GE2025 Mamlaka za maji kudaiwa kubambikia wateja bills imeanza kitambo, kwanini Samia achukizwe kipindi cha uchaguzi?

GE2025 Mamlaka za maji kudaiwa kubambikia wateja bills imeanza kitambo, kwanini Samia achukizwe kipindi cha uchaguzi?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mwizukulu wa Buganda

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2024
Posts
638
Reaction score
1,771
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akimnadi Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ndiye Rais wa Tanzania, ameelezea kuwa anasikitishwa na tabia ya baadhi ya mamlaka za maji kubambikia wananchi bili kubwa zisizo na uhalisia.

Najiuliza kwanini hatua za msingi hazikuchukuliwa mapema wakati malalamiko kama haya yamekuwa yakisikika kwa miaka mingi, kwanini iwe katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu? Au ni mkakati wa kisiasa wa kurejesha imani ya wapiga kura.

Hii ni i rushwa ya ushawishi kama njia ya kujipatia faida ya kisiasa

----


DKT. SAMIA ANACHUKIZWA NA UBAMBIKIZAJI WA BILI ZA MAJI KWA WANANCHI- AWESO

Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Pangani Mkoani Tanga na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeelekeza kuanza kutekelezwa kwa ufungaji wa Mita za Maji za malipo kabla ya matumizi (Prepaid) ili kuondoa tabia ya baadhi ya Maafisa wa mamlaka za maji nchini kubambikia wananchi bili kubwa za maji zisizoendana na matumizi halisi.

Aweso ametoa kauli hiyo leo Jumanne Oktoba 22, 2025 wakati wa Mkutano wa Mgombea wa nafasi ya Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Viwanja vya Kecha, Kinyerezi, Wilayani Ilala, Dar Es Salaam, akisema Rais Samia hafurahishwi na tabia hiyo yenye kumkandamiza mwananchi bila ya sababu za msingi.

"Ni haki ya Mwananchi kupata maji lakini mwananchi naye ana wajibu wa kulipia bili ya maji. Jambo linalomtesa, linalomuumiza Dkt. Samia ni kuona mwananchi anabambikiziwa bili za maji, hili halikubaliki hata kidogo. Nataka niwaambie wasoma mita, masuala ya kumbambikizia mwananchi bili ya maji hizo ni zilipendwa.

"Dkt. Samia maelekezo ambayo ametoa kwa DAWASA, maelekezo ambayo ametoa kwa Wizara ya maji sasa hivi tunapokwenda tunaenda kwenye luku ya maji, unalipa elfu tano unapata maji yako ya elfu tano.

... Kwa kumalizia Mhe. Mgombea wa kiti cha Urais, Jiji la Dar Es salaam mahitaji yake ya maji ni Lita Milioni mia sita na themanini na nne, uzalishaji wa maji kwasasa DAWASA ni lita Milioni mia tano na thelasini na nne. Tunajua mahitaji ni mengi kwenye miji ya pembezoni, wakati mwingine unakuta wanapata maji machache na ukimuuliza Mhandisi anasema ni kwasababu ya Presha, nataka niwaambie dawa ya Presha imekamilika na Dkt. Samia ananunua pampu nane za Bilioni 16 kuhakikisha maeneo yote yanapata huduma ya maji." Amesema Mhe. Aweso.
 
Kwa utatuzi wa shida za maji Tanzania, Aweso anafaa ku-act Hollywood.
 
Back
Top Bottom