Pepo linaloikumba Jezi namba 7 lishindwe na lilegee na kutokomea kabisa,kwa Depay likae naye mbali kabisa,wote tuseme Amen......
Ukitaka kuangalia sana, Baada ya Ronaldo kuicha jezi hiyo, wengi waliokuwa wakipewa ni Wachezaji ambao walionekana tayari ni maarufu kuanzia kwa Owen, Valensia mpaka hivi majuzi kwa De Maria.
Wachezaji, Mashabiki na Timu nzima ya Man U walijenga matuamini makubwa kwa wachezaji hao kutokana na umaarufu wao na namba ya jezi waliyokabidhiwa. Matokeo yake tunaona ni wachezaji hao kucheza Underpreassure kutokana na matumaini makubwa kwa Mashabiki na Wachezaji wenzao waliyojitwisha.
Hii ni tofauti kidogo na jinsi Alivyokabidhiwa Ronaldo jezi hiyo toka kwa Beckham, maana Ron alikuwa hafahamiki kwa yeyote, Mashabiki wakamuona Feggie chizi kwa kumkabidhi jezi maarufu mchezaji asiyefahamika na ambaye kiwango chake hakijulikani. Achia mbali umri wake mdogo..!!
Kwa muktadha huo, Ukiangalia kiwango cha Depay na namna alivyotua ndani ya Team na jinsi alivyoaminiwa haraka haraka na Wachezaji wenzake, Bechi la Ufundi na Mashabiki kwa ujumla, Namuona Dogo akienda kutoboa chini ya jezi hii. Hii kwanza ni kutokana na waliovaa jezi hii tangu kwa Ron, hakuna aliyeperfom kiasi cha kumbebesha yeye matumaini makubwa kama waliokuwanao Mashabiki kwa wachezaji waliopita wakivaa jezi hii. Hapa ninahakika Dogo anaenda KUTOBOA... tusubiri.
Nikija kwa sala yako, let me say Amen.
BACK TANGANYIKA