fuentte
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 3,210
- 9,206
Kwa jinsi Man Utd tunavyoingia dirisha la usajili imekuwa ngumu sana kubashiri tutasajili kwa kuboresha au kufumba macho washabiki. Ila kama tutasajili kwa uzingatia mapungufu yetu ya msimu ulioisha, nadhani idara zote 3 zinahitaji maboresho walau mchezaji mmoja mmoja. Ingawa idara ya ushambuliaji inahitaji maboresho zaidi pamoja na kiungo.Mkuu hivi usajili wa united unaweza predict nini maeneo tutasajili dirisha hili
Idara ya ulinzi inaweza kusubiri msimu ujao au dirisha dogo kama italazimika sana maana kwa hali yetu hatushiriki champions league hivyo tumekosa mvuto kwa wachezaji wazuri. Pia tukifanya usajili mzuri wa eneo la kiungo, automatically kwa asilimia kubwa hata eneo la ulinzi litaimarika.