Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Dah ila timu yetu Imeshabadilika tamaduni yetu ya fergie imeondoka itatuchukua miaka kama liverpool kuja kurudi tusifurahi tu haya mausajili mourihno siyo kocha

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Yani lingard ndio aje kuwa winger mahiri wa team yetu pendwa... Tuache ushabiki lingard hana uwezo wa kukabidhiwa wing ... Msimu mzima hajapiga hata cross 50 ....


Ndio maana mourinho kwa kulijua hilo anatafuta natural winger kama perisic ambae kwa msimu wa 2016/17 anepiga cross zaidi ya 100. Manchester kwa sasa hatuna natural winger, natural winger kama Ashley young hana uwezo ule aliokuwa nao miaka kadhaa nyuma.

Martial na Rashford kiuhalisia wanachezeshwa katika wing kwa kukosa viungo wa pembeni halisi lakini hawa sio Nafasi zao kiuhalisia...


Kwa aina ya uchezaji wa Lukaku anahitajika winger wa kumwaga majaro za hatari... Winger wa kukusanya kijiji..


Sent From My Nokia Ya Tochi
 
Hahahaaaaa....we Raphael hovyo kabisa. umenichekesha sana, wapinzani itabidi wapae tu ili kuvuka ukuta.....vinginevyo miguu hawana😀😀🙂🙂
 
Hahahaaaaa....we Raphael hovyo kabisa. umenichekesha sana, wapinzani itabidi wapae tu ili kuvuka ukuta.....vinginevyo miguu hawana😀😀🙂🙂
Kweli vile nenda utazame video yake kisha jiulize akiwepo Erick,Victor,Rojo, na Serge wapi mshambuliaji atapita !!

Usinisahau kwenye Baraza Jipya.
 
kwani Lingard ni Winger au Attacking Midfielder?
 
kwani Lingard ni Winger au Attacking Midfielder?
Umetumia lugha mbili tofauti lakini neno ni moja



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa hatuna Natural Wing,na vilevile hata Lingard na Rashford kiuhalisia ni Viungo washambuliaji ila kuwatumia natural wing inategemea na mifumo ya Kocha na Timu.

Kama ni Mfatiliaji wa Mpira utakubaliana na mimi kuwa mpira wa sasa umebadilika mno,Makocha wengi mafundi hawapendi kutumia mawinga katika timu zao,ni Makocha wachache sana wanaindelea na utamaduni huo kama Zidane.

Nishawahi kuandika hapa kuwa Mou sio muumini wa Mawinger hasa hawa Natural kama Ashley,ni muumini wa Viungo wa ukabaji na Ushambuliaji mana ndio wanaofiti katika mifumo yake.

Hawa Mawinger wanaopiga Cross now hawana nafasi,tunataka Mawinger kama Rashford,Lingard ambao kiuhalisia ni Viungo wa Ushambuliaji.

Hizi Cross zitapigwa na Mafull back ambao now ndio hutumika kama Wings.

Fanya analysis zako katika msimu uliopita uone kama tunahitaji Wings au Mou kama anahitaji kweli Wings.

Kwa michezo ya hizi match za majaribio tumeona angalau uelekeo wa Timu.

Na kwa mpira uliopigwa katika match na Man City nadhani Mou atakuwa na majibu mengi juu ya Mapungufu na aina ya timu aliyokuwa anaitaka.

Pale Mbele,weka 8 - Pogba,9 - Lukaku,10- Rashford,11 - Lingard,7 - Mikhityran,6 - Herera uone kachumbari.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawaza tofauti, kwa Lingard awepo Uan Mata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…