Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Screenshot_2017-06-06-21-06-43.png
 
Degea wamuache aende ,maana akiendelea kubaki atakuja kuondoka bure
Hivi kwann José hafanyi usajiri mapema au anasubri nn maana akiri ilikuwa kwa griezmann na tayari amekataa haondoki
 
Maoni yangu Juu ya Kipa wetu David De Gea.

Akili huwa na tabia ya kuchoka au kuzoea mazingira hivyo kuhitaji mazingira na changamoto mapya.

Akili ya David de Gea imeshachoka na kuzoea mazingira na changamoto za pale Old Trafford na hivyo kuhitaji mazingira mapya,ndio mana unaona katika match za mwisho wa msimu alianza kuwa nje ya mchezo na kufikiria uhamisho wake hasa baada ya Real Madrid kutaka kumsajili na Juu ya Mafanikio ya Real Madrid katika misimu hii miwili.

Hii inatokana na kuwa katika kiwango kuzuri pale Old Trafford lakini tatizo tuliokuwa nalo la kutokuchukua makombe katika misimu hii minne baada ya kustaaf kwa Kocha wetu mwenye mafanikio Sir Alex Fegurson ndio lililomfanya David de Gea kuyachoka na kuyazoea mapema mazingira ya Old T na hivyo kuhitaji changamoto mpya katika ligi nyingine.

Ni ukweli usiojificha katika misimu hii ambayo hatukuwa tukifanya vizuri ndio kipindi pekee ambacho De Gea alifanya kazi ya ziada kuzuia timu kutokupata matokeo mabaya Zaidi licha ya matokeo tuliyokuwa tunayapata lakini kwa kiasi kikubwa David De Gea alikuwa Imara langoni na kuchomoa mikwaju na michomo ya maana, ndio mana haishangazi kuona akichaguliwa kuwa mchezaji bora katika misimu hiyo ndani ya kikosi hiii ni kutokana na wachezaji wa ndani kutokufanya kazi yao ipasavyo/kutokuwa na wachezaji Wenye njaa na mafanikio pamoja na ubovu wa mbinu za makocha.

Kwa kiwango chake alichokionesha na kama tungebahatika kufanya vizuri katika misimu hii hasa kombe la ligi kuu na Uefa champion leo hii tusingesikia madai yake ya kutaka kuhama kwenda Madrid.

Now tuna Kocha wa Dunia anayejuwa mahitaji ya Timu na ni Kocha wa Makombe,Falsafa ya Mou ni kushinda Mataji popote anapokuwepo.

Mourihno anachotakiwa kufanya sasa ni kumjenga kisaikolojia David De Gea na kutengeneza mazingira ya kumuhakikishia juu ya kurudi kwa zama za makombe ndani ya Old T chini yake,kuja kwa wachezaji wa kiwango cha Dunia na ikiwezekana kumuongezea mshahara.

Nitafurahi kumuona David De Gea akiendelea kuwa nasi Next season hasa kipindi hichi tunachotakiwa kurudisha heshima Yetu kipindi hichi ambacho tumeanza kukisuka upya kikosi chetu.

Hivi De Gea kasema anataka kuondoka?
 
Degea wamuache aende ,maana akiendelea kubaki atakuja kuondoka bure
Hivi kwann José hafanyi usajiri mapema au anasubri nn maana akiri ilikuwa kwa griezmann na tayari amekataa haondoki
Ninachokiamini romero ni kipa mzuri sana pia,anachohitaji aaminiwe,afunzwe na apewe nafasi basi,Huyu de gea aachwe tu aende akapate anachokihitaji,natamani mourinho angefanya maamuzi kama ya fergie japo mara moja tu,mchezaji akizingua uza fasta.
 
Degea wamuache aende ,maana akiendelea kubaki atakuja kuondoka bure
Hivi kwann José hafanyi usajiri mapema au anasubri nn maana akiri ilikuwa kwa griezmann na tayari amekataa haondoki
Morata ndiyo dili kwa sasa hivi ila Real dau wanalodai ndicho kikwazo
 
Back
Top Bottom