Wewe tulia hapohapo na kama una jero mfukoni agiza Pepsi baridiii, tunataka tuwaonyeshe burudani na kuwafundisha Chelkenge namna ya kubeba kombe kwa kupiga comeback katika dakika za lala salama.
Raha ya kubeba kombe kama hili ni vile dakika zinakaribia kuisha na mashabiki wanakua wameshaanza kukata tamaa halafu ghafla unawanyanyua mashabiki kwa shangwe la hatari, hua inaleta msisimko wa hali ya juu sana.