Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Nimeangalia match kati yetu na Real Madrid na nimeona chambuzi nzuri humu na Mkuu@ubarnGentleman umeongea vema hasa ulipowazungumzia Lingard,Matial na Matta.

Kwa kifupi, tumecheza na kufungwa na timu bora kwa sasa ulimwenguni, Madrid wamekamilika kila idara.

Sababu kubwa ya kufungwa kwetu ni timu kukosa uzoefu, Kikosi chetu ndio tunakiunda kufikia ubora wa Madrid, wachezaji wetu wanahitaji kucheza pamoja kwa misimu mitatu au zaidi kuwa na ubora wa 99's

Kulikuwa na mapungufu makubwa Sana kwenye eneo la Beki yetu pengo la Baily na Rojo lilionekana dhahiri kabisa, nilionesha wasiwasi wangu katika eneo hili mapema.

Lakini kama wengi wetu tulivyotegemea tumeona kuimarika kwa eneo la kiungo, Matic ameongeza kitu katika eneo la kiungo, Chelsea nadhani sasa wanajutia juu ya maamuzi yao. Jamaa amepiga mpira mwingi mno basi tu kazi yake imeshindwa kunogeshwa na Pogba

Kazi nzuri kwa Matic, De gea, Fellain, Lukaku,Rashford,Herera na Valecia wameonesha kitu even Darmian

Lakini nasikitishwa na uwezo wa Pogba bado kuna shida kama tutaendelea kuipanga timu kwa kumuangalia Pogba, pamoja na gharama ya fedha alizonunuliwa Pogba anatakiwa kudhihirisha ubora na uwezo wake ndani ya Man U kama anataka kuwa mfalme wa Oldtraford, bado ana deni kwa mashabiki wa Man united.

Kwa kiasi kikubwa kufungwa kwetu kulitokana na poor performnce kutoka kwake, alishindwa kudrive timu katika eneo la mbele, akawapa kazi kubwa akina Herera, Lingard, Mikh na Lukaku.

Sasa nakubaliana na wengi humu kuna umuhimu wa kusajiliwa kwa Winger @Perisic kwa ajili ya kudrive timu

Ama tuanze kuwaamini Martial na Matta katika wingi ya kushoto na kulia.

Ni rahisi kocha kuipata first eleven kwa Madrid lakini ni ngumu kwa sasa kupata first eleven kwa urahisi kwa Man United, hasa eneo la kiungo kama Pogba hatobadlika.

Tunahitaji Match zaidi ya 10 - 15 kujua kikosi chetu cha kwanza.

Tuone mabadiliko ya kikosi chetu leo tukicheza na West ham.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pogba jana kacheza vizuri sana,wao na Matic waliwexa kuhakikisha timu inacheza na mipira inafika mbele. Najua mnamuogopa Pogba sana ndio maana tukifungwa lazima mumuongelee.
Kwanza mmewai kucheza Super Cup?
Hapana napingana na mashabiki wenzangu wa Man U, jana Pogba alikuwa katika kiwango kibovu zaidi tulivyotegemea angalia maoni ya wachambuzi wengi kuhusu Pogba katika Match ya jana.

Hakuwa katika kiwango chake, wengi tulishangazwa kutolewa kwa Herera na kuachwa Pogba uwanjani.

Pogba ni mchezaji mzuri akijitambua na akiacha Kuridhika na kujiskia, anakosa Moyo wa Cr7 katika kupambana.

Bado sio wa kumtegemea katika Match kubwa au kubadilisha matokeo tunapohjtaji kufanya hivyo.

Match ya Madrid alicheza hovyo mno, hadi sasa ni Match na Chelsea old T ndio alionesha angalau nusu ya uwezo wake.

Anatakiwa kubadikika kama anataka kweli kuwa Mchezaji bora wa Dunia na mfalme wa old T.

Vinginevyo Mou anatakiwa kuanza kumuweka banch ili kumpa changamoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Unashangaa ni kwanini Herrera alitolewa na Pogba akaachwa uwanjani? Kweli uliangalia mechi? Uliangalia jinsi Herrera alivyokua mbovu uwanjani? Yule Herrera aliecheza dhidi ya Madrid sio Herrera wa msimu uliopita.
Herrera wa mechi ya Madrid alikua mbovu sana na ndie aliesababisha eneo la katikati ya uwanja kupwaya. Na alivyoingia Fellain tukaweza kucheza kama timu kwasababu Herrera alishindwa kuendanana na kasi ya mchezo.
Pogba na Matic walicheza vizuri sana na sitosita kuwapongeza.
Halafu Pogba sio mchezaji wa kubadili matokeo kwasababu yeye sio namba 9,10,11 wala 7. Waliotakiwa kubadili matokeo nadhani uliona utumbo waliokua wanaufanya. Pogba apewe heshima yake ata kama mna chuki nae.
 

Mbona kikosi cha kwanza kinajulikana.

4-3-3
De Gea
Valencia
Bailly
Jones
Darmian
Matic
Herrera
Pogba
Martial
Micki
Lukaku.
Hiki ndio kikosi chetu cha kwanza na kinaweza kukupa matokeo mazuri kabisa.
 
Pogba n mzuri ila kuna muda anaacha kucheza mpira ili timu ipate ushindi yeye anaanza kucheza na wale wanaomdiss...hapa duniani ukitaka ushindwe anza kuwaridhisha wanaokudharau , tena uwaridhishe kwa nguvu...itakuchukua nishati nyingi sana.

Pogba anatakiwa akipata mpira apige chenga chache sana...au asipge kabisa iwap kuna nafasi yeye aangalie vijana wake wako wapi hasa wala watatu...wa mbele yake.

Napenda sana moto wa mikh yeye akipata mpira hana haja yeye ni kupeleka presha mbele ya timu pinzani, kwanza anaspeed kubwa pia uwezo wa kukimbia na mpra.

Alafu kingine Mikh anajitahidi sana kupiga mashoot golini anapofika karibia na kumi na nane ya adui...pia accuracy yake ipo nzuri , mie huwa naona ni mara kumi mchezaji apge shuti alafu kipa adake kuliko kupiga minazi kama ya pogba.

Pogba anapokuwa na golikipa, anakuwa hana sana umakini huishia kupga juu au kipa kudaka...hili tatizo analo sana rashford maana huwa anapiga huko huko ata kipo alipolalia.
 

Pogba na Micki kwenye umaliziaji hawana utofauti, angalia msimu uliopita walivyokua wanakosa magoli ya wazi.
Halafu tatizo lingine la Micki ni kushindwa kuficha mpira na kuanguka ovyo.
Mfano mechi ya Madrid alipata nafasi ya kupita kwenda kufunga lakini alinguka bila sababu yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…