Mamlaka ya wananchi juu ya kuchagua viongozi hasa nafasi ya rais katika katiba iweje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mamlaka ya wananchi juu ya kuchagua viongozi hasa nafasi ya rais katika katiba iweje?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by gidytitus, Feb 3, 2011.

 1. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mimi kwa maoni yangu ningependa bila kujali vyama vya siasa dini, kabila wala sura ya mtu, inapofikia kipindi cha uchaguzi mkuu, kabla viongozi hawajachukua fomu za kugombea nyadhfa mbalimbali hasa nafasi ya URAIS, wananchi tupewe nafasi ya kuwahoji na kuwapa maulizo ya kina haswa yaani Interview hao viongozi kwa njia za wazi wazi. Pia inapofikia kipindi mkuu wa nchi anaharibu afu anakuwa mbishi kujitetea kwa nini kaharibu, tuweze kuchukua hatua ya kumtoa madarakani kwa kutangaza nafasi ya mgombea mpya wa nafasi hiyo kwa kuzingatia sifa halali zilizotajwa na wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutoa matangazo kama matangazo mengine ya kuomba kazi yanavyofanywa! ukizingatia kuwa ofisi zote za nchi ni mali ya wananchi hasa ofisi ya Rais inawahusu wananchi moja kwa moja Sasa emu piga picha kama leo tungekuwa na uwezo na mamlaka hiyo kama Kikwete pamoja na wadau wake wangekuwa wanatufanyia huo ujinga wao, Eti wanailipa DOWANS mabilioni ya pesa bila hata ya kutuuliza sisi tuliowaajiri, tumekataa bado wanatumia ubabe, yan mpaka wanatuua waajiri wao, mi sijawahi kuona huu ukaudi na ukiburi wa wafanyakazi wa hivi!! Yaan wao kama ni kuharibu tayari washaharibu mno tena tangu 1995, na tangazo hilo ningependa liwe linatengenezwa kwa muundo huu!!
  TANGAZO LA KAZI!
  OFISI KUU YA UMMA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA INAPENDA KUWATANGAZIA KUWA BILA KUJALI CHAMA CHA SIASA,DINI,KABILA WALA SURA NA RANGI YA RAIA, OFISI INATAFUTA RAIA MWEMA ATAKAYEWEZA KUGOMBEA NA KUZIBA NAFASI YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. OFISI IMEBAINI NA IMEJIRIDHISHA NA KUWA NA USHAHIDI WA KINA NA WA KUTOSHA KUWA ALIYEKO MADARAKANI KWA SASA AMESHINDWA KUFUATA KANUNI NA TARATIBU ZILIZOWEKWA NA WANANCHI (na siyo nchi) BALI WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMESHINDWA KUKUKIDHI SIFA ZA KINIDHAMU NA ZA KIUTENDAJI KAZINI. HIVYO WEWE KAMA UMEKIDHI SIFA ZILIZOTAJWA HAPO JUU UNATAKIWA KUFIKA OFISI KUU YA UMMA (tarehe,na wakati inaoneshwa) ILI KUCHUKUA FOMU YA KUOMBA KUFANYIWA INTERVIEW NA WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA HATIMAYE URUHUSIWE KUCHUKUA NA KUJAZA FOMU YA KUGOMBEA NAFASI YA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
  Na ofisi hiyo itakayokuwa ikiangalia nyendo za kiutendaji wa ofisi kuu ya rais na mawaziri na ngazi nyingine za chini iwepo na ichaguliwe pia na wananchi mbali kabisa na Ikulu.
  Ndugu wadau wa JF nimeona nifanye hivi kwa sababu, walio wengi wetu hatujafahamu na kugundua kuwa tunayo mamlaka ya kubadili wafanyakazi katika ofisi zetu za nchi kuanzia juu mpaka chini pale tunaposhindwa kuona umuhimu wao kazini, tufahamu kuwa sisi ndo waajiri wakuu wa viongozi wote. Uzembe unaofanywa na wafanyakazi wetu serikalini ni kwa sababu sisi Maboss wao tumeridhika na utendaji wao, lakini sipaswi kuwalaumu ni kwa sababu nami pia nikiwemo tulifanya kosa wakati tunatunga katiba ile ya kwanza (ingawaje mi sikuwepo yumkini na wewe pia hukuwepo lakini babu yako alikuwepo), tukawapa nafasi nyingi za kujidai hao wafanyakazi kiasi kwamba wanafanya kila wanachokitaka wao wanapokuwa maofsini mpaka wanachati umbea live na kwa facebook wanapanga namna ya kuwafanyia birthday watoto wao, waume. wake. wapenzi, mashemeji, mawifi, wakwe, dah! mpaka mahoue girl na maboy!,wameamua kuweka vitanda 6x6 mpaka ofisini, mapenzi live mpaka kwenye kordo za kupitia!!? jamen, nyie watu!!!. huu muda watautoa wapi kama kweli maboss wao tutakuwa siriazi na ofisi zetu???
  Naamini hii ofisi ikiwepo, uovu na uzembe unaofanywa na serikali ya CCM ikiongozwa na kikwete hautakuwepo.
  Aisee wadau wa JF haya ndo mawazo yangu juu ya utengenezaji wa Mwongozo mpya wa nchi yaani katiba! Vipi mnasemaje hii iwepo??? au tuiboresheje? Jameni msinitupe niungeni mkono hii mambo iwepo km vipi tuwapatie vijana wetu makini 48 walioko mjengoni walianzishie mjadara moto moto ili lisichakachuliwe.
   
Loading...