Mechi ya Jumamosi itakuwa ngumu kupita maelezo.
Manchester ikitaka kushinda lazima ihakikishe sehemu ya kiungo inakamwatwa sawa sawa.Nina hakika Barcelona watakaa na mpira 70 % Manchester 30 % [Ball possession].Manchester watatakiwa kutumia vyema 30 % watakazo kuwa na mpira[Counter Attack] mashambulizi ya kushtukiza.Ngome ya Barcelona chini ya mkongwe Puyal na Pique ikipata mashambulizi makali ya wakina Chicharito na Rooney inapitika na kufungika.Sehemu ya kiungo ndio yalipo maneno haswa viungo wa Barcelona Xavi,Iniesta na Busquests ni engine na ndipo mipango ya ushindi inapofanyika Manchester United lazima wawe na mikakati ya kudhibiti viungo wote wa Barcelona kabla ya kumfikiria Messi.
Nategemea Manchester United itaanza na kikosi kifuatacho.
1. Van Der Sar
2. Rafael or Fabio kutegemea nani yuko fit zaidi ya mwingine
3. Evra
4. Vidic
5. Rio
6. Carrick
7. valencia
8. Anderson / Giggs kutegemea nani yuko fit kuliko mwenzake
9. Chicharito
10. Rooney
11. Park
Benchi awepo Nani,Smalling,Fletcher,Barbatov na Lindegaard
Ningependa Manchester watumie mfumo wa 4 5 1.