Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kocha wa Ajax Amsterdam Peter Bosz adai Mourhnio aache visingizio vya kuwa na ratiba mbaya ya mechi na wachezaji kuchoka

 
hivi bado nafasi ya sheikh yahya haijazibwa bado? nahisi inanifaa.
 
kwenye thread hii naamini miongoni mwa member wanayoifanya ichangamke ni Rutashubanyuma ila mimi kiukweli aina yake ya uandishi na uwasilishaji wake wa taarifa haunifurahishi japo kuwa anafanya kwa nia njema.

Mfano hapo juu taarifa ya tetesi ya usajili wa michael keane ametumia comment (ujumbe) zaidi ya tatu kwa ajili ya taarifa moja tu jambo ambalo lingewezekana kwa yeye kutumia comment moja tu iliyojitosheleza kuwasilisha taarifa yake.

Hii habari ya james rodriguez nayo ni vile vile ametumia comment zaidi ya 10 kwa ajili ya taarifa moja tu. hata ukijaribu kuangalia taarifa inayohusiana na reserve team ametumia comment za picha zaidi ya 7 jambo ambalo lingewezekana kwa kutumia comment moja tu kuwasilisha taarifa kuhusiana na mourinho kutumia wachezaji wa reserves katika mechi zilizobakia.

hata ile style ya uwasilishaji wa online match kiukweli ni jambo zuri sana unalolifanya kwani unawasaidia wale ambao wapo mbali na televisheni ila mimi ningefurahi zaidi kama ungelikuwa unaweka update kila baada ya dakika 10 na si baada ya dakika moja kama unavyofanya.
kiukweli aina hii ya uandishi huwa unanifanya niwe mvivu kuzipitia hizi kurasa(pages) ambazo sijazisoma comment zake.
ni mtazamo wangu tu naamini hutochukia kama yule jamaa (x)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…