Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Siku ambayo Amorim atatambua timu aliyonayo haiwezi kucheza mfumo anaotaka nadhani atakuwa tayari amefukuzwa.

Na kwa hii nafasi anayomchezesha Bruno, muda sio mrefu Bruno ataanza kuonekana mzigo na ataenda timu nyingine itakayoweza kumtumia vizuri katika nafasi yake ya CAM na atauwasha moto kama Scott.
 
Fikiria City hii mbovu hivi imetugalagaza hivi, city wanavyocheza leo ni hovyo hovyo . Gurdiola nahisi hata yeye leo atashangaa amepataje goli zote hizi jinsi city ilivyo taabani hivi.
Sema hili Mbeumo hapa ni uwekezaji mzuri.
 
Hahahahaha
Mkuu mbona umekata tamaa hivyo?


Si mlisema tatizo ni Onana?
 
mimi nina uhakika manjestaa itakuwa bingwa mdimu huu, uwezo huo mnao, nguvu mnazo, kikosi kikali macho, kochi mnaye, yani full mkoko 😄😄😄
 
niliwahi sema humu ......

Huu mfumo hautakaa ufanye kazi kwa wachezaji wale wa manutd na EPL hii ya sasa.....ni mfumo mgumu kuuelewa kwa hawa wachezaji waliopo pale.....

Kama hawezi badilika huyu ,ataliwa kichwa kabla ya November .....tupo hapa.
 
niliwahi sema humu ......

Huu mfumo hautakaa ufanye kazi kwa wachezaji wale wa manutd na EPL hii ya sasa.....ni mfumo magumu kuuelewa kwa hawa wachezaji waliopo pale.....

Kama hawezi badilika huyu ,ataliwa kichwa kabla ya November .....tupo hapa.
Huyu simuoni akiwa pale kwa miezi mitatu mbele, kocha hatakiwi kuwa mbishi. Kocha mzuri anaangalia wachezaji alionao na anatafuta mbinu za kuwafanya wawe bora.

Amorim anakuwa kama mwanafunzi aliyesoma kwa kukariri mfumo mmoja tu katika mafunzo yake ya ukocha.
 
Hii system ya kusema kuweka mabeki wengi kulazimisha wacheze sio positions zao, tutaendelea kufungwa na timu nyingi, especially timu za kingereza
 
niliwahi sema humu ......

Huu mfumo hautakaa ufanye kazi kwa wachezaji wale wa manutd na EPL hii ya sasa.....ni mfumo magumu kuuelewa kwa hawa wachezaji waliopo pale.....

Kama hawezi badilika huyu ,ataliwa kichwa kabla ya November .....tupo hapa.
Hata abadilishe mfumo, hatuna quality players wakutupa cha maana. Angalia vikosi vya washindani wetu wakubwa ulinganishe na sisi, tuko hoi. Msimu huu timu zifuatazo hatuwezi kuzifunga labda kwa bahati tu,
Liverpool
Arsenal
Bournemouth
Sunderland
Spurs
Crystal Palace
Chelsea
Newcastle
Fullum
Man city( japo naye yupo hoi, ila mechi zote atatuchalaza)

Bado zile zinazokaza kweli kweli kama, Aston Villa, Brighton, West, ham, Brentford.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…