Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Naiona Manjesta yanited ikishika mkia au nafasi za mkiani kule UCL msimu huu

Mancity ya pep msimu juzi walishika nafasi za mkiani

Kwa Manjesta hii yenye Kiungo Bonge Santos ,na mabeki kina Heaven sioni wakitoboa

Kwanza mnapewa wale Top Tier wawili ,watawalamba

Mnapewa wawili kutoka pot 2 , watawalamba

Wanabaki wanne kutoka pot 3 na 4 , hapo mtashinda mechi 2 na draw 2

Huku EPL mshatepeta


Kucheza mechi kila baada ya siku 3 na kikosi chenu finyu ni ngumu sana

Mara ya mwisho mlishika mkia mbele ya Copenhagen ya Norway vijijini na Galatasaray yenye wazee wastaafu
 
Manchester united wanakaribia kumsajili kiungo wa brighton carlos baleba. Huyu bwamdogo siyo player mbaya ila injury record yake kwa msimu uliopita ilikuwa inatisha, nafikiri ndiyo maana man utd walidanda kwa midfielders wengine.

Kabla ya kufanya sajili huwa scouts na boards wanafanya analysis ya mchezaji wanaemtaka interms of perfomance,injury records,intensity ya mchezaji kulingana na falsafa za klabu, pamoja na price.

Carlos baleba alikuwa na injury record mbaya na hii inanipa mashaka kama atakuwa na fitness ya moja kwa moja kutokana na kukosekana kwake uwanjani mara kwa mara, technical bench wanatakiwa kuhakikisha wanaboresha kiwango cha bwamdogo santos kwasababu dogo naona ana fitness sana kuliko baleba, ili baleba awe kama backup.

Man u wanafanya huu usajili kwa kuondoa lawama tu, bora wangeenda kutoa £70 kwa manu kone angalau ungekuwa usajili wa uhakika zaidi.
 

Attachments

  • 1787132553041.jpg
    95.7 KB · Views: 1
Ukiachana na kuwa injury lakini performance yake overall ilikuwa ni mbovu ya msimu uliopita sijui management ya man u wamezingatia Nini mpaka kutoa hiyo hela
 
Ukiachana na kuwa injury lakini performance yake overall ilikuwa ni mbovu ya msimu uliopita sijui management ya man u wamezingatia Nini mpaka kutoa hiyo hela
Sasa hivi transfer market iko inflated sana kiasi kwamba mchezaji wa thamani ya £40 anaweza kuuzwa kwa £70+ si kwasababu ya quality na performance ya mchezaji bali kwasababu ya trending. Mfano ni matheus fernandez

Sasa ukija kwa baleba msimu wa 24/25 alikuwa na perfomance nzuri labda sokoni angekuwa na thamani ya £60-65, lakini kwa msimu jana kwa hiyo price ya £65 ni kama man utd wamefanya kubet ila kiwango chake hakikuridhisha kabisa, wangeongeza £5 wamchukue yule manu kone ingekuwa bomba sana, yule manu kone angeoperate kama prime bisuma yule wa spurs, man u kwenye midfield wangekuwa hawashikiki.
 
Mashabiki wenzangu tuache lawama. Baleba ni premier league proven huwezi mfananisha na Kone. Wachezaji wengi kutoka Italy wamekuwa wakiflop premier mfano Damian, Zerzkee, Pogba, Hodjlund na wengine wengi.

Baleba ndoto yake ni kucheza utd na inawezekana hakucheza kwa moyo baada ya club yake kumbania kuja utd.
 
Eeh hapo ndio ukweli bana, Man U ndio timu pekee inayoweza kukufanya ucheke Jumatatu asubuhi na Jumamosi jioni uwe unalia 😂😂 Lakn naona hii msimu wanaanza ku-cook tena, ten Hag amepata kikosi kinachomfaa sasa. Bolton game jana ilikuwa ngoma kweli, wale vijana wadogo walicheza kama walikula nyama choma kabla ya mechi. Hata hivyo bado napo nasubiri tuzione dhidi ya big teams, hapo ndipo tutajua kama kweli tunarudi. kweli
 
Blaza shida ni bei yake . Soma hapo 60 yenyewe wanasema haitoshi.
 
Mda utaongea.

Ila my point is mkiendelea na sajili za hivi sijui mtafika wapi.
Mkuu wewe timi gani kwani maan msimu uliopita Carrick kawaparaza big six wote na kikosi kile na alichukua point nyingi kulikobkocha yoyoye EPL maana yake tungefukuza Amorim mapema huenda tungebeba ubingwa, mpira sio maneno ni data.
 
Mkuu wewe timi gani kwani maan msimu uliopita Carrick kawaparaza big six wote na kikosi kile na alichukua point nyingi kulikobkocha yoyoye EPL maana yake tungefukuza Amorim mapema huenda tungebeba ubingwa, mpira sio maneno ni data.
Sikatai mafanikio ya msimu jana, na yasifanye upofu.

Kulikuwa na game ngapi kwa week ?Ilikuwa weekend mpaka weekend. Recovery time ilikuwepo. Msimu huu ni tofauti kaka.

kumbuka Msimu huu ni bandika bandua.
My point is ili kuchallange epl lazima uwe na squad depth mzee. Labda kama unataka draw za kutosha.


Mimi Gunners mkuu.
 
Mkuu wewe timi gani kwani maan msimu uliopita Carrick kawaparaza big six wote na kikosi kile na alichukua point nyingi kulikobkocha yoyoye EPL maana yake tungefukuza Amorim mapema huenda tungebeba ubingwa, mpira sio maneno ni data.
Hii ndio squad yenu kaka. Magoli mtapata shida itakuja kwenye kuyadefend.
 

Attachments

  • Screenshot_20260819_175026_Chrome.jpg
    105.8 KB · Views: 1
  • Screenshot_20260819_175014_Chrome.jpg
    114.5 KB · Views: 1
  • Screenshot_20260819_174958_Chrome.jpg
    111.5 KB · Views: 1
Sasa squad depth ndiobinaundwa msimu mmoja? Nyie iliwachukua misimu mingapi kupata hiyo squad depth?
 
Sasa squad depth ndiobinaundwa msimu mmoja? Nyie iliwachukua misimu mingapi kupata hiyo squad depth?
Ni kweli ilichukua misimu mingi ila kulikuwa na nidhamu ya usajili pamoja na malengo yanayo onekana.

Je malengo yenu ni yapi msimu huu? Kushiriki au kushinda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…