Idrissa Gana, Tom Davies, Morgan shneiderlin na Glyf Sirgudson pamoja na ongezeko la Wayne Rooney katika eneo hilo la kiungo, kuiliwafanya Manchester united kupoteana katikati mwa uwanja na kuukabidhi mcheo wote kwa Everton. Kama sio umahiri wa Davide De Gea basi hesabu za Everton zingekuwa bora katika wakati ule wa umiliki wa mchezo. Pengine pia ni pamoja na kupungua kwa umakini wa Nahodha wa zamani wa mashetani wekundu hao Wayne Rooney, ndiko kuliko sababisha kushindwa kwake kupeleka mipira miwili ya wazi mbele ya de gea.
Baada ya Ronald Koeman kuona amefanikiwa kuufanya mchezo kuwa mgumu, na sasa akaamua kuingiza watu wa kufunguka ili kusawazisha goli. Kumtoa Wayne Rooney mtu aliyekuwa ameongeza wingi wa watu katika eneo la kiungo ilikuwa ni nafuu kwa united. Lakini pia kumtoa Idrissa Gana pamoja na Tom Davies wanadamu ambao waliwafanya viungo wa Manchester united kupoteza mipira muda mwingi na kuwaingiza Kelvin mirales, Calvert Lewin na Sandro Ramirez watu ambao wanakwenda na plan mpya ya kufunguka kutoka katika mpango kazi wa awali wa kulizima eneo la kiungo lote.
Bado tunatakiwa kumuombe Mtalii wa Tanzania Ronald Koeman kuendelea kuishi pale ili Msimu ujao aje tena katika utalii.
Huu ndio ule Msimu wa kuvuna ulichopandaa....