Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Natoa pongezi kwa wanazi wote wa Manchester united kwa kuuvamia na kuusasambua Uzi wa Chelsea .... Hawatasahau Yale mashambulizi ya Jana kutoka kwa Kamarada Enock Mwigane (everlink) na Mwalimu Gashasha (Sister)


Naomba team hii ipewe ulinzi wa kutosha , Mwenye namba ya Simon Sirro anipatie ili tuombe ulinzi si kwa kuuvamia Uzi wa Chelsea namna ile


Sent From My Nokia Ya Tochi
 
 
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 06.08.2017
Barcelona wanajiandaa kupanda dau kumtaka kiungo wa Tottenham Dele Alli, 21, baada ya kumuuza Neymnar kwa pauni milioni 200. (Sunday Express)
Bayern Munich wapo tayari kutoa pauni milioni 50 kumsajili kiungo wa Tottenham Eric Dier, 21. (Sun on Sunday)
Arsenal, Liverpool, Manchester City na Barcelona wanamtaka kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21. (Sunday Mirror)
Manchester United na Chelsea wanafikiria kumsajili kiungo wa Barcelona Sergi Roberto. (Don Balon)
Chelsea wanaonekana kuwa tayari kupambana vikali na Manchester United katika kumsajili Gareth Bale kutoka Real Madrid. (Sunday Express)
Barcelona wapo tayari kutoa pauni milioni 120 kumsajili kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho. (Star on Sunday)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp tayari anapanga kutaka kumsajili Manuel Lanzini kutoka West Ham kuziba pengo la Philippe Coutinho. (Mundo Deportivo)
Antonio Conte amesema hana nguvu zozote za kuzuia Chelsea kumuuza Eden Hazard. (Sunday Mirror)
Barcelona wapo tayari kuwatoa Andre Gomes na Rafinha kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Paulo Dybala kutoka Juventus. (Gazzetta dello Sport)
Everton wataamua kumfuatilia mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck, 26, iwapo watashindwa kumshawishi Olivier Giroud, 30, kuondoka Emirates. (Sunday People)
Meneja wa Everton Ronald Koeman ana matumaini ya kumsajili beki wa zamani wa Arsenal Thomas Vermaelen, 31, kutoka Barcelona. (Sun on Sunday)
Arsenal wanaongoza katika mbio za kutaka kumsajili Lucas Moura kutoka Paris Saint-Germain. (UOL)
Real Madrid wamemhakikishia Gareth Bale, 28, kuwa bado ana nafasi katika klabu hiyo katika hatua ambayo pengine itawahuzunisha Manchester United. (Observer)
Chelsea wana matumaini ya kuwazidi kete Liverpool katika kumsajili beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26. (Evening Standard)
Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri ameiambia Chelsea kuwa “hawana nafasi yoyote” na kumsajili beki kutoka Brazil Alex Sandro, 26. (ESPN)
Swansea lazima walipe pauni milioni 13 ikiwa wanataka kumsajili tena Wilfried Bony kutoka Manchester City. (Sunday Mirror)
Meneja wa Borussia Dortmund Peter Bosz amesema hana wasiwasi kuhusu kumpoteza mshambuliaji wake Ousmane Dembele, 20, anayenyatiwa na Barcelona. (Metro)
Barcelona wanamtaka kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast Jean-Michael Seri, 26, anayechezea Nice, ambaye pia anasakwa na Arsenal. (Mundo Deportivo)
Matumaini ya Liverpool kumsajili kiungo wa Rennes, Benjamin Andre, 27, yamefifia. (Sunday Express)
Newcastle wanamtaka kipa wa West Ham Adrian, 30, ili kuimarisha safu yao ya makipa. (Sky Sports)
Mnunuzi ambaye bado hajafahamika kutoka China ameonesha nia ya kutaka kununua baadhi ya hisa za Manchester United. (Sunday Times)
Usikose kuungana nasi leo moja kwa moja kutoka Wembley kusikiliza mpambano wa Ngao ya Hisani kati ya Arsenal dhidi ya Chelsea. Kuanzia saa kumi alasini saa za Afrika Mashariki.
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa.
 
