Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hii saa 12 as uh Man U iko live


Kuna mida sisi tukiwa tunaendelea na majukum leo wao watakuwa vitandani.


Bets ni noma
 
Yoro nje wiki 12
Rasmus nje wiki 6

Kwa Upande wangu Hizi Taarifa za Majeraha ni kama Nimependa Muda Zimejitokeza.

Pre-Season, Mwaka Jana Mainoo aliumia kwa Mechi aina hizi, Mbadala akaletwa Mwishoni tena kwa Mkopo Amrabat! INEOS Imeweka Uongozi kwa kufikia sasa Unajitahidi.

UTD inamhitaji sana De Ligt Sababu ndo kwanza ana Miaka 24, Ameanza ng'aa tangu ana miaka 17! Uzoefu wa timu ya Kumiliki Mpira {Ajax}, Kuzuia {Juventus} na Kushambulia {Bayern} Kifupi amekomaa. Atakuwa ni Kiongozi mzuri sana kwa YORO ili asiingie kwenye timu na Pressure. Haya Majeraha yanatoa taswira inabidi uwe na Kikosi kipana chenye Ubora.
 
Nakubaliana na hoja yako mkuu.
 
Tunaibomoa nyumbu kutokea kwa nyuma,

daktari mkuu wa nyumbu katokea arsenal ata mwezi haujafika tangu aanze kazi
Injuries: Yoro, hojlund, rashford
 
Katika injuries zote 4, inayoniuma zaidi ni ya Hojlund tu, wengine naona imetokea wakati sahihi ili kutokufanya mambo kwa mazoea alikokuwa nako Erik. Ninaamini Yoro tutapata mbadala kabla dirisha halijafungwa. Ila Rashy na Anthony wapumzike kwa amani kwa sasa kwanza.
 
AMAD anamuaibisha ERIK
Sure, nilisema hapa kipindi cha nyuma makosa makubwa sana kwa Erik ten Hag msimu uliopita hakutumia silaha mbili kuanzia raundi ya 2 yaani Sofyan na Amad.

Erik amekuja kushtuka mwishoni kabisa na hata sasa hivi INEOS wasifanye makosa ya kiufundi tunamhitaji sana Sofyan Amrabat bila kujalisha Ugarte anakuja au lah. Tuna DM mmoja tu mpaka sasa Casemiro na yeye hadhaminiki muda wowote anaweza Kula umeme au pancha.
 
Fanya uchunguzi wako vizuri kuhusu national team ya Morocco. Noussair Mazraoui ni kama alivyo Matthijs de Ligt weakness zao kubwa they're susceptible to injuries ila wakiwa fit ni wachezaji wazuri sana.
 
Noussair Mazraoui, Matthitjs de Ligt & Sofyan Amrabat. Hapa at least timu itakuwa ime-balance. Ujio wa Sofyan inabidi uwe separately from original plan bila kujali kitakachotokea kwa Ugarte.
Sofyan Amrabat huyu huyu ambae msimu uliopita alikuwa mzito sana na anapoteza mipira kirahisi?
 
Kama kuna kosa kubwa sana la kiufundi tutafanya ni kuanza msimu rasmi tarehe 16 dhidi ya Fulham tukiwa na kiungo mmoja tu wa chini (Casemiro). Ugarte au Sofyan lazima mmoja awepo kikosini au wote.
 
Noussair Mazraoui, Matthitjs de Ligt & Sofyan Amrabat. Hapa at least timu itakuwa ime-balance. Ujio wa Sofyan inabidi uwe separately from original plan bila kujali kitakachotokea kwa Ugarte.
Noussair Mazraoui, Matthitjs de Ligt hawa jamani hawajahamia bado..hamjui tabia ya man utd ???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…