Manchester United (Red Devils) | Special Thread

vp, anafaa kwenye viunga vya OT?..?
GASPERINI Project ya timu kama CHELSEA Itamfaa zaidi kwa sababu ya aina ya Wachezaji walionao. UTD Nadhani kiasili Nyota wake wengi wamekuwa ni WINGS, Nafasi ambayo kwa GASPERINI Haitumii kabisa.

Nje ya ETH, kama UTD inaangalia zaidi Mwalimu hakuna Perfect Fit zaidi ya KLOPP ila Haiwezekani. Chaguo Bora kwa aina ya Mpira wa UTD 'TRANSITION' ni Sebastian Hoeness maana anatumia Classic 4~4~2 ya Kushambulia kama UTD ya Miaka Yote na wanatumia Muda mchache sana kufika Goli la Mpinzani.
 
Haya
 
Gasperini Vs Alonso.

Dunia haimpi heshima kubwa huyu mzee.
Alonso ni hakuwa na plan B zaidi ya kutegemea bahati ya comeback tu.

Dakika 25 za awali zilitosha kumpa picha kuwa game plan yake ilikuwa imefeli.

Sikujua kwanini alimwacha nje Boniface, Patric Schick, Andrich na Odilon Kossonou.
 
Scouting ya UTD ipo Fresh sana ila watendaji walikuwa Hovyo. wale wa Holland walipendekeza TEUN tangu Yupo AZ Alkamaar tena kama DM na nyakati nyingine akiwa anacheza CB na alikuwa Nahodha.
OLE angekuwa Mzuri sana kama Mkurugenzi wa Michezo/Ufundi mana alikuja wakati wake.

EDERSON na SCALVINI nadhani kwa Timu ya Scouting ya UTD Italy wanaeza kuwa Moja ya wachezaji wanaotajwa sana kuwafatilia. INEOS sijajua utendaji wao utakuwaje ila wakianza na Sajili kama Hizi watakuwa kweli wapo Siriazi.
 
Teun Kopmeiners ni perfect fit ya mahitaji ya Ten Hag yeye na Bruno wanaweza kucheza vizuri.
 
Teun Kopmeiners ni perfect fit ya mahitaji ya Ten Hag yeye na Bruno wanaweza kucheza vizuri.
Sahihi! Ila TEUN Akicheza DM anatisha zaidi anakuwa kama MATIC.
Ila kwenda UTD naona Itakuwa Changamoto mana Arne Slot anamkubali sana na alikuwa Jeshi lake akiwa nao AZ ALKMAAR. Njia ya Kwenda LIVERPOOL inaweza kuwa Rahisi.

ATALANTA naona UTD ipambane zaidi na SCALVINI/EDERSON/SCAMACCA
 
Scamaca hapana na hawezi kuwa na impact
 
Scamaca hapana na hawezi kuwa na impact
SCAMACCA Mwangalie Upya! Anaweza Cheza kama Target Man.
SCAMACCA ni Hatari sana kwa Timu ya "Transition" anajua Cheza kwa kulipa Goli Mgongo na Ni hatari sana kwenye "KEY PASSES" Nadhani ana ASSISTS nyingi sana msimu huu na Nafasi kulinganisha na CF wengi.

kwa Uhitaji wa UTD, SCAMACCA Ni Chaguo Bora zaidi. Mwingine naweza Ona anafaa ni ZIRKZEE.
 
Scamaca? Unatania au upo serious? Timu inayohitaji kupambana na kina man city alafu target man anakua scamaca?
 
Nme kumbuka kule kipindi mme komaa na de jong nika cheka kwa saut ..utazani mko seriouse vile kwamba ange okoa jahazi
 
Alishindwa Westham
 
Scamaca? Unatania au upo serious? Timu inayohitaji kupambana na kina man city alafu target man anakua scamaca?

Alishindwa Westham
Countrywide UTD Tayari ina CF Mtoto HOJLUND Miaka 21. Pia ina kawaida Kuamini ACADEMY na Karibuni walau ACADEMY Ina majina ambayo yana Uwezekano kuingia Kikosi Cha Kwanza. ETHAN WHEATLEY Kama hatoki kwa Mkopo anahitaji watu wa Kujifunzia. Lazima Upate CF/SS Amesogea Umri na Profile tofauti na HOJLUND

SCAMACCA Kashindwa W/HAM Ila Majeraha ni sababu mojawapo. HALLER, TADIC, BLIND Kwa ETH alifufua Mpira wao wote. Kushindana na City si Lazima uwe na Kina Haaland. Unatengeneza timu Nzuri kulingana na Uhitaji wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…