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 05.08.2017
Chelsea wameripotiwa kuwasiliana na Paris Saint-Germain kutaka kumsajili beki Serge Aurier, 24, huku kukiwa na taarifa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast anakaribia kujiunga na Manchester United. (Manchester Evening News)
Inter Milan wanataka kuwapiku Manchester United na Chelsea katika kumsajili beki Serge Aurier wa PSG. (Calciomercato)
Meneja wa Monaco Leonardo Jardim amedokeza kuwa Kylian Mbappe, 18, anayenyatiwa na Real Madrid, Manchester City, Barcelona na Arsenal, huenda akaondoka kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Independent)
Philippe Coutinho, 25, ameachwa katika kikosi cha Liverpool kitakachocheza na Athletic Bilbao siku ya Jumamosi kwa sababu ya jeraha la mgongo. Mchezaji huyo ananyatiwa na Barcelona ili kuziba nafasi ya Neymar. (Mirror)
Barcelona wamewasiliana na Borussia Dortmund kuhusu mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Ousmane Dembele, 20, ili kuchukua nafasi ya Neymar. (Daily Mail)
Ousmane Dembele amesema anakaribisha taarifa za yeye kuhusishwa na kuhamia Barcelona. (Metro)
Barcelona nao wamejiunga katika mbio za kutaka kumsajili winga wa Monaco Thomas Lemar anayenyatiwa na Arsenal. (L’Equipe)
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 32, amekiri kuwa angependa kurejea England, wakati akizungumza mahakamani kwenye kesi yake ya tuhuma za kukwepa kodi nchini Uhispania. (Cadena SER)
Real Madrid watafikiria kumuuza winga Gareth Bale, 28, kwenda Manchester United, lakini ikiwa tu kipa David De Gea atahusishwa katika mkataba huo. (Don Balon)
Gareth Bale amemuambia mchezaji mwenzake Luka Modric kuwa anataka kurejea England na kujiunga na Manchester United. (Don Balon)
Paris Saint-Germain baada ya kumsajili Neymar, sasa wanataka kupambana na Arsenal katika kumsajili kiungo wa Nice Jean Michael Seri, 26. (Metro)
Monaco wapo tayari kupanda dau la pauni milioni 45 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28. (Sun)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte imeripotiwa yuko tayari kumruhusu beki Andreas Christensen, 21, kwenda Inter Milan ili kubadilishana na winga Antonio Candreva, 30. (Tuttosport)
Kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater yuko tayari kuiambia klabu yake kuwa anataka kuondoka na kujiunga na Chelsea. (Mirror)
Chelsea wamekanusha habari kuwa Antonio Conte anamtoa kwa nguvu Diego Costa, 28, Stamford Bridge. (Independent)
AC Milan wanafikiria kumchukua mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Chelsea Radamel Falcao, 31. (Sky Sport Italia)
Kiungo wa Inter Milan Geoffrey Kongodbia, 26, anayesakwa na Liverpool na Tottenham, ameomba kuondoka katika klabu yake. (Gazzetta dello Sport)
Everton huenda wakalipa pauni milioni 50 ambayo itavunja rekodi ya klabu ili kumsajili kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27. (The Times)
Watford wanamtaka beki wa Liverpool Alberto Moreno, 25, baada ya Liverpool kukataa dau la pauni milioni 11 kutoka Napoli. (Liverpool Echo)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa
 
 
Kaka jamani niliaga nilisema kipindi hicho mnisamehe kikiisha nitajaa tele n nikasema tutaonana August !!!
Wataka kusema nilikunukuu vibaya? mbaya zaidi umeibukia kwa jirani ilaa kheri cha muhimu uzima pia hongera kwa mapumziko uliojipa sisi tuliendelea kutupia japo mbili tatu mpaka umetukuta hapa. Karibu sana our first lady endelea kuongoza jahazi letu.
 
Yale mashambulizi yalikuwa ya kuteketeza kabisa sio ya mchezo yale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…