Tatizo mlipowafunga liverpool na man city mlidhani mmeshakuwa juu ya timu zote kiufundi na post nyingi humu zinaonyesha mlijiamini sana japo kocha wenu hakuwahi kujiamini kivile mbele ya watu wa darajani. Mnashindwa kujua kuwa aliyekuwa na pressure ya kushinda ni man u wala siyo chelsea! Mwenye shida ya kushinda alikuwa na jukumu la kushambulia! Lengo la Chelsea lilikuwa kutokupoteza mchezo kwa maana ya kufungwa, Hivyo tactics zililenga kuvuruga mipango ya malengo yenu msiweze kufunga. Ball possesion haikuwezeshi kufunga kama haikusaidii kutengeneza nafasi nzuri za kuweka mpira wavuni. Jiulize swali, kama ulikaa na mpira kwa asilimia 70, ulikuwa unafanya nao nini? Chelsea walikuachia uchezee mpira ili mradi tu unauchezea kwa namna ambayo hautaleta madhara! Kama kwa mfano ungebahatisha kufunga goli la kuongoza usitegemee kuwa ugeachwa ukae na mpira kwa kiasi hicho. Morinho alipoona mbinu zake zinafanikiwa hakuwa na sababu ya kubadili game plan. Kubalini kiwango cha kocha wenu hakifikii kile cha "special one" pia wachezaji wenu walio wengi bado sana kiwango. Ndio maana mkiwa na majeruhi timu nzima kuanzia kocha, wachezaji mpaka mashabiki wote mnaanza kulialia! Sisi Costa ni majeruhi na kila mtu anajua ni mchezaji muhimu lakini kocha halilii bali anapanga mbinu za kiufundi za kushinda mechi bila yeye! Poleni na jipangeni!