Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Last time man utd kufungwa kama hivi walibounce back na kuchukua treble, hope lvg airudishe 4-1-4-1 huu mfumo mpya wameuzoea.

Mashabiki kuweni na subira msiwe kama man city na chelsea fan wanaofukuza fukuza tu makocha,

Kocha anatakiwa kufanya kazi timu ifanye vizuri,huwezi kuwa na subira kama timu inazidi kudidimia otherwise hali itakuwa mbaya zaidi
 
Nzi where are you, baba ukuje tukusikie mawazo yako

Ha ha ha! I'm speechless re what is happening. Ila mimi siyo muumini wa fukuza fukuza ya makocha. Na hata LvG akifukuzwa sasa nani atashikilia mikoba ilhali makocha wote wa maana wapo busy na msimu. Kwa mara ya kwanza nakubaliana na alichokisema MosDef kumpa Giggsy kuwa interim manager katika nusu ya msimu iliyobaki ni hatari kubwa sana. Bado hana uzoefu. Anapaswa kufanya kazi chini ya makocha wazoefu kama misimu miwili mitatu hivi, ndipo anaweza kufikiriwa kuwa manager kamili.

Kama alivyosema huyo Scouser, LvG anawafunga sana wachezaji kuwa huru. Na hii ndiyo staili ya United siku zote. Kama unakumbuka mwanzo wa msimu nilisema, mchezaji kama Mata akicheza kwa uhuru huku akisaidiwa na Herrera, ushindi haukosekani. Na kuna games LvG aliwaachia uhuru na matokeo yalikuwa mazuri sana.

Pamoja kuwa naumizwa sana na matokeo haswa mechi mbili zilizopita kwa kufungwa na vitimu vibonde kabisa, kumfukuza LvG kwa sasa hakutaleta tija zaidi ya mkanganyiko na timu kukosa mwelekeo.

Labda kama kuna mgomo wa wachezaji kwa kutopenda mfumo wa LvG au kutompenda LvG mwenyewe. Kama kuna mgomo na LvG kapoteza nguvu kama manager kwenye dressing room, basi hiyo itakuwa hatari na kutimuliwa itakuwa sawa kabisa. Maana ni hatari sana kama wachezaji wakiweka mgomo baridi.
 
Last edited by a moderator:

Ha ha ha....mashabiki wa #ManUnited tulikuwa tumeshachukulia poa makombe (take for granted)...na SAF alitu-spoil sana...sasa ni ukweli mchungu (na nimekuwa nikisema humu) kwamba kupata stability baada ya kuondokewa na kocha aliyekaa kwenye timu karibu miaka 30 siyo jambo la kitoto....ndiyo maana mimi siamini katika kufukuza makocha...nilisema hivyo wakati wa DM (leo kuna watu wanalinganisha LvG na DM, na kusema bora DM!!) na ninasema wakati huu wa LvG. Timu inahitaji kujengwa ili kuwa stable, uzuri katika soka la leo (mpira pesa) ni kununua tu wachezaji wazuri na kuwa-supplement na home-grown players, basi unapata timu ya ushindi....

Ngoja tuendelee kuona hapa itakavyokuwa...
 
Tukiendelea na Makocha wa dizaini hii...na league yenyewe ndio hii EPL naliona anguko la baadhi ya timu zinazojiita big4 na rise za timu kama Tottenham.... Leicester city....hata Crystal Palace wanaweza ingia hapo. ......
 
Real Madrid have scored as many goals in
90 minutes today as Manchester United in
their last 11 league games.

philosophy
 

Wenzio hili hawalielewi kbs
 
Real Madrid have scored as many goals in
90 minutes today as Manchester United in
their last 11 league games.

philosophy

Toka 2008/2009 miaka saba iliopita madrid wamebeba mara moja tu ligi ya kwao.

Kushinda 9 sometime pia hakuna maana kama mkikutana na timu nzuri mnapigwa
 
I can confirm LVG is to be replaced by
Jose Mourinho in the next 48 hours. ( duncane castle)

Please be true
Duh! Hapa Mbona Mourinho kaokota embe chini ya mnazi, alisemaga ndoto yake ni kuwa longterm coach wa Manu baada ya Fergie!
Nina uhakika kama hizi ni habari za kweli, Mourinho ataisogeza Manu!
 
Duh! Hapa Mbona Mourinho kaokota embe chini ya mnazi, alisemaga ndoto yake ni kuwa longterm coach wa Manu baada ya Fergie!
Nina uhakika kama hizi ni habari za kweli, Mourinho ataisogeza Manu!

Just a rumours bro, kwa hali ilivo pale utd kila mtu atataka kuongea lake ili avute attention ya watu na kupata kick, ila class of 92 ndio wanampigia sana chapuo mou kwamba aje kufundisha, but sioni van gaal akimaliza msimu huu akiwa bado kocha wa utd, next game britania stadium hatuchomoki
 
Hiyo haiwezi kutokea kwasasa. Hapo atapewa Jose Mourinho kwa sharti la kuwatumia wasaidizi waliopo ili Giggs apewe baada ya miaka 3 hivi.

Mpaka sasa sioni sababu ya kumtimua LVG zaidi ya watu kupanic
 
Jamani tunafungwa had na vishorwe vya Norwich City..! C matuc sasa?.....Lisa Van Girl OUT !!!
 
Wacha awe sacked tu kitaeleweka mbele kwa mbele...

Ku sack sio solution....mwaka wa pili huu mna makocha wawili

Liver wameshafukuza sana makocha mpaka kesho wako Unga

Asee haya tupo hapa, ila kumbuka nilichokwambia kuwa Zama zimepita zimepita, so sasa wawe makini hii hire and Fire itakula

#LVGIN
 
Kwa hii performance ni ngumu kumaliza top 4, huu ulikuwa msimu wa kupigania ubingwa

Top 4 mnaweza ingia tena saafi kbs

mlichonacho mmepush "Panic" Button

Kuingia ni kusaka point kuanzia 65 kupanda....kitu ambacho mnaweza

sema mpaka mbadilike na inawezekana kbs

Afu Belo ubingwa unaosema ni upi? mmenunua wachezaji 7 msimu ulioisha wengine kadhaa....kupata hata First Eleven ni Ngumu, ukiachia mbali Stability, akija mwingine nae atafumua fumua timu atengeneze yake (itachukua tena msimu mzima)

asee haya tupo hapa.....Mfano uchukueni kwa Real madrid wamefukuza makocha wengi wamenunua wachezaji wengi sana ila miaka yoote hiyo LA LIGA MOJA tu

UCL moja toka 2007
 
Last edited by a moderator:
Ku sack sio solution....mwaka wa pili huu mna makocha wawili

Liver wameshafukuza sana makocha mpaka kesho wako Unga

Asee haya tupo hapa, ila kumbuka nilichokwambia kuwa Zama zimepita zimepita, so sasa wawe makini hii hire and Fire itakula

#LVGIN

Tutapambana mkuu siyo lazima wote tupitie kupotea huko,ila juhudi nayo inalipa tutakaa Sawa tu......halafu leo tupumzishe buana jamvi la tanga tushalianua hili tumelipeleka Anfield angalia nawe lisikukute.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…